Sioni Sababu ya Rais kuitangaza filamu aliyoicheza, Wizara husika zina Kazi gani?

Sioni Sababu ya Rais kuitangaza filamu aliyoicheza, Wizara husika zina Kazi gani?

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
4,153
Reaction score
3,800
Kwa uzoefu wangu wa awamu za Urais hapa nchini kuna jambo nimekuwa nikiliona. Hasa awamu za karibuni.

Nalo ni Viongozi wetu kutowaamini wasaidizi wao kwa mambo ambayo ni yakawaida sana.

Mfano ni huu wa Filamu ya Royal tour.

Kwa maoni yangu Mh. Rais ametumia muda mwingi kuielezea kwa Wananchi na manufaa yake, ambavyo kwa maoni yangu haikustahili.

Inatosha,angeacha ijieleze yenyewe au Wizara husika kama wanavyoonyesha mambo mengine kupitia Safari Chanel nk.

Hii itaepusha ulinganifu mwepesi wa yasiyotarajiwa na matarajio makubwa anayoyanadi Mh. Rais.

Hata hivyo,baadhi ya watazamaji wengi waliyoiona, wameshatoa maoni na tumeyasikia. Siyo kila anachofikiri kiongozi kuwa ni kizuri aweke nguvu kubwa ya hoja kikubalike bila kutoa nafasi ya anaowaongoza kijadili.

Mwl. Nyerere aliona maduka ya Ushirika ni suluhisho la wanyonge kupata bidhaa kwa bei nafuu. Alichukua muda mrefu kuyazungumzia bila ushiriki wa wananchi wa namna ya kuyaendesha.

Hata hivyo,Wananchi waliziona dosari na kukaa kimya kwa vile Rais keshasema ni mazuri na yana faida.

Wakuu wa Mikoa naWilaya nao waliombishwa wimbo wa Rais wao. Kilichotokea baadhi wanakumbuka.

Sina maana ya kupingana na wazo la Rais wetu kufungua Tanzania kitalii.
 
Back
Top Bottom