Sipati chaneli ya Russia Today kwenye Azam TV

Sipati chaneli ya Russia Today kwenye Azam TV

Hadi nyau wa Russia wanaisoma namba

Screenshot_20220303_101343.jpg
 
Labda azam wameitoa
Sio Azam kaitoa, imeblokiwa juu kwa juu
Wanamcheka North Korea na Cuba , kumbe na wao ni yaleyale tu, hii vita imewaumbua kweli , sijui kama watapata ujasiri wa kukosoa tena nchi zinazofungia vyombo vya habari.
 
BBC,Skynews,CNN wanapika sana habari linapokuja suala Russia na Ukraine.Kuikosa RT kipindi ni balaa kubwa vyombo vya magharibi vinatulisha habari za upande mmoja.

Nashauri tuandamane hadi ubalozi wa USA tukiwa na mabango ya kulaani kitendo cha kuminya uhuru wa habari.
Andamana Nije nikuminye pumbuu
 
Kweli nimeamini mabeberu sio watu wazuri... Aljazeera nao sasa hivi wanajimwambafy wamesahau trump alitaka kuwalima tofali la utosi, wamwsahau walifungiwa baadhi ya mataifa ya kiarabu eti sasa wanakenua kenua meno kuona RT imefungiwa...
 
Hapana, sidhani kama wanaipata kutoka DStv.
Fanya utafiti Azam wanaipata hiyo channel RT kutokea wapi, kama wanaipata thr DSTV, jibu lipo maana DSTV wameifungia hiyo channel na hiyo ndio inapelekea kutokuwepo Azam tv
 
Ndo media iliyokua inabalance habari ikiwa pamoja na CGTN ila sasa wameipiga Ban
Hazi balance habari aisee, wanachofanya wao ni kuwa tofauti na media za magharibi.

Mfano wa utofauti wao ni Russia watu wameandamana Putin katuma jeshi likawagonga na kutesa wapinzani media za west zikiripoti RT wanakuja na facts za hatari kupinga same kwa CGTN imebadilishwa jina makusudi kutoka CCTV.

Na marekani ikiua raia au blunders zozote za serikali ya marekani basi wazee wa propaganda RT na CGTN wataripoti hilo jambo mpaka kero
 
Kabisa nimehangaika sana kuitafuta kumbe wame mute hawataki tupate habari mpk nimeamua kustreem kwa gb 6 ili tu nimape RT TODAY naikubali sana kwa habari za uhakika ukizingatia mm ni mrusi mweusi
Vikwazo vilitangazwa na Ulaya vya kufungwa TV zote za Russia ikiwemo hiyo RT waliitaja kwa jina kutoonekana bara la Ulaya pia wanasema watafungia website zote za vyombo vya habari mitandaini
 
Wameitoa mpaka google,mwanzoni nilikua naipata website yao lakini kwasasa siipati kabisa!
Vikwazo mbona walihutubia kabisa kuwa watafungia vyombo vya habari vya Russia kutoonekana Ulaya na online
 
Back
Top Bottom