naona mnalishana matango pori na kuaminishana ujinga.
hakuna uhusiano wowote wa dstv na azamtv katika masuala ya channel.
iko hivi, azamtv inatumia satellite ya Eutelsat ambayo headquarter zake zipo paris ufaransa. kiufupi Eutelsat ni satellite ya mabeberu.
mlolongo wa channel zote zinazopatikana kwenye vifurushi vya azam tv, zinakufikia wewe mteja kwenye kiTV chako pale nyumbani, kwa support kubwa ya satellite ya Eutelsat.
kwa mantiki hiyo, linapofika suala la RT, azamtv hawezi kwenda kinyume na msimamo wa mabeberu ambao wengine ndio hao wamiliki wa Eutelsat.
kuna mawili, inawezekana azamtv wameiondoa RT kwenye chanel list ili kukazia misimamo ya mabeberu dhidi ya Russia, au Eutelsat wamei-block RT kwenye satellite yao.