Sipati usingizi usiku najikuta nafikiria matukio ya mchana

Pole sana...

Punguza mawazo, au kuwaza vitu ambavyo kwa namna moja au nyingine hutoweza kuvifanikisha...


Cc: mahondaw
 
Hewa ipo ya kutosha ni pazur ninapolala hapana shda kabxa
duh! mkuu hichi kiswahili chako sikipendi utanisamehe bure!,hivi hauwezi kuandika maneno ya kiusahihi..?
kumbuka mazoea hujenga tabia.
 
duh! mkuu hichi kiswahili chako sikipendi utanisamehe bure!,hivi hauwezi kuandika maneno ya kiusahihi..?
kumbuka mazoea hujenga tabia.
Natumia kifup cha mcng si nieleweke hamna haja ya kuandka lisentes liref liclokuwa na maana
 
Natumia kifup cha mcng si nieleweke hamna haja ya kuandka lisentes liref liclokuwa na maana

Umemaliza chuo hata hujui thamani ya lugha yako. Badilika katika hilo.

Kuhusu tatizo lako nakupa pole ila badili mfumo wa kufikiri mambo ukiyaangalia kwa uchanya.
 
Pole jaribu kutumia njia hii itakusaidia chukua bilinganya kata vipande vidogovidogo kiasi ambacho kitakutosha kula changanya na mayai moja au mawili ya kienyeji kaanga kwa pamoja tumia ndani ya wiki moja na ni mara moja tu kwa siku hakika utapata usingizi murua kabisa na ulete mrejesho hapa
 
Asante ntaleta mrejesho
 
Pole sana mkuu! Bilashaka ni matokeo ya jambo/mambo fulani ambayo yamesumbua saikolojia yako. Yawezekana ni mahusiano, uchumi n.k
Ushauri;
1. Tumia muda mwingi kufanyakazi/shughuli yoyote ambayo unaifanya
2. Fanya sala na maombi, soma neno la Mungu
3. Fanya mazoezi ya viungo kama vile kukimbia n.k
4. Epuka hali ya kujitenga yaani kuwa peke yako kwa muda mrefu
5. KWAMWE USI JARIBU KUTUMIA VIDONGE VYA USINGIZI AU KILEVI CHOCHOTE.
 
Asante my
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…