Sipendezwi na mbinu zinazotumika kuchochea hali ya wasiwasi kwa Tundu Lissu

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Kwenye sayansi ya tiba na saikolojia kuna kitu kinaitwa "anxiety" na "Post-traumatic stress disorder' au PTSD. Hizi ni hali zinazomkabili mtu baada ya kupitia tukio fulani linaloacha kumbukumbu katika saikolojia yake. Mtu aliye na tatizo hilo anaweza kupata kiwewe pale kichocheo fulani kinapotokea kinachoweza kumkumbusha ghafla tukio lake.

Siku hizi siyo mfuatiliaji sana wa siasa ila siku hizi mbili tatu nimeshuhudia matukio matatu yaliyotokea mahali alipokuwa Tundu Lissu yanayoniambia matukio hayo yametendwa makusudi ili kuangalia kama watapata reaction ya kisaikolojia dhidi ya Lissu wanayoweza kuitumia kumshambulia kisiasa. Nitaongelea specifically tukio moja kati ya hayo matatu.

Tukio hili ni wakati Lissu anahojiwa na kituo cha Clouds TV, kuna mtu alionekana na kusikika akivunja glass kwa nguvu eneo la nyuma ya alipokuwa amekaa Lissu na Lissu alionekana kushtuka kidogo. Sijui nini hasa kilichotokea pale ila kuna kitu kinaniambia tukio lile lilipangwa. Bahati mbaya kwa waliopanga lile tukio, pamoja na Lissu kushtuka alibaki na utulivu na hawakupata reaction yoyote mbaya inayoweza kuashiria kuwa Lissu anaweza kuwa na PTSD.

Siasa zetu zimekuwa chafu saaana ndiyo maana nimepoteza kabisa interest ya kuzifuatilia. Siasa zetu zimejaa unafki, machawa, wizi, ubadhilifu wa mali za umma, ujinga, ukosefu wa utu, uvunjifu wa sheria, udanganyifu na tumepoteza kabisa dira ya kitaifa inayozingatia kwanza uzalendo kwa taifa. Sioni ni jinsi gani tutarudi katika njia sahihi.
 
k
20250106_192816.jpg
 
mimi sio mtu wa siasa ila nimependa tu intelligencer ya mwandishi

hongera sana mkuu
 
Mbona unaechambua ugonjwa ndo unaonekana ndiye unayeumwa huo ugonjwa?!!! Sioni kitu zaidi uoga tu uliokujaa
 
Katika liletukio la Yule Msaidizi wa Lissu kuangusha zile Glass hakukuwa na hichokitu chakupangwa.Yule ni msaidizi wakaribu wa Lissu hawezi kupanga ujinga huo
 
Siasa zetu zimejaa unafki, machawa, wizi, ubadhilifu wa mali za umma, ujinga, ukosefu wa utu, uvunjifu wa sheria, udanganyifu na tumepoteza kabisa dira ya kitaifa inayozingatia kwanza uzalendo kwa taifa. Sioni ni jinsi gani tutarudi katika njia sahihi.
Haya yanafanywa na mawakala wa watawala na ni janga la kitaifa
 
Kwenye sayansi ya tiba na saikolojia kuna kitu kinaitwa "anxiety" na "Post-traumatic stress disorder' au PTSD. Hizi ni hali zinazomkabili mtu baada ya kupitia tukio fulani linaloacha kumbukumbu katika saikolojia yake. Mtu aliye na tatizo hilo anaweza kupata kiwewe pale kichocheo fulani kinapotokea kinachoweza kumkumbusha ghafla tukio lake.

Siku hizi siyo mfuatiliaji sana wa siasa ila siku hizi mbili tatu nimeshuhudia matukio matatu yaliyotokea mahali alipokuwa Tundu Lissu yanayoniambia matukio hayo yametendwa makusudi ili kuangalia kama watapata reaction ya kisaikolojia dhidi ya Lissu wanayoweza kuitumia kumshambulia kisiasa. Nitaongelea specifically tukio moja kati ya hayo matatu.

Tukio hili ni wakati Lissu anahojiwa na kituo cha Clouds TV, kuna mtu alionekana na kusikika akivunja glass kwa nguvu eneo la nyuma ya alipokuwa amekaa Lissu na Lissu alionekana kushtuka kidogo. Sijui nini hasa kilichotokea pale ila kuna kitu kinaniambia tukio lile lilipangwa. Bahati mbaya kwa waliopanga lile tukio, pamoja na Lissu kushtuka alibaki na utulivu na hawakupata reaction yoyote mbaya inayoweza kuashiria kuwa Lissu anaweza kuwa na PTSD.

Siasa zetu zimekuwa chafu saaana ndiyo maana nimepoteza kabisa interest ya kuzifuatilia. Siasa zetu zimejaa unafki, machawa, wizi, ubadhilifu wa mali za umma, ujinga, ukosefu wa utu, uvunjifu wa sheria, udanganyifu na tumepoteza kabisa dira ya kitaifa inayozingatia kwanza uzalendo kwa taifa. Sioni ni jinsi gani tutarudi katika njia sahihi.
Katika jamii yoyote kuna watu wanaofurahia matukio hasi na hilo kuwa sehemu ya maisha yao, kwakimombo wanaitwa pessimistic people,

Yaani Kuna binadamu wanaofurahia binadamu wengine wakipata changamoto
 
Katika liletukio la Yule Msaidizi wa Lissu kuangusha zile Glass hakukuwa na hichokitu chakupangwa.Yule ni msaidizi wakaribu wa Lissu hawezi kupanga ujinga huo
Nini kilitokea pale?
 
Back
Top Bottom