SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Hili nitalielezea kwa ufupi sana ila naomba ujumbe uwafikie wahusika na wawajibike.
Kuna haka kamtindo na katabia ka baadhi ya wanachama wa Simba, nimewahesabu wawili mpaka sasa ambao wana mtindo wa kujitokeza na kutoa taarifa za klabu ya Simba kabla ya taarifa rasmi kutolewa na klabu yenyewe.
Wa kwanza ni huyu anajiita "Aggysimba". Huyu nilishawahi kumsema kwa kucopy content zooote zinazotoka katika account ya Simba na kuziweka katika account yake. Jana niliposikia tetesi za kufungiwa kwa Simba nilipoanza kuangalia online kujidhihiridha kuhusu taarifa hizo nikakuta yeye ameripoti kabla hata ya klabu kutoa taarifa. Hili halijanifurahisha kabisa. Najua atakuwa alipewa za ndani labda na kiongozi lakini sijajua kiherehere cha kukimbilia kupost kilitokea wapi. Na mpaka sasa amelivalia njuga suala hilo utadhani ana maslahi nalo.
Wa pili ni huyu anajiita "Dr. Mohammed". Huyu huwa anaripoti taarifa za Simba hasa za usajili kwa mamlaka kabisa kama vile yeye ndiye msemaji mkuu wa Simba akitaja hadi gharama za usajili na mishahara ya wachezaji. Kajipachika msemaji wa tawi lake basi anajiona anaweza kuzungumzia habari za ndani za timu. Na huyu naye huwa anajipambanua kuwa na ukaribu na viongozi na sijawahi kuona wala kusikia akikemewa kwa tabia hiyo.
Naomba uongozi wa Simba uliangalie hili. Tusiwe kama klabu ya kihuni ambayo inajiendeshea mambo hovyo hovyo. Wanaokiuka taratibu au kuvujisha taarifa za klabu tuone wakichukuliwa hatua.
Ubaya Ubwela.