Kama ni taarifa iliyotoka mapema unashindwa nini kutaja hao waliopost mapema?
Narudia tena kwa mara nyingine maana ni kama hautaki kuelewa, shida niliyonayo ni yeye, mtu ambaye amejitanabaisha kama mshabiki mkubwa wa timu anayesafiri maeneo mbalimbali kuifuata timu (na inasemekana wanalipwa kufanya hivyo) kukimbilia kupost taarifa mbaya ya klabu kabla ya klabu yenyewe haijafanya hivyo. Kama hauoni hilo ni tatizo, basi akili zako na zake zinafanana.
Kumbuka hata page za CAF zilikuwa hazijapost taarifa hiyo kwa hiyo bado ilikuwa ni taarifa za ndani. Hakukuwa na ulazima wa kukimbilia kupost halafu baadae kujifanya umeumia saaana!