Sipendezwi na wanachama wa Simba wanaotoa taarifa za klabu kabla ya klabu yenyewe

Bado haujajibu swali. Unaposema ilipostiwa mapema, nitajie wapi na muda gani. Pia kama umeona Micky ni shabiki wa Simba kwa hiyo anakaushia habari mbaya, je huyo mwingine kwa nini hakusubiri kama mwenzake? Hiyo ndiyo hoja yangu ya msingi.
Acha kujifanya kila kitu wewe unajua mkuu,unataka nianze kukutajia watu ili iweje? Hiyo taarifa ilitoka mapema tu,Simba walikuja ku-clear the air tu....maana kulikuwa na mkanganyiko kwa mbumbumbu wenzio wengi.........kama una shida zako na huyo shabiki mwenzio sawa ila taarifa ilikuwa inafahamika mapema labda wewe uliko na access ya information ndiyo changamoto
 
Kama ni taarifa iliyotoka mapema unashindwa nini kutaja hao waliopost mapema?

Narudia tena kwa mara nyingine maana ni kama hautaki kuelewa, shida niliyonayo ni yeye, mtu ambaye amejitanabaisha kama mshabiki mkubwa wa timu anayesafiri maeneo mbalimbali kuifuata timu (na inasemekana wanalipwa kufanya hivyo) kukimbilia kupost taarifa mbaya ya klabu kabla ya klabu yenyewe haijafanya hivyo. Kama hauoni hilo ni tatizo, basi akili zako na zake zinafanana.

Kumbuka hata page za CAF zilikuwa hazijapost taarifa hiyo kwa hiyo bado ilikuwa ni taarifa za ndani. Hakukuwa na ulazima wa kukimbilia kupost halafu baadae kujifanya umeumia saaana!
 

Huwezi kuelewa,baki na unachokiamini
 
View attachment 3203999
Huwezi kuelewa,baki na unachokiamini
Sasa hiyo picha ndiyo ushahidi niliokuwa naulizia ama inahusiana vipi na mjadala huu? Mbona unafeli bwashee?

Mimi napenda kuwa challenged, nikadhani utaniletea taarifa ambayo nilikuwa sina ili unishawishi nibadili mtazamo wangu kumbe ni wale wale tu.
 
Kuna watu wanaopenda kusikia matokeo hasi, (pessimistic)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…