Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Habari wadau,
Kuna jambo moja linakera ila naona wengine kama wanaona ni vizuri kwao, sasa inanifanya nijiulize nina matatizo au vipi. Ni kuhusu kupeana vitu na watu, hasa nyumbani na majirani. Sitaki Jirani anipe vitu vyake wala sitaki aniombe vya kwangu, labda awe ametokewa na shida ya kweli. Vitu vyenyewe ni kama vyakula, vifaa vya ndani, n.k
Aisee kuna nyumba za kota tumehamia mimi na wife hapa, kuna majirani wana roho nzuri lakini naona hii ni too much, wanapenda sana ku-share vitu, yaani kuna siku moja atamuita wife wakapike chakula cha pamoja, siku nyingine mwingine atapika chakula kisha atuletee wakati sisi tumeshapika, siku nyingine atawaambia mumpakulie kwa kuwa yeye hajisikii kupika siku hiyo, wakati mmepika cha size yenu pekee.
Kuna mmoja juzi katoka mkoani kaleta mazagazaga mengi kampa wife, sasa siku hiyo ndio natoka kunununa vyakula vya wiki nzima nakuta friji imeshajaa, sasa na wao unakuta siku wanakuambia gesi imeisha tunaomba tutumie jiko lenu.
Wife nishampiga marufuku kuomba ama kuchukua vitu kutoka kwa majirani lakini imekuwa mtihani kukataa na yeye akiwapa vitu kesho naye atakuja kuomba kwenu, hii inaharibu ratiba na bajeti kwani mimi ni mtu ninayependa kupangilia kila kitu changu kwa usahihi.
Naona ni kama tunalazimishana kuishi kijamaa wakati haya maisha sijayaozea kabisa, japokuwa nimekulia kijijini tulikuwa hatuombani vitu hovyohovyo, labda iwe imetokea shida ya kweli.
Sasa watu wengine niliowakuta hapa naona wanaiona ni lifestyle nzuri, najiuliza pengine mimi ndio nina roho mbaya ama hili linawakera pia baadhi yenu?