NYAMUHANZI
Senior Member
- Apr 7, 2017
- 187
- 389
Mkuu ninavyofikiria mimi ni kwamba maeneo ya jikoni hiyo ni idara inayomuhusu yeye moja kwa moja, majukumu yako yanaingia pale ambapo umepokea bajeti ya manunuzi ya vifaa vya jikoni....
Najua wajua lakini siyo mbaya kukumbushana. Kimsingi majukumu yote ya nyumbani ni ya Baba (Kiongozi mkuu katika familia) ila kwa kuwa Baba hawezi tekeleza yote peke yake ndiyo anatafuta msaidizi wa karibu ambaye ni mama na kumkasimia baadhi ya majukumu. Hivyo basi kumkabidhi jiko mke wako haina maana kwamba wewe hutakiwi kujua kinachoendelea huko jikoni. Ukiwa kama kiongozi unatakiwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kupata maoni na kutoa mapendekezo yako na kuchukua hatua pale unapoona mambo hayaendi sawa.
Siku zote mambo yanapoharibika sehemu yoyote wa kulaumiwa huwa ni kiongozi mkuu wa eneo hilo.