Sipendi kuomba wala kuombwa vitu. Je, nina roho mbaya au ni kawaida?

Sipendi kuomba wala kuombwa vitu. Je, nina roho mbaya au ni kawaida?

Mimi naona mwanaume Yuko sahihi kabisa Mimi binafsi staki mazoea hayo ya kuombana chumvi Mara ku share jiko sijui msosi huko Ni kutokujielewa tu na kuharibiana budget kwa kweli. Mimi mwenyewe nikiwa Sina hicho kitu siombi, maana omba omba huwa nikujizalilisha na ulizoea vya bure unalemaa, so Mimi siwezi subiri mwanaume anikataze naweza ku handle mapema tu hyo situation.
Ngoja na mi nijiseti mapema nikioa tu niwe na ka utaratibu kangu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi naona mwanaume Yuko sahihi kabisa Mimi binafsi staki mazoea hayo ya kuombana chumvi Mara ku share jiko sijui msosi huko Ni kutokujielewa tu na kuharibiana budget kwa kweli. Mimi mwenyewe nikiwa Sina hicho kitu siombi, maana omba omba huwa nikujizalilisha na ulizoea vya bure unalemaa, so Mimi siwezi subiri mwanaume anikataze naweza ku handle mapema tu hyo situation.

We Mwanamke una akili ya maisha, safi sana maelezo yako nimeyaelewa. Hivi umeolewa?
 
nikiwa form 3 kuna jirani yetu alihamia kwenye jumba lake pale mtaani,alikuwa anafanya kazi BOT nadhani,alikuwa akitoka kazini akifika getini anabonyeza tu rimoti geti linafunguka anaingia kwake hana habari na watu,haongei na watu wala hajishughulishi na shda za mtaa,ila kwenye michngo mkienda kuomba michango anatoa vizuri ila hashiriki,siku ya siku mkewe alipata ajali na mtoto ote wakafariki,msibani hakwenda mtu hata mmoja sema mtaa mzima tulimchangia around 1.8m,ambzo alipeleka mjumbe toka siku hyo alibadilika na kwenda kuomba radhi kwa kila nyumba na tinted alitowaga.Ishi na watu vizuri hasa mtaani kwako haijalishi unauwezo gani au mamlaka gani kwani siku yakikukuta hao ndo wakwanza kukusaidia
kweli aisee hii inanihusu mimi maana ni kauzu kweli kweli + sipendi mazoea na watu
 
mazoea yana tabu......itafikia hatua mnaanza kuazimanana wake na nguo za ndani kiroho safi tu mkuu,mimi sina roho mbaya ya kumnyima mtu kitu ninachokimudu ila sipendagi tabia za mtu kuyajua maisha yangu kiundani hasa mtu asiyekuwa ndugu wa karibu.una roho nzuri sana kama mh.
 
Brother, utakuja kufanya kitu ambayo itarefulekiti balaa, hama nenda mitaa ya Kishimba achana na kota.
 
Anyway haka katabia nyumban kapo na majiran ndo wamenilazimsha niwe naishi nao hvyo ingawaje sikapendi ngoja nikipige stop rasmi....ukauzu tu sahivi!
 
nikiwa form 3 kuna jirani yetu alihamia kwenye jumba lake pale mtaani,alikuwa anafanya kazi BOT nadhani,alikuwa akitoka kazini akifika getini anabonyeza tu rimoti geti linafunguka anaingia kwake hana habari na watu,haongei na watu wala hajishughulishi na shda za mtaa,ila kwenye michngo mkienda kuomba michango anatoa vizuri ila hashiriki,siku ya siku mkewe alipata ajali na mtoto ote wakafariki,msibani hakwenda mtu hata mmoja sema mtaa mzima tulimchangia around 1.8m,ambzo alipeleka mjumbe toka siku hyo alibadilika na kwenda kuomba radhi kwa kila nyumba na tinted alitowaga.Ishi na watu vizuri hasa mtaani kwako haijalishi unauwezo gani au mamlaka gani kwani siku yakikukuta hao ndo wakwanza kukusaidia
mzee wa chai kama kawaida yako!
 
Habari wadau,

Kuna jambo moja linakera ila naona wengine kama wanaona ni vizuri kwao, sasa inanifanya nijiulize nina matatizo au vipi. Ni kuhusu kupeana vitu na watu, hasa nyumbani na majirani. Sitaki Jirani anipe vitu vyake wala sitaki aniombe vya kwangu, labda awe ametokewa na shida ya kweli. Vitu vyenyewe ni kama vyakula, vifaa vya ndani, n.k

Aisee kuna nyumba za kota tumehamia mimi na wife hapa, kuna majirani wana roho nzuri lakini naona hii ni too much, wanapenda sana ku-share vitu, yaani kuna siku moja atamuita wife wakapike chakula cha pamoja, siku nyingine mwingine atapika chakula kisha atuletee wakati sisi tumeshapika, siku nyingine atawaambia mumpakulie kwa kuwa yeye hajisikii kupika siku hiyo, wakati mmepika cha size yenu pekee.

Kuna mmoja juzi katoka mkoani kaleta mazagazaga mengi kampa wife, sasa siku hiyo ndio natoka kunununa vyakula vya wiki nzima nakuta friji imeshajaa, sasa na wao unakuta siku wanakuambia gesi imeisha tunaomba tutumie jiko lenu.

Wife nishampiga marufuku kuomba ama kuchukua vitu kutoka kwa majirani lakini imekuwa mtihani kukataa na yeye akiwapa vitu kesho naye atakuja kuomba kwenu, hii inaharibu ratiba na bajeti kwani mimi ni mtu ninayependa kupangilia kila kitu changu kwa usahihi.

Naona ni kama tunalazimishana kuishi kijamaa wakati haya maisha sijayaozea kabisa, japokuwa nimekulia kijijini tulikuwa hatuombani vitu hovyohovyo, labda iwe imetokea shida ya kweli.

Sasa watu wengine niliowakuta hapa naona wanaiona ni lifestyle nzuri, najiuliza pengine mimi ndio nina roho mbaya ama hili linawakera pia baadhi yenu?

Mkuu ili wasikushtukie una roho mbaya hama hapo tafuta self apartment ambayo kila mtu na mambo yake, hata mimi sipendi kuomba wala kuombwa ombwa, ila nna huruma na wenye shida tena nimsaidie freely sipendi aje aniombe, sio vitu tu hata kuomba lift ya gari au pikipiki sipendi na mimi sipendi kuomba lift, hata mtu akiniona njiani na kujipendekeza kunipanlift namwambia nafika hapo mbele tu nshafika kumbe sipendi mavyombo ya watu hayo. Anaweza kupata shida njiani akakuomba umsaidie kutatua, tayari kisha kupotezea gape
 
Mimi naona mwanaume Yuko sahihi kabisa Mimi binafsi staki mazoea hayo ya kuombana chumvi Mara ku share jiko sijui msosi huko Ni kutokujielewa tu na kuharibiana budget kwa kweli. Mimi mwenyewe nikiwa Sina hicho kitu siombi, maana omba omba huwa nikujizalilisha na ulizoea vya bure unalemaa, so Mimi siwezi subiri mwanaume anikataze naweza ku handle mapema tu hyo situation.
Dah... umenikumbusha back in the days!! Sister angu wa ma'mkubwa kaachika wakati alikuwa anaishi na mdogo wake aliyekuwa anasoma day! Wakapiga hesabu huyo msichana akaishi wapi wakati anamalizia shule, wakaona aje kuishi home kwetu ambako by the time nilibaki peke yangu!!

Akaja kuanza maisha mapya!!

Wiki haijapita... sijui ilikuwaje kuwaje, nikatoka mlango wa nyuma ambako nilikutana nae tit-for-tat anatoka nyumba ya jirani, tena kupitia mlango wa nyuma! Nikashangaa kuona mtu ambae hata wiki hajamaliza, anatoka nyumba za watu! Ile kumuuliza, with confidence ananiambia eti alienda kuomba chumvi!!

Alinikera balaa!!!
 
Mimi naona sawa tu mwanaume siku akija anipe support huongeza upendo na urafiki, sisi kwetu wanaume wanajua kupika Tena chakula kitamu Sana ndio tulivolelewa so Mimi sioni shida ukiwa mwanaume siku moja ukapika kwa familia yako.
I can do anything with that lakini kukuna nazi, hapana aisee!! Hivi unapokuna nazi na zile mbuzi zetu za Uswahilini si lazima ujilegeze hivi huku unanesa nesa kwa madaha ya twiga anaetembea, au?! Au ni mbwembwe tu zile za akina dada wakuna nazi?!

Yaani hakuna ukombozi alionifanyia Bakhresa kama zile nazi zake... been asking myself what if kusingekuwa na zile nazi!!!
 
Mi kuombwa sina tatizo, tena huwa nafurahia kutoa kama ninacho lakini kuomba siwezi na sitaki!!!

Hata hivyo, kwa vitu vidogo vidogo kama vile vya jikoni, ukiniomba na kama ni kitu cha kuhitaji kurudisha basi nirudishie mara utakavyomalizia shughuli zako vinginevyo nitakususia jumla kwa sababu sina desturi ya kupiga hodi nyumba au milango ya watu!!

Kwa mfano mtu unaenda kuomba kisu, na unajua kabisa mtu hawezi kuwa na kisu zaidi ya kimoja; halafu unaomba lakini kurudisha hadi mwenyewe akifuate tena... wtf?!

Trust me, kama nitafuata mara ya kwanza, halafu ukachukua tena na ukabaki nacho, kitakachofuata hapo ni mimi kwenda kununua kingine ili nikuachie "kisu chako"!
 
Back
Top Bottom