Sipendi kuona mume wangu anakosa hela, huwa nampa hela, je inatokea kwa wanandoa wote?

Hiyo biashara ni ya mme wako au ya kwenu wote? Kama ni ya mme wako kwanini usiongee nae mkafanya pamoja?
Yeye akachangia nusu na wewe ukachangia nusu na wote muwe na maamuzi sawa kwenye hiyo biashara yenu?
Yote unayomfanyia haukosei na kama anarudisha na kutumia pesa kiungalifu haina shida kabisa.
 
Hongera kwa kufanya hivo
Upendo amani ni kitu cha muhimu sana

Mshauri afanye uchunguz kwa nin biashara yake haendi mbele
Kila wakati mnatop up mtaji....mtafute MTU wa mahesabu awashauri

.....pia ndoto zako ziweke wazi ili mfanye kwa pamoja
Hutakiwi kufanya kitu cha pekeako as uko kwenye ndoa

Kila LA kheri my.....pia jitahd kuepuka makundi mabaya ya kina Dada/mama ili uendelee na moyo huo huo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpendwa nimekuelewa vizuri ila naomba tu utambue kwamba hizi hela nampa mume wangu sizijutii na sijawahi kujutia kumpa na Mungu shahidi ninampa kwa moyo mmoja na ndani yangu nina amani.unaposema kumchoka mume wangu sijawahi kuwaza na sintakuja kumchoka inshort naonaga Mungu kanipendelea sana kunipa yeye.he is such a blessing to my life .kwenye maisha naamini katika amani na sio kitu kingine chochote hata kama hatuna kitu but as long as kuna amani mimi ndo kitu kikubwa kwangu.Hakuwahi nikosesha amani.pakiwa na shida mahali tunaweka sawa kwa upendo .yeye Ndio chanzo cha amani yangu ndo maana sitaki kabisa akose amani niko tayari kufanya kila ninaweza arelax.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye ndoa hakuna changu wala chako bali kuna chetu. Hongera kwa kufikia hatua hiyo kwenye ndoa, hiyo ndio ndoa ya mfano na ndivyo inatakiwa kuwa, hongereni momie.

Vv
 
Mpendwa nimemshirikisha hata kabla hatujafunga ndoa na anajua na kweli anajitoleaga but shida mimi ndo namshawishi kwamba afanye tu biashara yake ndo ya muhimu kwa sasa maana muda si mrefu watoto watahitajika kusoma na mambo mengi so yeye ajiweke tu vizuri mimi hizi za kwangu itafanyika tu nitajikusanya but priority iwe kwako kwanza.Anakubali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ni Upendo,
Lakin usiwe hivyo wakati wote....huyo mwanaume anaweza kufikir huna malengo wala akili yako haiwazi kujishughulisha,

Ni vizuri unapomsaidia lkn pia wanaume na ss tunajisikia vizuri tunapowasaidia mnapokwama kwenye shughuli zenu...

Anza biashara mama mshirikishe mumeo....jinsi wewe unavyosikia raha na furaha unavyomsaidia ktk biashara zake anapokwama ndivyo na yeye atakavyojisikia raha na furaha atakapo kusaidia na wewe.

Usibaki na hiyo furaha pee yako Emoj mpe na mumeo.

Mungu aibariki ndoa yako zaidi.
 
Acha ujinga wewe tengeneza dream zako, jamaa aki-dead( japo sikuombei) ndugu watavipurusa vyote afu hutajiona mjinga. Mwache mwanaume apambane mwenyewe
Unaongea usivyojua. Ndoa ikifikia hivyo ujue mwenza hana kitu peke yake, kila kitu kinamilikiwa kwa pamoja, wao ni mwili mmoja.

Vv
 
Mpendwa sijui umemaanisha nini kusema nimeoa but tumeoana.Upendo unetuleta pamoja na kila saa kila wakati nafeel upendo wa mume wangu kwangu.Kwa hakika ni mume haswaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja nikushauri kitu mamii though sijaolewa.......jifunze kuwa na akiba yako mwenyewe na kuwa na business yako kama mwanamke...kusaidiana haikatazwi ila not to that extent Cc Tuwaseme huyo ni mume wako inabidi awe anaumiza kichwa jinsi ya kupata hela na sio kidogo tu unampa hela hata kama hela hazina kazi kwa muda huu ila hapo baadae mtahitaji sana kutokana na matumizi yatakavoanza kuongezeka mfano school fees

Kingine kuwa na maisha yako sio unampa hela mwanaume tu hata kama kupenda sio kihivo yani unamaliza hela zako za bank kisa kumfanya awe na furaha.......

Siwezi kusema mengi ila wewe ni mtu mzima i hope utaelewa na kujirekebisha
 
It's true, sijui shida ni nini? Watu wamejichokea na ndoa zao, wanachofurahi kusikia ni matatizo ya wengine. If at all mtu alete mada ya kuonyesha kuifurahia ndoa, watu wapo so negative.

Nadhani ndoa zetu nyingi wala hazina furaha, wala hatuzifurahii, tupo tu kwa vile hatuna pa kwenda. Ndoa nyingi zimeshakufa, by reading some people's comments you can easily notice.
 
Mpendwa sio kwamba hanishiki mkono.kweli anatoa hela na ananipa ushauri but sipokei hela namshawishi sana hadi ananielewa pesa anarudisha kwenye mzunguko wa biashara zake.Na nakuwa na amani.yaani ni kwamba napenda sana yuko pale juu natamani sana.maisha yetu sio kiivyo so we still have a long way to go.akiongeaga tu kwamba mke wangu tumwombe Mungu tuwe smwhere mwaka fulani ndo nataka ifikie pale .nataka ile picha ya maisha anayotamani tuyaishi yatimie.Me ndio furaha yangu kuona tu anatimiza malengo yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanaume lazima wakusifie
life is for living kama uko happy that's is life
 
ngoja tuwasubiri wanandoa, but katika ndoa siku zote kumbuka hapo mnatimiza ndoto zenu pamoja ogopa sana kuwaza kuwa ww ndoto zako hazimii wakati hiyo miladi anayofanya mmeo ni ya familia.
Umenena vema mkuu,, kuwa na Amani kwny ndoa ni jambo kubwa sana ambalo kila mwanandoa anapaswa kumshukuru mungu..wanandoa wanatakiwa kuishi kwa kuwa na ndoto ya familia kiujumla na si kila mmoja kivyake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…