Carmel,
Hakuna mume/mke ambaye anapenda mwenzi wake atoke nje ya ndoa. Huo ni ukweli na inauma sana mtu akigundua kwamba mwenzi wake katoka nje ya ndoa.
Takwimu alizoweka Caren hapo juu zinasema wazi kwamba wengi hawajui kama wenzi wao huwa wana-cheat, huo ni ukweli. Wako wanao amini mke/mume hajawahi kutoka nje ya ndoa kwa kuwa hawajui. Na anaweza kusema mbele za watu kwamba mwenzi wake hajawahi ku-cheat! Temea mate chini dada yangu, shetani apitie mbali. Ninakupa mfano mdogo sana, kuna Mwinjilisti anaitwa Teddy Haggard, yule baba akihubiri ilikuwa ni upako kwa kwenda mbele. Siku maisha yake ya gizani yalipokuja kuwekwa hadharani, ilikuwa ni shock kwa waumini. Kumbe alikuwa ni ni shoga (anapanda mwanaume mwenzake), na alikuwa anatumia madawa ya kulevya. Sasa niambie huyo baba ambaye anaonekana kwenye TV kila siku na ana waumini karibu laki moja kanisani kwake, ilikuwaje asijulikane? Mkewe alikuwa anajua kwamba mume ni mlokole na mwinjilisti na hawezi kufanya madudu ya aina yoyote. Ndoa iliyumba, mke wa huyo baba ameandika kitabu akielezea kwanini aliamua kubaki kwenye ndoa (Why I Stayed). Huo ni mfano mmoja, na iko mingi sana.
Ku-cheat is not a crime, ila ni dhambi kwa waumini wa dini. Ndiyo maana nilisema watu wanaona ni kitu cha kawaida tu ni sawa na kudanganya, kutamani, na dhambi nyinginezo ambazo watu wanazifanya kila siku.
Wengi wanao-cheat huwa wanafanya siri, na huwa hawagunduliki kirahisi.
Kama mumeo haja-cheat, shukuru Mungu na endelea kumuomba Mungu ili mumeo aendelee kuwa hivyo. Ila angalia tu siku ukija kugundua unaweza kujimaliza kwa mshituko.