Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Majumba saba

Senior Member
Joined
Feb 1, 2019
Posts
145
Reaction score
610
Mie ni muhitimu wa Degree ya Kwanza ya Banking na Finance mwaka huu wa 2020 na nimepata GPA kubwa. Kinachonishtua ni ofa zinazo patikana ni mishahara kiduchu mno!

Kiukweli, over my dead body, sipo tayari kwa ajira ambayo take home yake ni chini ya milioni moja.

Hope zinapatikana bila shaka.
 
Kuna mtu alikuitia ajira huku??
we subiri baada ya miezi sita utakua ufuta huu Uzi hapa na kuomba hata kazi ya kufagia kwa mama lishe
Hajui ugumu wa mtaani huyu, wahitimu wengi hua na matumaini makubwa sana kuliko uhalisia na ndio maana wanapata msongo wa mawazo,
Kipindi hicho namaliza chuo rafiki yangu mmoja alisema bila 2m take home hafanyi kazi, ajabu zaidi alianza na laki 8 kwa mchina.
 
Kwani sasa hivi unakaa wapi?Kama unakaa nyumbani kwa wazazi au kwa shemeji wakikuchoka utapata tu akili
Ndugu, Bora ningepata hio laki nane, fursa nyingi napata microfinance, na wanataka niwe tayari kuanza na shilingi laki tatu na nusu. Sasa nawaza, maisha ndio yatakuaje? Hio Nile, nipange, niende saloon, nitoe sadaka kha
 
Ndugu, Bora ningepata hio laki nane, fursa nyingi napata microfinance, na wanataka niwe tayari kuanza na shilingi laki tatu na nusu. Sasa nawaza, maisha ndio yatakuaje? Hio Nile, nipange, niende saloon, nitoe sadaka kha
Better take that chance, fanya kwa bidii, onyesha thamani yako na tengeneza umuhimu wako kiasi kwamba siku ukitaka kutoka wanahisi kupoteza human capital ya muhimu. Kuhusu matumizi, jibane, ishi kuendana na kipato..Ni wachache sana wanaobahatika kuanzia unapopataka.

NAFASI UWEZO JINA PESA, hii ni chain muhimu sana ambayo ukiizingatia itakupa zaidi ya hiyo milion moja...Chukua nafasi, Onyesha uwezo, tengeneza jina then ingiza pesa.

Usisahau, your value depreciates with time. Better understand that. Gud luck
 
Over my Dead body Kama huyo wa kwenye Avatar ndio wewe walah hicho kiuno na kalio utapata hata 2M take home, we tembea tembea tu utapata!!!
Mkuu, kumbe na wewe umekagua avatar yake [emoji3][emoji3][emoji3][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Back
Top Bottom