Kulingana na kazi yangu kama mlinzi wa taasisi moja ya serikali sometimes nakuwa dereva, sometimes nakuwa receptionist and so.
Wahitimu wa shahada ya kwanza wanaokuja kuomba kazi ya usafi kazini ni wengi sana. Sasa sijui ni ugumu wa maisha au wanatafuta connection tu!
Sipingani na mawazo yako ila ngoja nikuambie kitu.
Mimi niliwahi kukataa kazi ya police, jeshi na nilikataa kusomea ualimu.
Maisha yalinitandika mpaka nikanyoosha mikono.
Imagine sasa Mimi ni mlinzi , ningekuwa mjeshi sasa tayari ningekuwa na nyota 3.
Huku niliko nalipwa vizuri tu. Nimejenga, nina gari ya kutembelea lakini naichukia title hii ya "Mlinzi". Hata ujasiri wa kutaja kazi yangu mbele za umma sina