Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Ndugu, Bora ningepata hio laki nane, fursa nyingi napata microfinance, na wanataka niwe tayari kuanza na shilingi laki tatu na nusu. Sasa nawaza, maisha ndio yatakuaje? Hio Nile, nipange, niende saloon, nitoe sadaka kha
Kwa hiyo usipofanya kazi hayo mahitaji yako utayatimizaje? au bado upo upo home. Serikalini take home ya 1M si mchezo, yaani wawe wamekata kodi yao sichini ya laki 2.5 (TRA), mifuko ya hifadhi ya jamii (10-15%), bima ya afya (si chini ya 50,000/=), mkopo wa bodi kama ulikopa (15%), vyama vya wafanyakazi nk, nk. Na hata ujuzi huna ndo unaanza kazi!!!. Hata sector za mabenki binafsi kwa wanaoanza kama bank officers, hiyo take home ya 1M ni ngumu sana. Wacha kuishi ulimwengu wa ndoto jishikize ukiwa unagain experience na kupata connections.
 
Wasikutishe mkuu kikubwa itunze thamani yako wasije kukutisha sijuwi mtaani kugumu! Wanasahau nawewe upo mtaani unayaelewa mazingira! humu duniani kila mmoja ana riziki yake na kama ipo, ipo tu
#nyie walimu wa mtaa kaeni kwa kutulia sio watu wote wana dhiki za hizo kazi za mia mbili mia mbili
 
Nakumbuka wakati nipo 4th year Chuo nilienda kwa Uncle wangu mmoja huku ninakunywa chupa kubwa ya maji ya Kilimanjaro. Wakati huo chupa ilikuwa inauzwa nadhani TZS. 900/-. Uncle akanicheeeeck then akasema dogo ‘unatupa’ 900 nzima kununua maji ya kunywa tu wakati huku kitaa tunanunua ndoo nzima ya lts. 20 kwa TZs. 200?? Chunga sana!

Anyway, huyu kijana huenda ana vision kubwa na hataki kuchukua just any salary. Ila sometimes ni bora sana kuchukua kazi ili ukapate experience huku ukilipwa hata hiyo kidogo. Experience itakusogeza huko kwenye salary unayoitaka mbele ya safari. Itafika wakati unaweza kujikuta unaomba hata kujitolea bure kabisa mambo yakishakugomea

All the best!
 
Mie ni muhitimu wa degree ya kwanza ya Banking na Finance mwaka huu wa 2020 na nimepata GPA kubwa. Kinachonishtua ni ofa zinazo patikana ni mishahara kiduchu mno!

Kiukweli, over my dead body, sipo tayari kwa ajira ambayo take home yake ni chini ya milioni moja.

Hope zinapatikana bila shaka.
Majumba saba hujambo? Hiyo avatar ni picha yako halisi? Mimi nipo tayari kukuajiri kwa hicho kiasi unachokitaka, fanya chap kunitafuta.
 
Una matatizo ndugu
Mie ni muhitimu wa degree ya kwanza ya Banking na Finance mwaka huu wa 2020 na nimepata GPA kubwa. Kinachonishtua ni ofa zinazo patikana ni mishahara kiduchu mno!

Kiukweli, over my dead body, sipo tayari kwa ajira ambayo take home yake ni chini ya milioni moja.

Hope zinapatikana bila shaka.
 
Acha porojo
TRA wenyewe kwa weye fresh graduate haupati hiyo 1M
wasikutishe mkuu kikubwa itunze thamani yako wasije kukutisha sijuwi mtaani kugumu! Wanasahau nawewe upo mtaani unayaelewa mazingira! humu duniani kila mmoja ana riziki yake na kama ipo, ipo tu
#nyie walimu wa mtaa kaeni kwa kutulia sio watu wote wana dhiki za hizo kazi za mia mbili mia mbili
 
Mie ni muhitimu wa degree ya kwanza ya Banking na Finance mwaka huu wa 2020 na nimepata GPA kubwa. Kinachonishtua ni ofa zinazo patikana ni mishahara kiduchu mno!

Kiukweli, over my dead body, sipo tayari kwa ajira ambayo take home yake ni chini ya milioni moja.

Hope zinapatikana bila shaka.
Utakua unakaa kwenu au kwa shemeji yako, ukiwa mkubwa ukakaa kwako hiyo hela utaichukua tu,kuna watu wanachukua 300,000 wako hapa unakuja kuwatukana na kuwakejeli?
 
Kulingana na kazi yangu kama mlinzi wa taasisi moja ya serikali sometimes nakuwa dereva, sometimes nakuwa receptionist and so.

Wahitimu wa shahada ya kwanza wanaokuja kuomba kazi ya usafi kazini ni wengi sana. Sasa sijui ni ugumu wa maisha au wanatafuta connection tu!
Sipingani na mawazo yako ila ngoja nikuambie kitu.

Mimi niliwahi kukataa kazi ya police, jeshi na nilikataa kusomea ualimu.
Maisha yalinitandika mpaka nikanyoosha mikono.

Imagine sasa Mimi ni mlinzi , ningekuwa mjeshi sasa tayari ningekuwa na nyota 3.
Huku niliko nalipwa vizuri tu. Nimejenga, nina gari ya kutembelea lakini naichukia title hii ya "Mlinzi". Hata ujasiri wa kutaja kazi yangu mbele za umma sina
 
Back
Top Bottom