Siri gani ambayo huwezi kumwambia mtu yeyote kwenye maisha ya kweli lakini utaisema humu kwa kutumia anonymity? ?

Siri gani ambayo huwezi kumwambia mtu yeyote kwenye maisha ya kweli lakini utaisema humu kwa kutumia anonymity? ?

Asalam ndugu wa jf

Kama kichwa kinavyojieleza hapo

je ni siri gani unayo ambayo huwezi wala hukuwahi kumwambia yeyote in real life

But would on JF using anonimity'''

Siri yangu mimi... sijawahi kuwapenda wenye mtazamo hasi kwangu. Japo nacheka nao
There is no anonymous in JF... There is classified IDs
 
Siri yangu kuanza drs LA kwanza nikajua kusoma sitamsahau mwl wangu hiyo ndio siri yangu
 
Nimesha lala na mwanaume ambaye nampenda ila yeye hakujua kama nampenda na sikuwahi kumwambia yeye wala mwingine yeyote.

Niliiba kalmati ndani ya kabati na San vita kwa baba taibali bila kulipa. Sikuwahi mwambia yeyote.

Najua kuendesha gari manual ila nilipokuwa na baby hajui kuendesha manual nikamwambia sijui hata kuendesha gari na hadi kesho sijawahi mwambia. Kila nikienda mahali tuonane nachukua uber au bajaji. Nikiwa kwenye misele yangu nabadili gear kama Michael Schumacher.

Kasie Matata.
Ha ha ha ha ha ha ha ha
 
Jamaa yangu flani hapa job alinileteaga nuksi/uchuro tena nusra nifukuzwe kazi na hiyo ilikuwa baada ya kusimamshwa kazi mara kadhaa, sio mini tu na wenzangu pia. Yeye alikuwa na ukaribu/undugu na boss wetu.
Nikajisemea wacha ninkabidhi kwa Mungu juu ya dhurumati yake. Leo hii ni miezi mitatu tangu ajali ya pkpk, yupo Bugando hospital kavunjika mguu mara 2 na sehemu ya nyonga, kazini boss kashaanza kumsahau.
 
Back
Top Bottom