Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Mkuu Malyenge,
Hoja kwamba Roho mtakatifu anapatikana vipi si muhimu hapa na kwa wakati huu na vile vile Biblia iko very clear on how to receive the Holy Spirit.
Aidha, makosa yaliyomo kwenye Biblia ni ya kiuandishi au niseme ni ya kibinadamu na wala siyo ya kitheolojia kwamba yanaweza sababisha mkanganyiko wa kiimani!

Hata hivyo, mambo haya uwa proved practically ktk uwanja wa kazi (kanisani) ambapo kwa nguvu ya Neno watu hugeuzwa kutoka maisha ya uovu na kuwa waadilifu kwenye jamii, wengine huponywa magonjwa yao na mambo kama hayo.

All in all is to prove and validate the authenticity of the Bible.

Ahsante.
 
Aisee mkuu nimekuelewa sana umejibu mada kwa busara na kunielewesha vizuri kabisa bila matusi wala kejeli.... sasa wewe ndio great thinker umefanya analysis ya pande zote mbili

Ubarikiwe mkuu
Matusi, kejeli, vijembe kwa mtoa hoja badala ya kuikabili hoja ni alama ya utoto na jeuri tu itokanayo na roho ya kukosa maarifa!
 
Huyo Roho Mtakatifu ni nani? Na wako Roho Mtakatifu Wangapi?
Huwa ananenaje na sisi binadamu?
 
Biblia is the greatest scam ever made!

Na hawa wazee wa kipumbavu wa kiyahudi waliyoitunga ni wakuchoma kabisa!

F.uck jews,f.uck god,f.uck all religions,f.uck everybody...and if you mind,F.UCK YOU TOO!
 
Mkuu Malyenge,

Kwa kuwa tunazungumza kwa muktadha wa Biblia, naomba nikupe nukuu hii kutoka Matendo 10.

Inaelezea vizuri na kujibu vyema swali lako.

9 Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;


10 akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia,


11 akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;


12 ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.


13 Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule.


14 Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.


15 Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.


16 Jambo hili likatendeka mara tatu; kisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni.


17 Hata Petro alipokuwa akiona shaka ndani ya nafsi yake, maana yake ni nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiisha kuiulizia nyumba ya Simoni, wakasimama mbele ya mlango,


18 wakaita; wakauliza kwamba Simoni aitwaye Petro anakaa humo.


19 Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta.


20 Basi ondoka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma.


21 Petro akawashukia wale watu, akanena, Mimi ndiye mnayemtafuta. Mmekuja kwa sababu gani?
 
Hoja?
 
Ikumbukwe ya kwamba,pamoja na ukweli wa MUNGU yupo lakini wakati mzungu na mwarabu wanazitangaza dini ukanda wa Afrika kuna mambo pia waliyaficha ili kulinda makusudi yao.na mahubili mengi yalijaa vitisho ili tusiwasumbue na kuwaondoa kwenye ardhi yetu.swala hapa ni kujua why kitabu fulani na fulani kilichomolewa na kwa manufaa gani wa wakati huo.

kulikua na vitisho vingi na hasa moto wa jehanamu au laana na hukumu,vitu ambavyo mwanadamu yeyote hawezi kuvithibitisha kuwepo au kutokuwepo.
 
Majibu mepesi sana hayo
 
katika zama hizi za imani tumefundishwa mambo mengi ambayo sio uhalisia wake.
imani ya viongozi wa dini ilipelekea kutufundisha hivyo kwa kuamini ndio tutakua na imani kubwa kumbe ni hapana.

walituaminisha kwamba biblia ni maneno ya Mungu wakiwa na maana mwandishi ni Mungu akimwongoza mwanadamu na sisi tukaelewa kwamba binadamu alikua kama mchapa kitabu na mtunzi ni mwingine!!

kwa uelewa wangu ukimwamini Mungu unaanza kuwa mfuasi wake, tokea hapo unaanza kutembea kwa kumwiga yeye. haina maana hatua zako anazcontroo Mungu,hapana ww utaishi kulingana na yale uliyojifunza. hicho ndicho kilichotokea kwa waandishi. hapo ndipo nawasifu na kuiamini biblia. maana waliandika watu tofaut jambo moja kwa mfanano wa karibia 99% inaweza kukosewa kitu kidogo lakin sio maudhui.

roho mtakatifu hakukatazi kutotenda dhambi anakufundisha ubaya wa dhambi. tukisema waandishi waliandika kwa kutumia akili ya Mungu tunamfanya Mungu ni dicteta anaweza kuhodhi akili ya binadamu kwa kipindi fulan. tutofautishe unabii na mafundisho.

nihitimishe kwa kusema biblia ni mafundisho ya pamoja toka kwa watu wa Mungu kiukweli wanashabihiana japo wameishi vipindi tofaut. na wakati mwingine waliandika vitu ambavyo hawajawahi hata kuviona mfano mussa, aliandika mambo ya uumbaji miaka elfu kadhaa
iliyompita.

ni amri kumi tuu ndio Mungu alihusika kwa 100% . hata unabii walifunuliwa baadaye wakaanza kuelezea . kuna wakati waliwahi kusahau ila wakakumbushwa
 
Hakuna jambo zuri kama kujifunza kuhusu mungu na imani kwa ujumula wake.usiwe mfia dini na kukalili tu na usijitie mjuaji tuendelea kujifunza
 
Hao watu waliyopata maarifa ya biblia kupitia Roho mtakatifu mbona hatujawahi kuona kuja kutumegea hayo maarifa?
Wengi hutumia hii kama defence mechanism ila huwa hawamaanishi hasa pale wanapoishiwa hoja ndio maana mijadala mirahisi hawakwambii kamuulize Roho mtakatifu ila mijadala migumu ndio wanajibu hivyo hapo huoni kuna shida??

Kama kweli wangekuwa wanamtumia Roho mtakatifu kusingekuwepo na madhehebu mengi wala version za Biblia nyingi ambazo zimeleta hizi discrepancy bali maaskofu wotte wangejifungia chumba kimoja na kumuuliza Roho mtakatifu dhehebu au Biblia gani ni sahihi basi wangekuwa kitu kimoja ila hawafanyi hivyo lakini walipigwa maswali magumu ndio wanamrushia kete roho mtakatifu??

Huu ndio unafiki mkubwa zaidi
 
Huyo Roho Mtakatifu ni nani? Na wako Roho Mtakatifu Wangapi?
Huwa ananenaje na sisi binadamu?
Roho Mtakatifu ni mmoja aliyeko ndani ya Mungu Baba na Mwana.Ananena kwa kukuongoza binadamu ili usipotoke dhambini,Dhamira inapokusuta kwa tendo ulilofanya hapo ni Roho anafanya kazi.Mimi Si Mchungaji ila kwa uelewa wangu mdogo wa Biblia.
 
Roho Mtakatifu ni mmoja aliyeko ndani ya Mungu Baba na Mwana.Ananena kwa kukuongoza binadamu ili usipotoke dhambini,Dhamira inapokusuta kwa tendo ulilofanya hapo ni Roho anafanya kazi.Mimi Si Mchungaji ila kwa uelewa wangu mdogo wa Biblia.
Uliahawahi kuongea naye? Akinena suti yake inafanana na sauti gani?
 
 
Roho Mtakatifu ni mmoja aliyeko ndani ya Mungu Baba na Mwana.Ananena kwa kukuongoza binadamu ili usipotoke dhambini,Dhamira inapokusuta kwa tendo ulilofanya hapo ni Roho anafanya kazi.Mimi Si Mchungaji ila kwa uelewa wangu mdogo wa Biblia.
Hivi unaelewa maana ya kunena?
Kunena ni kutamka kwa sauti.
Swali:
Je umewahi kuiskia sauti yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…