Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

heri mimi mwenye kumjua Mungu kuliko wewe 'kafiri'.
unazungumza kama mjuaji ila si kueleweshwa nadhani ukitaka nikufafanulie jifunze kuandika kwa uelewa.
 
Dar wewe bana kiboko ya rigwaride ulisomea seminary ya wapi kijana. Umri wako tafadhali?
Wengine ni mapadri,siyo Bure tufungue kanisa tu. la wana jamii forum.napmba mchagiue vyeo.
ila mimi niwe mtunza fedha wa church.
 
Mengi hapo ni maelezo ya Devil worshipers kupitia the knight of Columbus,the skull and Bones ya akina Bush, John Kerry etc
Biblia ni kitabu kitakatifu
 
Mungu wa kwenye biblia anapigana "wrestling" na binaadam, kama hiyo haitoshi, Mungu wa biblia anawashika binaadam mpaka "uvungu wa mapaja"!

Biblia, mwanzo 32:
24 Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako n'nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.
30 Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.
 
Mengi hapo ni maelezo ya Devil worshipers kupitia the knight of Columbus,the skull and Bones ya akina Bush, John Kerry etc
Biblia ni kitabu kitakatifu
Mkuu jikite kwenye hoja nini mtazamo wako kwa NIV kufuta mistari zaidi ya 64,000 iliokuwepo kwenye King james Version (Ambayo Biblia ya kiswahili ilitoholewa humo) na wamedai iliongezwa kimakosa na wahuni...... Je NIV wako sahihi kufuta?? Je kama kweli iliongezwa na wahuni nini hatma ya Biblia kma kitabu kitakatifu??

Pia kama NIV wameifuta kimakosa.... Je nini hatma ya Biblia kama mtu yeyote anaweza punguza/ongeza mistari ya Biblia anavyotaka.... Je hizo version wanazotengeneza zinaifanya bado Biblia kuwa kitabu kitakatifu au wanakuwa wameinajisi??

Pia nini msimamo wako juu ya kitabu cha wimbo ulio bora, Vitabu 4 vya injili na waebrani n.k ambavyo mpaka leo mwandishi wake hafahamiki lakini vimewekwa kwenye Biblia?? Je kwanini vitabu kma Enoch au Gospel of Judas Iskariot vimezuiwa kisa mwandishi hafahamiki vizuri ila hivi vya injili vimechukuliwa ilihali mwandishi mpaka leo hajulikani??? Huoni kuna double standards hapo mkuu??

Karibu
 
Shetani mwenyewe kaja kivingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu jikite kwenye hoja nini mtazamo wako kwa NIV kufuta mistari zaidi ya 64,000 iliokuwepo kwenye King james Version (Ambayo Biblia ya kiswahili ilitoholewa humo) na wamedai iliongezwa kimakosa na wahuni...... Je NIV wako sahihi kufuta?? Je kama kweli iliongezwa na wahuni nini hatma ya Biblia kma kitabu kitakatifu??

Pia kama NIV wameifuta kimakosa.... Je nini hatma ya Biblia kama mtu yeyote anaweza punguza/ongeza mistari ya Biblia anavyotaka.... Je hizo version wanazotengeneza zinaifanya bado Biblia kuwa kitabu kitakatifu au wanakuwa wameinajisi??

Pia nini msimamo wako juu ya kitabu cha wimbo ulio bora, Vitabu 4 vya injili na waebrani n.k ambavyo mpaka leo mwandishi wake hafahamiki lakini vimewekwa kwenye Biblia?? Je kwanini vitabu kma Enoch au Gospel of Judas Iskariot vimezuiwa kisa mwandishi hafahamiki vizuri ila hivi vya injili vimechukuliwa ilihali mwandishi mpaka leo hajulikani??? Huoni kuna double standards hapo mkuu??

Karibu
 
Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mathayo 11:25-28.

Nimeona niambatanishe hoja yangu na hilo hiyo mistari hapo juu. Unaweza kuwa mjuzi sana mwenye elimu kubwa sana au mwanasayansi mkubwa kama Newton au Einstein, lakini ukashindwa kuyaelewa maandiko.Kuna tofauti Kati ya karama na elimu.
Walioandika biblia walijaliwa karama ya unabii ambapo hata sayansi haina majibu ya unabii.
 
Biblia ipi unayoongelea NIV au KJV?
Unaongelea septuagint au masoretic??
Unaposema muandishi wa Biblia mfano kitabu cha Mathayo ulichonukuu mpaka leo hajulikani?? Kama unamfahamu naomba ututajie then ndio tutajua alikua na hizo nguvu unazosema au lah.

Ni hivi mkuu imani ya ukristo ni ya ku reason sio ya kuburuzwa kama punda. Shida inakuja unapohoji unaonekana kama shetani fulani au umepungukiwa hekima ingawa kweli kuna hoja zina mashiko.

Sasa mfano Mtume Yuda kanakili mstari wa Kitabu cha Henoko ambacho Biblia haikitambui na inadai cha kishetani ndio maana kanisa ikakitenga Huoni kuna double standards??

Leo hii muandishi wa Mathayo mpaka Yohana hajulikani (kama unamfahamu tusaidie) lakini kwenye Bible kimeachwa ila vitabu vingine kama Jasher vimefutwa sababu eti muandishi hajulikani?? Je huoni kuna siri inafichwa hapa.

Haya maswali nayohoji yana mashiko ndugu yangu ni vizuri uchukue muda wako utafiti uje na majibu kuliko kuishia kutoa kejeli.

Sasa hapo unasema WALIOANDIKA..... But hapo hapo humjui alieandika kitabu cha Mathayo does it make sense??
 

Hata manabii akina Jeremiah na Isaiah wanatambua hii kitu ya watu kuweka mikono kwenye maandiko:

Mfano nabii Jeremiah kwenye Jeremiah 8:8 anasema:

"'How can you say, "We are wise, for we have the law of the LORD," when actually the lying pen of the scribes has handled it falsely?"(Jeremiah 8:8)
 
Hivi hivyo vitabu vya Josher,Enoch NK havipo kwenye bibilia ya watu weusi(Ethiopian Orthodox Bible)?
 
Hivi hivyo vitabu vya Josher,Enoch NK havipo kwenye bibilia ya watu weusi(Ethiopian Orthodox Bible)?
Exactly lakini inahesabika sio mainstream Christianity yaani viko grouped kma pseudepigrapha yaani maandiko yenye SHAKA na POTOFU.
 
Exactly lakini inahesabika sio mainstream Christianity yaani viko grouped kma pseudepigrapha yaani maandiko yenye SHAKA na POTOFU.
Ni jambo la kutia shaka ikiwa Ethiopia walipata injili kabla ya rumi iweje ,wakoloni waje kutufundisha injili kuna vitu vinavyoonesha uwakala wao kwa shetani walivipunguza
 
Kuna watu wa imani niliwahoji juu ya hili suala, sasa hivi wananiona mimi nimepotoka
 
Ila kama upo Dini nyingine tuachie wenye Dini
kwahiyo mkuu unaamini dini usiyoijua? Yaani unatii tuu bila kuhoji uhalisia wa chochote usichoelewa??
Anyway Kwa maoni yako mkuu Biblia ipi ni halali NIV au KJV??
 
Ukienda library kuna vitabu vingi vya fani mbali mbali. Kuna vitabu vya Sheria, sociology, Psychology, research, education, engineering, mawasiliano, afya na udaktari, philosophy, uongozi, history, lugha, policies nk. Ni vingi na kila somo kuna vitengo vyenye upana wa kujisimamia na vina vitabu vingi na vingi isiyo na kifani.

Kuna maarifa na weledi mkubwa sana kwenye dunia hii. Watu wengi wameandika vitabu vingi na vyenye mashiko ya hali ya juu kulingana na somo linalofundishwa . Dunia imejaa vitabu na maarifa makubwa kuliko tunavyoona au tunavyofikiri.

Kwa aina ya watu wa nchi za magharibi na utamaduni wao wa kujibidisha kuandika, hawawezi kushindwa kuandika Bible. Maarifa ya biblia ni ya kawaida sana kwa sababu yamejaa history za jamii za watu ambazo ni rahisi kwa mtu mwenye kichwa cha akili. KINACHOTOFAUTISHA BIBLE NA VITABU VINGINE NI KULE KUPEWA HADHI YA UMUNGU. Hali hiyo kimekifanya kitabu hicho kionekane tofauti lakini si kweli kwa sababu hakuna panapojidhihirisha kuwa ni cha Mungu.
 
Kitendo cha Bible kuitwa kitabu kitakatifu cha Mungu au kitabu chochote haimaanishi ni cha Mungu. Kuingiza neno "Mungu" au "Yesu" au "Roho mtakatifu" haimaanishi kinakuwa cha Mungu. Kitabu chochote kinaweza kubandikwa kitabu cha Mungu, mtu yeyote anaweza kukiita kitu chochote kuwa ni cha Mungu.

Udhaifu wa binadamu katika kuumbwa kwake ni kuwa maarifa ya binadamu hutokana na kujifunza katika mazingira yake. Mtu mmoja au kundi la watu laweza kufundisha watu wengine mfumo fulani wa maisha na ikafanya kuwa ndio mfumo sahihi.

Hoja hiyo huwa inawahiwa na wafia imani au watumwa wa dini kuwa ni Mungu anayefanya hivo au yeye ndo amesema au yeye ndo kasimamia uandishi. Kwa vile binadamu hujifunza kwa milango yake mitano ya fahamu, akisikia au kuona/kusoma au kuhisi maumivu au furaha na kuyaita ni ya kimungu ataelewa hivo.

Kwa mantiki hiyo, kinachojadiliwa kuhusu vitabu vya biblia, tunajadili mafundisho au taarifa tulizopewa au kufundishwa kwa kusoma au kusikiliza. Biblia ipo na kuna tofauti za biblia lakini inawezekana hakuna hata kimoja kilichowahi kuwepo na maisha yakaendelea .

Ebu chunguza hili jambo dogo la mfano, harafu jiulize. Tumefundishwa symbol au alama "a", fanya kuisoma/kuitamka. Ebu fikiria, hivi kuna uhusiano wowote kati ya hiyo alama "a" na sauti uliyoitoa wakati unasoma?
Je, mtu ambaye hakukulia au kufundishwa hizi Roman alphabets hatamki huyo herufi ? Fikiria tu. Je unadhani watu wa jamii ya China, uarabuni na Korea kwa mfano ambao hawakutawaliwa, kuathiriwa au kufundishwa hizi Roman alphabets, kwa mfano wetu "a" hawaitamki? Yaani hakuna sauti "a" kwenye lugha zao? Jibu ni kuwa sauti hiyo ipo, ila haiandikwi hivo. Kwa hiyo ni mafundisho, ni mapokeo ya jamii ndiyo humtrngeneza binadamu alivyo.

Kwa maana hiyo, kama sauti tu ya herufi fulani kama "a" tunaamini baada ya kufundishwa kuwa inatamkika hivyo, ni rahisi kutuaminisha baada ya kutufundisha kuwa kitabu fulani na mistari yake ni vitakatifu au vya ki-Mungu labda na vingine si vya ki-Mungu. Na tukapata shida sana na kuona kuna agenda iliyopo. Hii ni kwa sababu ya yale madhaifu ya binadamu katika kutengeneza.

Na kibaya zaidi, maarifa ya awali huonekana kweli kuliko yanayofuata, ndo maana watu wanahamaki watu wakisema kuna shida au uongo au changamoto kwenye vitabu vilivyoitwa vya ki-Mungu.

Kunaweza kukawa na uongo mkubwa kwenye vitabu hivi viwili vya imani kuliko uongo mwingine kiimani duniani. Mfano, siku za hivi karibuni kuna kiongozi mkubwa wa kiimani duniani alisikika akisema kuwa hadithi ya Eden juu ya Adam and Eve ni story ya kutungwa na haina ukweli. Sasa jiulize, yule kiongozi ndo wenye hii Bible na ndo wenye ukristo na wanajua ndani nje ya hii imani, sasa kama Adam and Eve ni fake story unadhani kuna maandishi yoyote kwenye Bible yatakayofuata yakiwa na ukweli? Utatoka wapi wakati kizazi cha Adam and Eve hakina ukweli wowote!? Na ndo maana kiongozi huyo huyo akaja na hoja pia kuwa hata moto wa milele wa jehanamu haupo.

Kwa kumrejelea huyo kiongozi na ambaye ni mweledi mkubwa wa biblia na mambo ya imani, maana yake biblia ina uongo mwingi. Wanafahamu uongo uliomo kwa wao walishiriki kujumuisha biblia. Wanafahamu malengo ya kufanya hivo, wameshafanikiwa lkn wanaona binadamu bado ametopea kwenye uongo na ujinga waliotengeneza. Sasa wanakuja hadharani kutaka kumuondoa kwenye dimbwi la uongo??

Jiulize, kama imani, dini na vitabu vyake vina uwezo na nguvu zilizotamalaki, kwa nini hawawekezi kwenye vitabu hivyo? Wako busy na elimu, wako busy na nguvu za kijeshi, wako busy na science and technology, wako busy na kwenda kwenye sayari nyingine, wako busy kutafuta utajiri na Mali kwa ajili ya vizazi vyao, wako busy kuhakikisha wanatawala dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…