Siri imefichuka: Mishahara ya Wabunge wa Tanzania ni kuanzia milioni 11 kwa mwezi

Siri imefichuka: Mishahara ya Wabunge wa Tanzania ni kuanzia milioni 11 kwa mwezi

XI JIN PING II

Senior Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
125
Reaction score
110
Habari wana JF,

Siku zote nimekuwa nikijiuliza jambo moja hapa Tz kwanini Ma Profesa, Wahandisi na wataalamu wabobezi kwenye fani mbalimbali wanaamua kuzipa kisogo fani zao na kukimbilia kwenye siasa hasa ubunge?

Sasa leo Kisalala mbunge wa jimbo la Sumve amenipatia jibu. Wanafuata maslahi manono sana, kama kwa mwezi mbunge anapokea mshahara milioni 11 yaani huu ni nje ya posho zake unafikiri nani hatamani kupata fedha zote hizi?

Profesa wa chuo kikuu hapa bongo hata 7m hafikishi kwa mwezi sasa kwanini asiache kufundisha akakimbilia siasa?

Hayaaa bhana kuleni tu hizo milioni 11 za kila mwezi sisi wananchi tunaendelea kula msoto.

Wasalaam Xi JinPing
 

Attachments

  • IMG_5394.MP4
    10.9 MB
Hiyo hela ni ndogo. Miaka yake miwili ya kwanza anafidia madeni ya uchaguzi. Hiyo mitatu inayobaki hafikishi 1bn. Kama anarudi tena utakuta hajapiga hatua unless kuna biashara ya maana au uwekezaji mkubwa kafanya. Au katumia goodwill kama mbunge akapata gedha sehemu nyingine
 
Wacha niendelee kufuatilia mkuu kwasababu wanalipwa kutokana na kodi ninayo lipa.
Una cha kufanya baada ya kujua? Kama huna, acha tu, utaishia kuumia na tulaki kadhaa twetu hutu! ila kama una cha kufanya, endelea ILA KUMBUKA HUWEZI KUMSAIDIA MASIKINI KWA KUMSHUSHA TAJIRI, BALI KWA KUMPANDISHA MASIKINI AMFIKIE TAJIRI.
 
Una cha kufanya baada ya kujua..?? Kama huna, acha tu, utaishia kuumia na tulaki kadhaa twetu hutu..!! ila kama una cha kufanya, endelea... ILA KUMBUKA HUWEZI KUMSAIDIA MASIKINI KWA KUMSHUSHA TAJIRI, BALI KWA KUMPANDISHA MASIKINI AMFIKIE TAJIRI...
Cha kufanya naandaa mkakati wa kugombea Udiwani 2025 then ubunge 2030 ili nami niwe mnufaika wa keki ya Taifa.
 
Hapa mkuu umechambua vizuri sana.

Mwisho wa siku anayefanikiwa atakuwa ni yule anayechekecha vizuri kichwa chake pamoja na kutengeneza connections mbalimbali za kibiashara.
Hiyo hela ni ndogo. Miaka yake miwili ya kwanza anafidia madeni ya uchaguzi. Hiyo mitatu inayobaki hafikishi 1bn. Kama anarudi tena utakuta hajapiga hatua unless kuna biashara ya maana au uwekezaji mkubwa kafanya. Au katumia goodwill kama mbunge akapata gedha sehemu nyingine
 
Back
Top Bottom