Siri imefichuka: Mishahara ya Wabunge wa Tanzania ni kuanzia milioni 11 kwa mwezi

Siri imefichuka: Mishahara ya Wabunge wa Tanzania ni kuanzia milioni 11 kwa mwezi

Raha ni pale million 11 inalingana na kazi wanazofanya. Na Siku hizi Rais anapopita majimboni wananchi ndio huwa wanafanya tathmini

Maendeleo hayana vyama
 
Mfanyabiashara wa uchumi wa kati anaingiza zaidi ya iyo pesa[emoji5]
Mm nazungumzia mfanyakazi wa kawaida,,

Kupewa pesa hizo ni nyingi sana.

Ukileta mambo ya wafanyabiashara basi hata 100 milioni ni ndogo sana pia.
 
Kama USD4800.00
Pesa ya kawaida sanaa
Ni ya kawaida sana ukiwa tuseme nchi kama Marekani, maana purchasing power ya dollar 4800 ukiwa Marekani ni sawa na purchahsing power ya kama shilling million 4 za mtu aliye Tanzania. Dollar 4800 kwa mtu aliye Tanzania zina purcahing power inayoweza kulingana na dola elfu 12 za mtu aliye Marekani. Naomba usisahau hilo tafadhali!
 
Ndo unajua leo mkuu??

Mbunge kwa mwezi anavuta m12 pamoja na posho 360k per kikao

Waziri anavuta m8,so msela akiwa mbunge halafu no waziri anavuta 20m +posho ya ubunge +posho ya uwaziri😛😛
Yani neema tupu!!
Af mnamcheka mzee wa nje ya Box dah! 😂😂😂
Jamaa kapunguziwa share tu ila still anaendelea kumenya kuliko Graduate mwenye stress za HESLB 😂😂😂😂😂 na huna mchongo town
 
Mfanyabiashara wa uchumi wa kati anaingiza zaidi ya iyo pesa☺
Huyo mfanyabiashara awe na capital sio chini ya 500M ndio atakuwa anakula hizo share kwa mwezi.
Msichukulie kitoto, mshahara wa 20M kwa waziri ambaye ni mbunge pia sio kifala ndio maana Kigwangwise alikuwa anashinda twitter tu 😂😂😂
 
Habari wana JF

Siku zote nimekuwa nikijiuliza jambo moja hapa Tz kwanini Ma Profesa, Wahandisi na wataalamu wabobezi kwenye fani mbalimbali wanaamua kuzipa kisogo fani zao na kukimbilia kwenye siasa hasa ubunge?!

Sasa leo Kisalala mbunge wa jimbo la Sumve amenipatia jibu. Wanafuata maslahi manono sana, kama kwa mwezi mbunge anapokea mshahara milioni 11 yaani huu ni nje ya posho zake unafikiri nani hatamani kupata fedha zote hizi?

Profesa wa chuo kikuu hapa bongo hata 7m hafikishi kwa mwezi sasa kwanini asiache kufundisha akakimbilia siasa?

Hayaaa bhana kuleni tu hizo milioni 11 za kila mwezi sisi wananchi tunaendelea kula msoto.

Wasalaam Xi JinPing
Mkuu sio 11 m tu jumlisha marupurupu ya kila kikao laki tatu pamoja mafuta ya Gari Lita 2000 kwa mwezi,na Ela za Jimbo.
 
Hiyo pesa kwa wenye pesa sio pesa kabisa.Utakuta watu kama kina Kigwangala wanafikia hatua ya kuwatoa watoto wao kafara ili wabaki na ubunge


Pesa hizi bwana
 
Ulisha ambiwa miaka 5 ya ubunge unakuwa umepata pesa dhamani ya 1+ Billion, hapo ni juhudi zako utaokoa sh ngapi kwenye kula bata.
 
Jamaa ana hoja hasa ukilinganisha na mishahara wanayolipwa watumishi wa nchi hii hii. Hapo ndo utaona umuhimu wa kuboresha mishahara kwa watumishi angalau ifanane na ile ya wabunge kwani nao wana changamoto zilezile kama walizo nazo wabunge.
 
nchi ambayo watu wake wengi masikini, changamoto lukuki inawezaje kuwalipa wabunge ambao ni watumishi wa wananchi mshahara mkubwa kiasi hicho?!! haiwezekani, si kweli.....maaana tungeamua kukata mshahara hiyo na wakalipwa japo nusu yake naaamini fedha nyingi ingepatikana kutatua vhangamoto zingine zinazo wakabili wananchi.
 
Yaani mbunge ale 11m kwa mwezi halafu raia namba moja ale 9m kwa mwezi? Mbona hii hesabu haikai?! Kuna kitu hakipo sawa hapa.
 
Back
Top Bottom