Siri imefichuka! Yajue Magonjwa Yanayosababishwa na Kutenda Dhambi

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Nyakati hizi, kuna watu wengi wanaobubujikwa na machozi ya huzuni kwa sababu ya magonjwa yanayowasumbua. Katika kutafuta chanzo cha magonjwa, watu wengi huelekeza macho yao kwenye vyanzo kama vile bakteria, virusi, mazingira machafu, lishe duni, magonjwa ya kurithi, msongo wa mawazo nk. Sawa, hivyo ni vyanzo vinavyokubalika kisayansi. Hata hivyo Biblia inatufundisha kwamba kuna chanzo kingine cha magonjwa kisichoonekana kwa macho ya kawaida. Chanzo hiki ni dhambi.

Ukweli ni kwamba unaweza kujitahidi kuishi kwa kuzingatia kanuni zote za kiafya lakini bado ukaugua kwa sababu ya chanzo hicho: dhambi.

Je ni kweli dhambi inaweza kusababisha mtu augue? Jibu ni ndiyo. Biblia inaonyesha wazi kuwa dhambi inaweza kuleta magonjwa ya mwili. Angalia mifano hii ya kibiblia. Katika kitabu cha Kutoka 15:26, Mungu anasema:
"...utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri...”

Hii ina maana tukienda kinyume na agizo hilo tunaweza kupatwa na magonjwa.

Yohana 5:14 inaeleza kwamba Yesu alipomponya yule mtu aliyekuwa mlemavu kwa miaka 38 alimwambia: “Usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.”

Katika 1 Wakorintho 11:29-30, Paulo anasema kuna watu waliopatwa na magonjwa na hata kifo kwa sababu walikula Chakula cha Bwana isivyostahili.

Ukisoma Hesabu 12:1-10 utaona kuwa Miriamu alimsema vibaya Musa. Mungu alikasirika akamwadhibu Miriamu kwa kuachilia ugonjwa wa ukoma juu yake.

Kumbuka pia majipu waliyopata Wamisri(Kutoka 9:8-12). Hilo lilikuwa pigo la Mungu juu ya Wamisri waliokataa kutii sauti yake.

Utajuaje sasa kama ugonjwa fulani umesababishwa na dhambi na sio vyanzo vya kawaida vya magonjwa? Endelea kusoma...
 
Njia zifuatazo zinaweza kukusaidia kutambua iwapo ugonjwa ulio nao umetokana na dhambi:

1. Roho Mtakatifu anaweza kuongea na wewe. Mtu anayemwamini Kristo ana Roho Mtakatifu ambaye huonyesha kosa na kuleta msukumo wa kutubu. Kwahiyo ukijisikia unaumwa na dhamiri yako inakukumbusha dhambi fulani, usipuuze, inawezekana ni Roho wa Mungu anakuonya utubu.

2. Ugonjwa kama haueleweki kitaalamu au usiopona kwa njia za kawaida licha ya matibabu sahihi, inawezekana chanzo chake ni dhambi. Kwa mfano: mtu anaumwa moyo au tumbo, lakini vipimo vyote vya kisasa vinaonyesha yuko sawa.

Kuna watu wamewahi kushuhudia kuwa waliugua magonjwa mabaya, wakazunguka hospitali zote kubwa kubwa India na Ulaya lakini hawakuona tatizo, lakini walipotubu na kuombewa kwa Jina la Yesu walipona. Magonjwa ya aina hii chanzo chake kinaweza kuwa dhambi au kuonewa na Ibilisi.

3. Maisha ya dhambi ya wazi au ya siri ni njia nyingine ya kutambua kuwa ugonjwa umetokana na dhambi. Kama mtu amefanya dhambi ya uasherati au uzinzi, au wizi, kisha ghafla akaanza kuumwa, inawezekana kabisa dhambi hizo zikawa ndiyo chanzo cha kuugua kwake.

4. Mungu anaweza kukuonya katika ndoto au kupitia watumishi wa Mungu kuwa ugonjwa wako umetokana na dhambi fulani. Kuna shuhuda za watu waliokuwa wagonjwa, wakatubu baada ya kuota ndoto ya onyo, au kusikia sauti ikiwahimiza kutubu. Baada tu ya kutubu na kuomba rehema, walipona. Soma ushuhuda huu wa juzijuzi:

Usinielewe vibaya. Sijasema kila anayeumwa ugonjwa fulani amefanya dhambi. La hasha. Ila ni muhimu tukubali kwamba maisha ya uasi dhidi ya Mungu yanaweza kutusababishia magonjwa. Hivyo tutubu na kujiepusha na dhambi.
 
Kama unaumwa, na umeenda hospitali nyingi na kutibiwa sana lakini hujapona, jihoji sasa: Je, kuna dhambi ambayo hujatubu? Kama hukumbuki, omba kwa unyenyekevu, mwambie Mungu akuonyeshe chanzo cha ugonjwa wako.

Ukitambua kuna dhambi umefanya, tubu dhambi hiyo na usirudie tena kuitenda, kisha muombe Mungu akuponye. Unaweza kuomba sala hii ya toba na maombi ya uponyaji:

"Ee Baba wa rehema, Mungu uliye mtakatifu na mwenye huruma. Ninakuja mbele zako kwa unyenyekevu na toba ya moyo wangu wote. Nakiri kwamba nimetenda dhambi mbele zako, kwa mawazo, kwa matendo, na kwa maneno. Nimeacha kutii Neno lako na kufanya yasiyokupendeza.

Bwana, naomba unisamehe dhambi zote na unitakase kwa damu ya Yesu Kristo. Unioshe kabisa uovu wangu wote. Kama kuna dhambi yoyote iliyoleta hali hii ya mateso au ugonjwa, nakusihi uifunue na uniwezeshe kuitubu kwa moyo wa dhati.

Ninakukiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Naomba uingie moyoni mwangu, utawale maisha yangu.

Ee Mungu rejesha afya yangu na furaha yangu. Naamini ni mapenzi yako niwe na afya njema. Kwa sababu hiyo napokea uponyaji wangu kwa imani. Naahidi kuishi maisha ya utakatifu na utii kwako, siku zote za maisha yangu.

Asante kwa kusikia maombi yangu. Asante kwa msamaha na kwa uponyaji. Kwa jina la Yesu Kristo, Amina.
 
Kuna wengine wanapatwa na magonjwa sio kwa sababu wamefanya dhambi. Mfano mzuri ni Ayubu. Ayubu alikuwa mcha Mungu sana lakini Mungu alimruhusu shetani amjaribu Ayubu. Shetani akamletea Ayubu majipu na vidonda vibaya.

Katika Yohana 9:1-3 kuna habari ya mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Watu wakamuuliza Yesu chanzo cha upofu wa mtu huyo ni nini. Ni dhambi yake au ya wazazi wake? Yesu aliwajibu hivi:
"... wala hakutenda dhambi huyu, wala wazazi wake; bali ni ili kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.” (Yohana 9:1–3)
 
Je, dhambi ya uasherati, uzinzi na ushoga ni chanzo cha magonjwa ya zinaa (Sexually Transmitted Infections – STIs)
Mfano: UKIMWI (HIV), Kaswende (Syphilis), Kisonono (Gonorrhea), Herpes na HPV?? Wewe unaonaje?
 
Nyakati hizi, kuna watu wengi wanaobubujikwa na machozi ya huzuni kwa sababu ya magonjwa yanayowasumbua. Katika kutafuta chanzo cha magonjwa, watu wengi huelekeza macho yao kwenye vyanzo kama vile bakteria, virusi, mazingira machafu, lishe duni, magonjwa ya kurithi, msongo wa mawazo nk. Sawa, hivyo ni vyanzo vinavyokubalika kisayansi. Hata hivyo Biblia inatufundisha kwamba kuna chanzo kingine cha magonjwa kisichoonekana kwa macho ya kawaida. Chanzo hiki ni dhambi.

Ukweli ni kwamba unaweza kujitahidi kuishi kwa kuzingatia kanuni zote za kiafya lakini bado ukaugua kwa sababu ya chanzo hicho: dhambi.

Je ni kweli dhambi inaweza kusababisha mtu augue? Jibu ni ndiyo. Biblia inaonyesha wazi kuwa dhambi inaweza kuleta magonjwa ya mwili. Angalia mifano hii ya kibiblia. Katika kitabu cha Kutoka 15:26, Mungu anasema:
"...utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri...”

Hii ina maana tukienda kinyume na agizo hilo tunaweza kupatwa na magonjwa.

Yohana 5:14 inaeleza kwamba Yesu alipomponya yule mtu aliyekuwa mlemavu kwa miaka 38 alimwambia: “Usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.”

Katika 1 Wakorintho 11:29-30, Paulo anasema kuna watu waliopatwa na magonjwa na hata kifo kwa sababu walikula Chakula cha Bwana isivyostahili.

Ukisoma Hesabu 12:1-10 utaona kuwa Miriamu alimsema vibaya Musa. Mungu alikasirika akamwadhibu Miriamu kwa kuachilia ugonjwa wa ukoma juu yake.

Kumbuka pia majipu waliyopata Wamisri(Kutoka 9:8-12). Hilo lilikuwa pigo la Mungu juu ya Wamisri waliokataa kutii sauti yake.

Utajuaje sasa kama ugonjwa fulani umesababishwa na dhambi na sio vyanzo vya kawaida vya magonjwa? Endelea kusoma...
Mkuu.....Ukoma haupo, Majipu hayapo tena ndio kusema Dhambi hakuna?
 
Je, dhambi ya uasherati, uzinzi na ushoga ni chanzo cha magonjwa ya zinaa (Sexually Transmitted Infections – STIs)
Mfano: UKIMWI (HIV), Kaswende (Syphilis), Kisonono (Gonorrhea), Herpes na HPV?? Wewe unaonaje?
Mbona wanapona bila kuombewa na bila kutubu dhambi?
 
Mkuu.....Ukoma haupo, Majipu hayapo tena ndio kusema Dhambi hakuna?
Mkuu, wewe umeambiwa na nani ukoma haupo duniani? Ukoma umepungua tu kwa sababu kuna tiba yenye nguvu (Multi-Drug Therapy - MDT) inayotolewa bure duniani kote kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO).
Ugonjwa huu unagundulika mapema na kutibiwa kabla ya kuenea.
Lakini wagonjwa wa ukoma bado wapo, my friend, Bush Dokta. Kulingana na takwimu za WHO zaidi ya watu 100,000 hupata ukoma kila mwaka, hasa katika nchi za India, Brazil, Indonesia...
 
Mboma hapa Tanzania haupo dhambi imeisha?
 
Mbona wanapona bila kuombewa na bila kutubu dhambi?
Fikiri tena nje ya box, mkuu. Na adhabu ya moto wa milele watapona bila kutubu?
Ni sawa, wanaweza kupona kwa rehema tu ya Mungu kama njia ya kuwavuta wapate kutubu. Mungu ni mvumilivu.
Warumi 2:4
Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
 
Wanapona kwa rehema ya Mungu? Wakati wanalazimika kumeza madawa? Waache kumeza uone kama wanapona.
 
Mboma hapa Tanzania haupo dhambi imeisha?
Unaota ndoto, mkuu? Kamuulize Mkurugenzi mpya wa WHO kanda ya Africa - Professor Janabi, atakupa data za TZ.
Shirika la Afya Duniani liliripoti kwamba Afrika (Tanzania included) ilishuhudia visa vipya zaidi ya 21,000 vya wagonjwa wa ukoma mwaka 2023!!!
 
Thank you
 
Wanapona kwa rehema ya Mungu? Wakati wanalazimika kumeza madawa? Waache kumeza uone kama wanapona.
Kwani Mungu hahusiki na hizo dawa? Mungu ndiye aliyeumba kila kitu. Hivyo ukimeza dawa ukapona, bado ni rehema tu za Mungu. Na Mungu akiamua kuzuia hizo dawa zisiponye anaweza. Angalia jinsi Mungu alivyosema katika Yeremia 46:11
Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.
 
Back
Top Bottom