Siri kubwa 2 zilizojificha nyuma ya maumivu ya mapenzi unayokutana nayo

Siri kubwa 2 zilizojificha nyuma ya maumivu ya mapenzi unayokutana nayo

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Watu wengi hukutana na maumivu ya mapenzi. Kila mmoja anakutana nayo kwa namna tofauti.

Wapo ambao wanapenda wasipopendwa. Wengine husalitiwa wakiwa ndani ya uhusiano. Wengine huachwa baada ya kuwa pamoja kwa muda mrefu.

Kuna watu ambao hawajawahi kabisa kuyafurahia mahusiano. Kila wanapoweka moyo wao, huishia kuumizwa na kujeruhika.

Lakini kuna siri 2 kubwa zilizojificha nyuma ya maumivu hayo.

1. Ishara kwamba si mtu sahihi

Kuna msemo unasema, “When somebody is not right for you, God will continuously use him or her to hurt you until when you are strong enough to leave.”

Unapokuwa katika uhusiano na mtu asiye sahihi, Mungu ataendelea kumtumia mtu huyo kukuumiza mpaka utakapochukua hatua ya kuachana naye.

Kiashiria kimojawapo kitakachokusaidia kujua kwamba upo katika mahusiano na mtu asiye sahihi kwako ni maumivu na mateso unayoyapata kwa kuwa katika mahusiano na mtu huyo.

Kuna maumivu yamekuja kukupa taarifa kwamba, “We ndugu, huyu si sahihi kwako, ondoka.”

Ni maumivu yanayokutaka uchukue hatua.

Na usipofanya hivyo, utaendelea kuumizwa na kuteswa hadi utakapokubali kumuacha aende.

2. Malipo ya uliowaumiza

Kama unapitia maumivu, ni muhimu sana kujua kwamba yawezekana kuna maumivu ya mapenzi ambayo unakutana nayo leo kwa sababu ya mtu uliyewahi kumuuma.

Kuna mtu amewahi kukupenda, akajitoa kwa ajili yako na kuwekeza hisia, muda na fedha zake, lakini uliishia kumjeruhi.

Na kwa sababu ulimjeruhi na kumuuma kwa makusudi, likawa kama deni ambalo ndiyo leo unalilipa kwa maumivu unayopata kwa unayempenda.

Hata maandiko yanasema, “Maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.”

Hii humaanisha kwamba maumivu unayopitia leo yanaweza kuwa matokeo ya maumivu uliyowahi kumsababishia mwingine.

Nashauri, kama unaweza, mtafute au watafute na uombe msamaha.

Ikiwa kuwapata ni ngumu, nenda mbele za Mungu, kafanye toba ili wakuachilie katika mioyo yao.

Wakati mwingine maumivu tunayopitia yanaweza kuwa somo la kutufanya tujifunze kuthamini watu wanaotupenda kabla hatujawapoteza.

broken.png
 
Back
Top Bottom