Mfano wa Jua kuzunguka Dunia unaupata hata katika saa ya Mshale, na Ujue tuu wazee wa zamani kutumia Jua kujua masaa ndio kulileta idea yakutengeneza saa ya mshale kwa kufuata hesabu za mzunguko wa Jua linapoizunguka dunia Masaa 24.
Na katika hili nikugusie kidogo sababu ya wewe Kudanganya mengi, Nikuulize hivi kati ya Jua na Saa kipi kinatoa Muda wa Ukweli, ikiwa wazee waliamini kwa mfano kivuli cha mti kikiwa pale ni saa flan, lakini wewe ni mara ngapi unaamka jua linaonesha ni saa mbili ila saa inaonesha ni saa 12 au kinyume chake..
Nijibu ukiweza... Hivi ni kwanini Kama Jua linazunguka masaa 24 net, lakini masaa ya kuchomoza na kuzama kwake hubadilika? je kwa kutumia jua kuna mabadiliko ambayo yangekua yanatokea kama hayo? mfano mkisema muwe mnaenda shambani jua linapoanza kutoka na mwingine aseme linaanzaga kutoka saa 12, nani atakua kupuyanga?
Sasa chukulia duara la saa ya Mshale ni kubwa kama lile la katikati ya Dimba la mpira, then Chini ya point ya mshalewa saa tuweke taa inayomulika namba. Je huo mwanga utalimulika Duara zima? kama sivyo basi patakapokua na mwanga ndio panaitwa mchana na patakapoukosa mwanga pataitwa usiku.
Si hivyo tuu kama wewe ni Muumini wa imani ya Dini, katika uumbaji Mungu aliumba Jua, Mwezi na Nyota ili tuweze kujua Saa na Majira.