Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Si unaona ulivyo mbumbumbu wewe na flat earthers wengine
Hapana sijaikwepa,....ishu ni kwamba sioni logic ya maswali husika....Kwa mfano anauliza kwanini position ya Jua kuzama na kuchomoza inabadilika......hapa alitakiwa atuambie position inabadilika vipi na amethibitisha vipi kama inabadilika
 
Hiki ndicho ulichobakiza,

Ajabu umepewa majibu mengi sana humu, Ungekua mtu ambae ni mwepesi wa kupambanua mambo nadhani mpaka sasa ungekua umeshafahamu Dunia ni Tufe.
Bado hujathibitisha chochote.......👇🏼

Unachotakiwa ni kuthibitisha:-
1. Dunia ni Tufe 👉🏼 🌍
2. Dunia inazunguka.
 
Kwa ndege yenye ukubwa wa kutosha, inapokuwa imeshapaa na kutulia hewani, pasipotokea misuko suko unaweza kuweka kikombe cha cha chai na kisitikike wala kupata vibration. Kwanini na ndege ipo kwenye movement?
 
Kwa ndege yenye ukubwa wa kutosha, inapokuwa imeshapaa na kutulia hewani, pasipotokea misuko suko unaweza kuweka kikombe cha cha chai na kisitikike wala kupata vibration. Kwanini na ndege ipo kwenye movement?
In the first place umejuaje kama Ndege ipo kwenye movement?

Hilo swali kuhusu kikombe cha chai linapaswa kuja baada ya kujua whether Ndege ipo kwenye mwendo/not.

Yaani ishu ni kwamba umejuaje kama Dunia ipo kwenye movement?? Hilo ndiyo swali la msingi
 
Usiwe na haraka, huko kwenye dunia tutafika, tubaki kwanza kwenye ndege.

Ulipanda, ulijua itamove, ikamove, na ulithibitisha hilo sababu ulitua sehemu tofauti na ulipopandia, sasa swali ni sababu za kikombe cha chai kutokuwa na vibration ilihali ndege ilikuwa kwenye mwendo. Sababu ni ipi?
 
Mfano wako haupo relevant,... Kwasababu kiwango cha liquid kilichopo kwenye kikombe cha chai ni kidogo sana,.. compared na ukubwa wa Ndege......

Ili mfano uwe relevant,...let's assume Ndege iwe filled na liquid Kwa zaidi ya 75%.....nini kitatokea Kwa liquid husika ikiwa Ndege ina move?
 
kinachosababisha vibration ikosekane ni nini hilo ndo swali, lijibu hata ukiweka assumption ya 75%. Usikimbie kimbie, jibu swali sio unakuja na assumptions kuwa swali si relevant wakati si wewe umeuliza, jibu swali kwanza ili muendelezo wa hoja uendelee.
 
Nikimbie kitu gani sasa,...Sipo hapa kujibu maswali yako Tu bali nipo hapa kutoa elimu na kufundisha watu namna ya kufikiri Kwa kutumia akili zao ili waweze Ku question yale waliyoaminishwa.,

Nikirudi kwenye swali lako vibration haikosekani completely kwenye Ndege bali inakua minimal kulinganisha na other modes of transport kama usafiri wa nchi kavu na majini.....na kinachosababisha usihisi vibration mojawapo ni kuwa Ndege inasafiri kwenye hewa so haikutani na speed bumps, potholes na vitu kama hivyo,...
Sababu nyingine ni balanced operations za Engine za Ndege, altitude na kadhalika.
 
Dunia ingekua Tufe....basi mambo yangekua hivi.......👇🏼
 
Nikimbie kitu gani sasa,...Sipo hapa kujibu maswali yako Tu bali nipo hapa kutoa elimu na kufundisha watu namna ya kufikiri Kwa kutumia akili zao ili waweze Ku question yale waliyoaminishwa.,
Hiyo elimu inatolewa bila kuulizwa maswali au kuna waliolipa ada ndo wana haki ya kukuuliza maswali?
speed bumps, potholes na vitu kama hivyo,...
Sababu nyingine ni balanced operations za Engine za Ndege, altitude na kadhalika.
Vibration inakosekana pale kunapokuwa na constant speed, bila kupungua au kuongezeka ghafla inayoweza kusababishwa na hayo uliyoyataja, Ila kwa sababu huna muda wa kuulizwa maswali ngoja tuishie hapa uendelee na wanafunzi wako boss.
 
Kuuliza maswali sio tatizo kabisa ni sehemu ya kujifunza,.....ili sidhani kama ni sahihi kupinga pindi swali lako linapowekwa sawa ili kulifanya liwe na mantiki & relevant to mada husika.🤝🏼
 
Why chini na sio pembeni au juu mkuu
Kwanza unakubaliana na hiyo image hapo., Kwamba ikiwa Dunia ni Tufe basi maji ambayo yapo attached na Dunia hayatostick kwenye Tufe yatamwagika Kwa kuwa yapo kwenye liquid form?... unakubali?


Maana nikijibu swali lako itakua tumeruka stage ya msingi sana..
 
Kaka bado upo vilevile tu? Basi ngoja nikuongeze swali la mwisho hilo tufe halidondoki? Kwanini utake yadondoke maji tu?
 
Kaka bado upo vilevile tu? Basi ngoja nikuongeze swali la mwisho hilo tufe halidondoki? Kwanini utake yadondoke maji tu?
Mimi nataka maji yadondoke? Hapana

Mimi sikubaliani na nadharia ya Dunia Tufe,..so Tufe kutodondoka sio ishu...

Ishu ni mechanism gani inafanya Maji yastick kwenye tufe(linalozunguka)?

NB:- Ukileta hiyo mechanism usisahau kuambatanisha na uthibitisho.
 
Reactions: Lax
Mkuu nahisi hujaelewa swali, ukiachia kitu hewani kinashuka chini,
Katika picha yako ya maji ya mwagika kuiacha dunia, kwa nini na dunia isianguke kuyafuata maji?
Maana ukiacha kitu hewani iwe object iwe liquid uelekeo ni ulele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…