Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Yaan we jamaa hamna kitu kabisa, pamoja na maelezo yako hayo umejipinda weee! Sasa kama dunia ni tambarare tunawezaje kupata usiku na mchana? Muda uliopo sasa mpigie mtu aliyeko USA au Australia akwambie ni saa ngapi? Kama ni tambarare basi kungekua na mchana au usiku dunia nzima, dah! Yaan we jamaa hamna kabisa, unamanini kwa kichwa yako?
 
Kuondoa ubishi si watume vyombi vyao wanavyoviamini angani watupigie hiyo picha inayoonyosha dunia ni tambarare manake satellites zoote zilizopo angani zinapiga picha ya dunia duara na sio kwamba satellites zote ni za mtu mmoja kuna hadi satellites za makampuni binafsi zoote hizo hawaziamini.. Haya kuna sayari zinaonekana kwa macho kabisa angani na ukitafuta hata darubini za kutengeneza mwenyewe unaweza kuziona vizuri kabisa kuwa ni kama tufe.. Mwezi ni umbile la tufe na kuna hadi picha walizopiga watu wa kawaida kabisa online za sayari na mwezi zinaonyesha umbile la tufe so whats so special about our earth iwe tofauti kabisa na sayari nyingine zote? Na huko pembezoni mwa dunia (kama ni flat) mwisho wake wapi? ISS skuizi wanarusha live coverage yake inavyozunguka dunia na popote inapopita inaonekana vizuri kabisa ukiwa duniani(kama ni mfuatiliaji wa mambo ya vitu vya angani) at the same time kama inavyoonyesha kwenye live coverage(hii ya ISS hata mimi nimeshaishuhudia mara kadhaa tu) na wapo wengi waliopinga hii live coverage kuwa ni feki na nasa walishatangaza anayeona ni feki athibitishe hamna hata mmoja... Hivi kweli mataifa mengine makubwa kama Russia anaweza akakubali kulishwa uwongo na watu kama nasa?
 
baharini kwenyewe kama ni tambarale mbona meli inapoanza kuonekana huanzia ncha ya juu na kuendelea kuonekana kama vile inaibuka kutoka ndani ya maji kidogo kidogo ? huo ni ushahidi rahisi sana kwamba dunia ni duara. halafu mtoa uzi kama alivyoambiwa inakuwaje nchi moja usiku na kwingine mchana ?
 
Ninyi acherni utoto kwa kujaza sever za JF bila sababu za msingi,majibu ya mlichouliza yapo kwenye uzi huu huu,someni....

Nashangaa sana watu wavivu kuja kusoma mada lakini hawataki kutumia muda kusoma post za wengine,yaanbi wanaanzia hapo walipokuta bila kufikiria kusoma post za wengine ili wajue kama wanachotaka kuuliza kimeshajibiwa au hapana.....

Sitegemei kabisa watu ambao wako interested na mada hii wawe wavivu namna hii,zaidi naona watu wasiojielewa wakija na kutaka kuvuruga tu hapa.....

Acheni watu wenye maswali ya maana waje waulize hapa ili tupate changamoto zaidi na wengine wajifunze.....
 
Mzee uzi tumeupitia tangu mwanzo hamna majibu mliyoweka zaidi ya hoja za kupinga kuwa dunia sio tufe.. Maelezo yote mliyoweka humu hayana hoja za msingi za kisayansi na zina maswali mengi zaidi ta hayo unayoita majibu.. Umeweka historia nyingi za watu na link zao wanaotetea flat earth.. Watu hapa wanachotaka ni physical evidence na sio maneno mengi na hoja za kukanusha... Weka hoja za uthibitisho wa unachokisema.. Umeulizwa maswali jibu na sio kupiga kelele tu mtu aanze mwanzo wakati hoja ulizoweka ndo zinazoleta hayo maswali unayoulizwa mzee..
 
kama kweli unataka kujua ukweli na ushahidi wa dunia tambarare, kitu cha lazima kwako ni kuwa wewe kama wewe kwa akili zako wewe, then kama ulivyofundishwa dunia ni DUARA kama mpira (mviringo) inabidi na hapa uwe tayari kufundishwa kuwa dunia ni DUARA kama sahani (tambarare)

baada ya hapo kwakuzitumia akili zako, utachanganua ipi ni ipi bila kulazimishwa na mtu wala kumkosoa mtu coz hakuna zawadi wala kombe la mshindi wa hoja na hatushindanishi hoja humu, zaidi ya kuujua ukweli kupitia mafundisho tuliyoletewa,

maswali yako na wenzako wengi yapo humu humu kwenye uzi so kama unabishana na maandishi ni ngumu kueleweshwa hata kwa ushahidi unaoutaka. kama umeshindwa kujua usiku na mchana unapatikana vp ktk dunia tambarare... fanya hivi, nenda kalale ukiamka anza tena kuusoma uzi huu kuanzia uzi wenyewe na kila aliyechangia....

NAPENDA KUKUSAIDIA TUU, MSAADA WANGU UPO KATIKA MAJIBU UTAKAYOYAPATA KATIKA MASWALI NINAYOKUPA. ILA KAMA UNAAMINI WE NI MBISHI NA HAUTAKI KUSHINDWA.. KAUSHA!!

SWALI LA KWANZA........ KUJUA KAMA DUNIA NI TAMBARARE AU DUARA MVIRINGO
kabla haujafundishwa kuwa Dunia ni Duara Mviringo, na baada ya kufundishwa hvyo. wewe kama wewe unaionaje, je ni mviringo au tambarare?... nipe ushahidi wako wewe vile unavyoiona, yaani bila kudeal na kitabu chochote kile wala elimu yoyote ile wala video wala picha, JE DUNIA NI DUARA MVIRINGO AU NI TAMBARARE?

SWALI LA PILI..... KUJUA USIKU NA MCHANA.
pamoja na nchi kutofautiana masaa na hali ya usiku na mchana... ni kwanini hakuna nchi zenye utofauti wa MASAA KUMI NA MAWILI...? yaani kama huku kwetu ni saa sita mchana, ni nchi gani itakuwa saa sita usiku? kwanini?

SWALI LA TATU.......... JUU YA KUPATA PICHA INAYOONESHA DUNIA NI TAMBARARE AU MVIRINGO.
angani ni wapi...... je picha unayoipata ukiwa katika ndege... inakuonesha nini.....utambarare au uduara? Kipi kina speed kati ya ndege na dunia?

UKIYAJIBU HAYO TUTAENDELEA KUBADILISHANA UELEWA.
Ila kabla ya yote napenda kukushirikisha kitu kimoja hivi..... hivi haufikirii kuwa kutokana na macho yetu kuwa katika hali ya uduara flani yanaweza kufanya kitu kinachokuwa mbali sana tukione katika hali ya uduara kutokana na kucover eneo kubwa la upeo. ukitumia jicho moja kuangalia na unapotumia macho yote unadhani kwanini haoni picha mbili mbili. maana yangu ni kwamba...... lens za kamera hazina utofauti na mfumo wa lens za macho yetu, ndio maana unachokiona wewe hakitakuwa tofauti na ukipiga picha japo lenzi ni ya duara ila picha itatoka mstatiri, so tufikirie kiundani kama macho yetu yanapofika ukomo wa kuona kwanini yanaform taswira ya uduara. tena hilo duara huwa ni mbele ya upeo na angani tuu ila pembeni na ardhini uduara huwa hatuuoni, huwa ni kwanini, mimi mwenyewe natafuta majibu hayo.
kwa mfano baharini, kweli meli ikiwa inakuja kutoka mbali utaanza kuiona sehemu ya juu kwa macho ila kwa darubini inaonekana yote, (kabla ya kubisha uwe umejaribu zoezi hilo) vile vile ukitazama hiyo meli kwa umbali ule ule uliouiona pindi unaangali mbele, ukiiangalia kwa usawa wa mashariki magharibi napo utaiona yote, ili kunielewa namaanisha meli inaonekanaga nusu mtu anapoiangalia kwa usawa wa mbele, lakini kwa usawa wa pembeni inaonekana yote (pitia picha ya mleta uzi).
So kama macho yetu utengeneza uduara hakuna camera itakayokwenda kinyume na macho yetu. so ushahidi wa camera ni sawa na ushahidi wa macho tuu, kwa hiyo hata watu wa flat earth wakipiga picha uduara utaendelea kuonekana labda wabuni lens zao mpya za camera zisizofanan na lens za macho yetu.
pia kwa speed inayotumiwa na dunia katika kujizungusha hata mimi nitasema hiyo live streaming ya ISS ni uongo labda wawe wameweka slow motion.
 



Duhh we jamaa wa ajabu sana..hoja zote unazotoa ni zile za kupinga tu kuwa Earth sio tufe na kwamba tulifundishwa vibaya na tunapewa picha za kutungwa. Ila huleti facts za kuelewka zaidi ya hoja zinazoongeza maswali na kuendelea kung'ang'ania kuwa ulishatoa majibu(ambayo bado yanaleta maswali)... Sasa kama unasema camera zinazotumika zinafanana la lens za macho na zinatoa picha feki ya dunia kwa sababu ya lens ya duara kwaiyo hata macho yetu yanatupa picha nyingi ambazo ni feki hivyo kuna vitu vingi tunavyoviona ni feki maana unasema hizi camera ambazo zinafanana kila kitu na macho yetu haziaminiki sasa tutayaaminije macho yetu... Hizo camera mnazozitumia ardhini kuonyesha flat earth kwa nini msizitumie hizo kutupigia picha from above tukaiona jinsi dunia yote ilivyotambarare? Au hamziamini hizo camera sababu zikiwa kwa juu zinadanganya au...? Kama mnaweza kuiona meli ikiwa mbali kuwa dunia ni tambarare mziboreshe hizo kamera then mtupigie picha ya full earth..? Afu hiyo flat earth chini imeshikiliwa na nini sasa... Inaelea? Kama inaelea wat follows ukifika ukingoni mwake....?

Afu unataka kusema hapa ikiwa ni saa sita basi dunia yote ni sasa sita? Basi we noma! Hiyo ya 12+ diff ipo mzee.. Mfano Morocco ni GMT0 na fiji ni GMT +12 so tofauti ya mda baina yao ni 12 hours mzee.. Kama huamini hata hilo tafuta watu wa huko uwaulize manake nikisema usearch Google utasema wanadanganya... Na kama unaamini kama hapa kwetu ni mchana basi kuna nchi ni usiku thena wats happening hapo...inakuaje kama dunia ni flat? Hizo hoja zako zote za ndege mzee hazina maana... Hivi hujiulizi mbona nzi ndani ya gari akiwa anaruka anaenda pamoja na gari... Kwa nini asiwe anaachwa mpka anajigonga nyuma ya gari? Sababu ni sehem ya gari kwa mda huo...yupo ndani ya atmosphere ya gari... Hakuna ndege inayoweza kuruka nje ya atmosphere ya dunia mpaka ikaachwa kwa sababu ya mzunguko wa dunia.. Atmosphere ya dunia mzee inaenda mpaka 700km above surfaces na ndege haiendi zaidi ya 20km above earth.. Mambo mengine hayahitaji hata kutumia nguvu mzee.. Kwaiyo pia unataka kusema hao wanaoamini flat earth hamna hata mwenye uwezo kisayansi akaingia mashirika makubwa ya kisayansi na kutupa data za ukweli kuhusu hiyo flat earth?

Majibu ya maswali yako:
1. Haya mambo yote mzee tumejifunza tu hamna mtu amezaliwa anajua... Ila unachojifunza kinabebwa na facts.. Kama kuna ushahidi unaonekana kwa macho then its proven... Nimefundishwa dunia duara.. Wanasayansi woote hata wale wa kale kabisa wasiokuwa na vifaa vya kisasa walili prove hilo.. Mimi mwenyewe naona tofauti ya masaa hapa duniani.. Mwezi unaonekana kwa macho jua linaonekana kwa macho na zipo sayari zinaonekaka kwa mcho zote hizo ni tufe na satellites kbao hadi za watu binafsi zimejaa kibao zote zinaprove same thing..

2. Swali la pili nimekujibi hapo juu.. Chukua tu Morocco na Fiji ni tofauti ya masaa 12..na nchi nyingine zoote ambazo ni GMT 0 na GMT 12..

3. Unauliza juu ni wapi? Sasa kitu kikiwa tambarare juu ni wapi? Duh kazi ipo! Yaan we unasema dunia ni tambarare ila hamjui juu ni wapi ndo maana hamwezi kupiga picha ya dunia.... Ndege inaruka umbali mdogo sasa mzee kutokea ardhini ukilinganisha na ukubwa wa dunia..na huwezi kuona dunia nzima ukiwa juu ya ndege ila ingekuwa ni flat labda ungeweza kuiona dunia nzima.. Kama unataka picha ya dunia lazima uwe umbali wa kutosha na ndo maana nikasema nyie sasa ndo mtumie kamera zenu..mtupigie hiyo picha ya flat earth ya dunia nzima tuione..ila hampajui juu ni wapi......kuhusu speed ya ndege na dunia mzee hata ku search kidogo tu.. Aaah huiamini google...sorry! Hivi nzi na gari kipi kina speed kubwa.. Mbona nzi aliye ndani ya gari anaruka kwa uhuru anaoutaka bila kuonekana kuachwa na gari wakati gari ipo speed 130km/hr?
 
Afu unasema ISS ni slow motion? Kama unajua speed ya dunia kujizungusha na speed ya ISS kuzunguka dunia wala usingetoa hoja hiyo! Kitu kinachoenda speed ya 120 na kile cha 125 Kuna tofauti ya speed ya 5 hapo ambayo itaonekana ni ndogo sana kqa sababu ni relative speed... Unless useme na physics inadanganya... Mzee kwa technologia iliyopo saiz huwezi kudanganya kila mtu... Sayansi ni tofauti na imani mzee kwenye imani kuna vitu tunaamini bila kujali vinaonekanaje mzee ila sayansi is based on facts.. So dont mix science and faith baba.. Hata mimi ki imani naamini Biblia na yote yaliyomo na namuamini Mungu pia ila ki Science ina nafasi yake na hii ni kidunia tu na sio ki imani.. Science inatupa nafasi tu ya kuelewa mazingra yetu jinsi yalivyo .. Mfano creation kisayansi ni tofauti kabisa na kiimani na mimi naiamini imani ipo sa hihi.. So usijivuruge kwa kuchanganya imani na Science..
 
Kuna mtu ameuliza hapo juu kuwa "kama dunia ni flat unawezaje kupata usiku na mchana"? Swali hili limejibiwa na hadi picha ya mfano imewekwa,watu wenye akili hujibu kilichojibiwa na siyo kuuliza swali lilelile lililojibiwa,hii ni kuonesha aliyeuliza hajielewi kabisa.....
Watu hapa wanachotaka ni physical evidence na sio maneno mengi na hoja za kukanusha...
Duh!!


Unataka physical evidence kwenye forum? Unajua hata unachohitaji kweli jombaa?
Weka hoja za uthibitisho wa unachokisema..
To begin with,kuna uthibitisho upi kuwa dunia ni duara?Hoja zote ambazo zilionekana kuonesha dunia ni duara zimejibiwa,hili linaonbesha umedanganya kuwa umesoma mada yote hii..
Umeulizwa maswali jibu na sio kupiga kelele tu mtu aanze mwanzo wakati hoja ulizoweka ndo zinazoleta hayo maswali unayoulizwa mzee..
Yaani mtu aulize mchana na usiku unapatikanaje halafu ajibiwe,ndiyo izae swali la mchana na usiku unapatikanaje?

Nyie watu ni shida sana....
 
Hahahaa... Kila swali unalouliza unaambiwa limeshajibiwa ukitafuta unakuta maelezo yanayoleta maswali zaidi na ukiuliza unaambiwa umeshajibiwa... Picha mmeweka za mifano ukiuliza kwa nini wasipige picha ya dunia nzima sasa mtuwekee hapa mnaleta michoro ya kuchora.. Picha za wenzenu walizopiga mnasema feki za kutengeneza ila mlizopiga nyie kwa kutumia kamera hizohizo walizotengeneza wao ndo sahihi ila hamuwezi kutuwekea picha halisi ya dunia nzima kwa pamoja..

Mzee physical evidence kwenye forum ni picha halisi au video ya kitu husika.. Najua kuna picha na video za kutengeneza ila technology hiyo hiyo bado inaweza kutambua feki na original.. Sasa kwanini msiweke hiyo mnayoamini ni original ya flat earth?

Nyie ni sawa na mtu umemwambia nimeenda baharini huko nikakuta kuna sehem kuna bonge la nyumba..vifaa nilivyoondea nimekuonyesha ukitaka na wewe uende unabisha hamna nyumba baharini huku hata ufukweni mwa bahari hujawahi kufika ila unambishia yule aliekwambia amefika.. The only way ya kukataa ni wewe kwenda huko na kuthibitisha kuwa ni uwongo sio kutumia nadharia na kuanza kujenga hoja zisizokuwa na evidence..

Hoja yenu ya flat earth hatukatia inaweza kuwa kweli sawa ila how? Maswali ni mengi kuliko majibu mnayotoa ambayo hayajitoshelezi.. Na majibu yote mnayotoa yapo kinadharia zaidi ya vitendo.. Fanyeni kwa vitendo then tutaamini... Tumeni chombo au watu wenu mnaowaamini juu kabisa then watuletee picha au video ya hiyo flat earth mnayotuambia...its that simple..! Zaidi ya hapo ni maneno matupu tu ya kiimani zaidi ya ki science... Technology iliyopo saizi mzee unaweza ukathibitisha chochote kile unachohitaji ki Science.. Watu wanaenda space nyie mnasema waongo, satellite zipo huko mnakataa.. Ila mnaamini live coverage za mipira na vitu vingine vinavyorushwa kwa kutumia satellites hizo hizo zinazotuma picha ya dunia... Taabu sana.. Mnaongea sanan ila mpaka sasa hamna picha wala video hata moja inayoonyesha dunia yote kwa pamoja ikiwa flat...sababu hamna technology ya kuthibitisha hilo ila mnakataa technology iliyopo inayothibitisha dunia ni tufe..
 
Asante saaaana Mkuu!
 
Aha ha ha ha jamaa kajiwahi kujiona yeye ni wakala wa ibilisi halafu anakusingizia wewe.
 
Duh, mbona unaandika kwa mihemko kiasi hiki mkuu?? Kuna nini??
Ishu hapa nibkwamba hatujakubaliana kimtazamo, mfanyakazi wa shetani anatoka wapi tena!!
Tufanye "nimekuelewa", case closed kati ya mimi na wewe, HAPPY NOW??
Cheerz!
Wewe kweli barafu ya moto.
 
Halafu tujiulize kuwa kwanini Mungu alimwambia Joshua asimamishe Jua na si dunia ikiwa dunia nayo inazunguka.
 
Hahahaa... Kila swali unalouliza unaambiwa limeshajibiwa ukitafuta unakuta maelezo yanayoleta maswali zaidi na ukiuliza unaambiwa umeshajibiwa...
Hatusemi na wala sisemi yamejibiwa kwasabau nataka kusema hivyo bali ninakuambia kitu ambacho ni kweli kabisa,uzuri nimekueleza pia kwamba ni namna ipi unapaswa kufanya swali linapokuwa limejibiwa kwa majibu ambayo wewe hujayakubali...

tatizo unaonekana uko hapa kiushabiki na kushindana zaidi na ukidhani kila mtu hapa anashindana kitu ambacho siyo kweli.Tupo hapa kusaidiana kuuona uhalisia....
Picha mmeweka za mifano ukiuliza kwa nini wasipige picha ya dunia nzima sasa mtuwekee hapa mnaleta michoro ya kuchora..
Wakati mwingine mnashangaza sana ninyi watu....

Ukiambiwa unadanganya na hujasoma mada unakataa.Mtoa mada amesema ni kwanini hakuna picha iliyoweza kupiga dunia nzima kama ilivyo,hapa naona unakuja na hoja ile ile ambnayo imeshajibiwa.Ambacho unapaswa kukifanya wewe siyo kupoteza muda kuuliza vitu ambavyo utaonekana tu unafanya ushabiki,soma mada kisha uulize maswali yanayoeleweka....

Mwenye busara angekuja na hoja kupinga hoja ya mtoa mada aliyosema ni kwanini haiwezekani kupiga picha dunia yote na siyo kuja na hoja ya kumtaka alete picha ya kitu ambacho alishasema haiwezekaniki kiwepo.....
Picha za wenzenu walizopiga mnasema feki za kutengeneza ila mlizopiga nyie kwa kutumia kamera hizohizo walizotengeneza wao ndo sahihi ila hamuwezi kutuwekea picha halisi ya dunia nzima kwa pamoja..
Mtoa mada ameshasema kuwa wao ambao wanasema kwamba wanakwenda huko angali mbali kabisa nje ya anga ya dunia wanaweza kuona na vyombo vyao vimepiga picha,cha ajabu ni kwamba zile picha siyo hata za kamera ambazo zimeonekana nazo zina sida bali ni picha za kutengeneza.Hii ina maana kwamba hakuna picha hata ya kamera a mabayo ni halisi ikionesha dunia ilivyo kutoka kwenye vyombo vya hao wanaosema kuwa wanakwenda huko anga za mbali na kuiona dunia kwa vifaa vyao,unadhani swali la picha anapaswa alijibu nani?

Hoja yako ya picha halisi ni ya ajabu na nimeishaielezea hapo juu....
Mzee physical evidence kwenye forum ni picha halisi au video ya kitu husika..
Picha na video zinaweza kuwa manipulated kama hujui na hivyo siyo ushahidi katika mambo haya.Ndiyo maana nilikuambia kuwa inawezekana hujui unachohitaji.....
Najua kuna picha na video za kutengeneza ila technology hiyo hiyo bado inaweza kutambua feki na original.. Sasa kwanini msiweke hiyo mnayoamini ni original ya flat earth?
Hili swali nimeshalijibu hapo juu....
Tatizo hujaliona bado....

Huwezi kuniambia umeenda huko ukiwa na vifaa ambavyo unaweza kupiga picha na kuchukua video kwa mfano,halafu uje huna picha na video halafu uniambie tu nikuamini.Kwanini hukupiga picha? Kwanini huna ushahidi wa maneno yako?

Hadithi za kufikirika hizi....
Hoja yenu ya flat earth hatukatia inaweza kuwa kweli sawa ila how?
Kwanza hoja hii siyo yangu,mimi ni mtu ninayehoji na kujihoji,natafuta ukweli,hoja na mtoa mada ina mashiko,kwanini nisihoji na kujihoji?

Au kwako wewe mtu anayehoji jambo anakuwa amelikana au kulikubali?
Inaweza kuwa ni kweli kuna maswali zaidi ya majibu,lakini hayo maswalikila mtu ana wajibu wa kujibu siyo kundi fulani tu.Kwakuwa wameshakuonesha kuwa inawezekana kuna mahali umedanganywa ni jukumu lako kuutafuta ukweli na siyo kumbebesha aliyekuonesha uwezekano huo wa kudanganywa.....

Nakushauri uusome huu uzi utapata jibu la hoja yako ya kuhusu kutuma chombo.Ndiyo maana nakuambia hgujasoma hii mada lakini unabisha,unajenga hoja kutoka kwenye mambo ambayo yana majibu humu,acha uvivu....
Zaidi ya hapo ni maneno matupu tu ya kiimani zaidi ya ki science...
Dunia kuwa duara ni imani vile vile,hakuna uthibitisho,kama unao nipe....
Technology iliyopo saizi mzee unaweza ukathibitisha chochote kile unachohitaji ki Science..
Naomba uthibitishe wewe upo na siyo kwamba unaota....

Tumia sayansi yako hapa....
Watu wanaenda space nyie mnasema waongo, satellite zipo huko mnakataa.. Ila mnaamini live coverage za mipira na vitu vingine vinavyorushwa kwa kutumia satellites hizo hizo zinazotuma picha ya dunia... Taabu sana..
Haya yote una uthibitisho au umeambiwa tu na wewe umeyemeza tu?

Unajua hata maana ya uthibitiosho?
Mnaongea sanan ila mpaka sasa hamna picha wala video hata moja inayoonyesha dunia yote kwa pamoja ikiwa flat...sababu hamna technology ya kuthibitisha hilo ila mnakataa technology iliyopo inayothibitisha dunia ni tufe..

Soma mada na angalia kama unasoma kwa makini acha kujadili mambo ambayo unaona uvivu kuyafuatilia....
 
Hahahaa... Mzee nimesoma mada vizuri tangu mwanzo na kama ulivyosema swala sio kubishana ila ni kuelimishana na pale ninapokuwa na swali inanibidi kuuliza.. Nasema hoja za flat earth zina maswali mengi zaidi ya majibu sababu inaonesha kwa hoja hizo kuwa haiwezekani kupiga picha ya dunia yote kwa pamoja ila mnaweza kuichora kwa kutumia hizo theories.. Kwaiyo kwa kifupi unasema kwa technologia yooote tuliyonayo saiz HAIWEZEKANI kupata picha ya dunia yote na kuona umbile lake kwa pamoja...? Kwaiyo unasema pia picha zooote zinazopigwa na satellite zote hizo zilizopo angani ni feki maana yake tusiamini kitu chochote kinachorushwa kwa njia ya satellite? Manake maelezo yenu asilimia kubwa ni kwamba technology yote iliyopo saiz inaongozwa na hao ma secrets society na ndo waliobuni huu uongo wa dunia tufe au sio? Kwaiyo kwa kifupi tusiiamini hii technology...
 
Dunia haiwezi kuwa flat hata siku moja. Simple answer ni kama dunia ingekuwa flat kusingekuwa na nyakati tofauti.
 
hapo naomba kutafautiana na wewe. Inamaana wakati huo wazungu walikuwa hawajajuwa kuwa dunia ni mduara. kwa sababu walikuja kujuwa kuwa dunia ni duara karne ya 14 AD
Mimi najuwa kuwa dunia ni duara. nilifanya utafuti kwa kuweka nguzo za miti. ilikuwa wakati wa kiangazi. Mti wa kwanza asubuhi, kivuli chake huoni kinaishia wapi. lakini ikifika kuanzia saa 3 au 4 ndiyo unaona kivuli kinaonekana kutokea magarbi kurudi mashariki.
hii ikanipa picha kwa mfano ukiwa unasafiri kwenye gari na uko kwenye spidi kali. Utaona kuwa miti au vitu ambavyo havihamishiki vinakimbia kukufata. wakati ukweli wewe ndiye unakimbia kwenye gari kuvielekea. hii ni wazi kuwa dunia ndiyo inazunguka juwa kilekivuli cha miti nilile juwa unona lina hama wakati dunia ndiyo ina hama. Hivyo dunia ni mduara ndiyo maana kuna usiku na mchana.
Hivyo ndivyo nilivyo elewa.
 
Huwezi kuwa umesoma mada halafu unaendelea kuuliza maswali yale yale tu unless uwe huelewi unachosoma au unachouliza...

Unachopaswa kukifanya wewe ni kuonesha inawezekana kupiga picha dunia yote na siyo kuendelea kuuliza maswali yale yale tu....
Kwaiyo unasema pia picha zooote zinazopigwa na satellite zote hizo zilizopo angani ni feki maana yake tusiamini kitu chochote kinachorushwa kwa njia ya satellite?
Ndigu,nakushauri uache kuendelea kupost hapa maana unaendelea kuonekana wa ajabu zaidi....

Mtoa mada ameeleza ni aina ipi ya picha unazodhani ni halisi,unaweza kukagua ili kuona kama amedanganya au hajadanganya,unapoendelea kupost post za namna hii hapa unaendelea kujionesha namna ulivyo,nakushauri acha au anza kuhoji mambo ya msingi....

Kama unaona uvivu kusoma mada acha kubisha kishabiki hapa......
Manake maelezo yenu asilimia kubwa ni kwamba technology yote iliyopo saiz inaongozwa na hao ma secrets society na ndo waliobuni huu uongo wa dunia tufe au sio? Kwaiyo kwa kifupi tusiiamini hii technology...
Hunaelewa mambo kinyume kabisa....

Kukosoa kitu siyo kukana uwezo wake.Unahoji uwezo wa teknolojia,hivi unadhani unahitaji teknolojia yenye uwezi upi kuweza kupiga picha dunia yote?

Halafu mbona hujathibitisha uwepo wako jombaa? Maana ulisema inawezekana,au hukuona hili swali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…