Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710

Kushoto hapo ni picha ya dunia na mwezi imepigwa kutoka mars( zoom in ili uone vzr) kulia ni picha ya mars imepigwa hapa duniani. Mars na earth zimefanana umbo ila hakuna anaesema mars ni flat
 
View attachment 439435
Kushoto hapo ni picha ya dunia na mwezi imepigwa kutoka mars( zoom in ili uone vzr) kulia ni picha ya mars imepigwa hapa duniani. Mars na earth zimefanana umbo ila hakuna anaesema mars ni flat
Mzee wenyewe wanakwambia hizo picha ni feki eti ni za kutengeneza na hamna mtu alieenda outer space.. Na hata hizo satellite wanazosema zipo juu huko ni uwongo... So mzee jiandae kuambiwa hata hizi live events zinazurushwa live kwa satellites kutoka sehem moja kwenda ingine kama mpira ni feki.. Wanakataa kama kuna kitu kinaweza kuleta picha ya dunia kutoka angani, hao waliopiga hizo tunaambiwa tunadanganywa.. Nasa waongo, wajapani waongo warusi waongo wahindi wakorea waongo. Wahindi waongo na woote wanaosema wamerusha satellites angani ni waongo ingawa hizo satellites zinavyokuwa zinaondoka duniani hapa huwa watu wanaona live kutoka lunch pad na live coverage zinakuwepo pia ila hivyo vyote ni feki according to flat earth community ... So unafanya kazi bure tu kuweka picha..
 
Cha ajabu kuhusu hawa watu hata kutengeneza baskeli hawawezi ila ukiwaambia nasa wamepeleka chombo mars wanakataa. Sasa unabisha vp kitu ambacho huna uelewa nacho? Ingekua Russia ndio wamesema nasa ni waongo hapo kweli ningeamini...halafu mbona ISS inaonekana vizuri tu bila hata darubini unaweza kuiona inapita juu sema hawa watu ni wabishi sana Hata ukiwaonesha watasema ni ndege.
 
ISS ipo kabisa hata mimi kila baada ya siku mbili naiona, nina application kwenye simu yangu inaitwa iss detector kila wakati iss ikipita nyakati za usiku inanipa taarifa,kama kuna mtu anaitaka anaenda playstore kwa simu zinazotumia android OS inaitwa ISS detector, uki download una set longitude na latitude za mahali ulipo nimei screenshot hapa


 
Yeah hii application ipo vizuri hata kwenye website ya nasa pia unaweza kuona inapita mda gani sehemu ulipo.
 
Yeah hii application ipo vizuri hata kwenye website ya nasa pia unaweza kuona inapita mda gani sehemu ulipo.
Picha za iss zinaonyesha kabisa dunia ni duara sasa hawa wanaosema tambarare sijui wanatoa wapi data zao
 
Mkuu kama picha za satelite zinaweza kuonyesha mabara yote, iweje jua lishindwe kumulika mabara yote!? Pia jamaa alisema kwamba dunia imetulia na haina movment yeyote bali jua na vingine ndo vinazunguka dunia na akahoji pia kama dunia inazunguka kwa kasi mbona hatuhisi huo mzunguko?

Kuna nyakati hasa za usiku sana ukitoka nje pametuliaaa...! Hakuna hata upepo, huo mzunguko ni wa aina gani ambao hauwezi hata kuhisi upepo?

Na zaidi kimfano mvua inaweza kunyesha labda masaa 7 eneo flani tu, ni kwa nn iendelee kunyesha hapo hapo tu ilhali dunia inazunguka!? Au na mawingu ya mvua nayo yanazunguka pamoja na dunia?

Haya mambo hayahitaji hasira, ukifikiria kwa makini kuna maswali mengi hayana majibu ya kuridhisha, na mwanasayansi wa kwanza aliesema dunia inazunguka alihukumiwa kifo baada ya kukataa kukanusha kauli yake!

Dunia ina milima na mabonde kijiji A wanaweza kuliona jua saa 1 asubui lakini kijiji B wakaliona saa 3 hapahapa tz sembuse huko mbali!
 
Wawakamatishe uongo wao sio kuishia kusema picha ni feki ndio eti sisi tuwaamini.
 
Lini inaweza kupita tena anga la dar mkuu? Na ikipita unaitambuaje yaani inaonekana vipi?
 
Lini inaweza kupita tena anga la dar mkuu? Na ikipita unaitambuaje yaani inaonekana vipi?
itapita Sunday November 27 saa 1925,huwa inaonekana kama nyota inayotembea ukiangalia angani utazani ka nyota kadogo ila tofauti yake hii inatembea
 
itapita Sunday November 27 saa 1925,huwa inaonekana kama nyota inayotembea ukiangalia angani utazani ka nyota kadogo ila tofauti yake hii inatembea
Mara nyingi naziona satelllie(kama vinyota vinatembea) kama hizo zikikatiza angani usiku . kumbe muonekano ni kama satellite nyingine tu
 
Mara nyingi naziona satelllie(kama vinyota vinatembea) kama hizo zikikatiza angani usiku . kumbe muonekano ni kama satellite nyingine tu
Ndio muonekano wake kama satellite nyingine tu ila yenyewe ni kubwa kiasi
 

Mkuu hili swala la mzunguko wa dunia limezungumziwa sana na hao flat earth ndo sehemu kubwa waliongangania... Kuna sehem humu nimetoa mfano kuwa inzi iliyepo ndani ya basi linalokimbia 100+ km/hr kwa nini anaweza kuruka ndani ya basi kwa uhuru bila kuonekana kama anaachwa na akajigonge nyuma kabisa ya gari? Shida watu wanapoingelea mzunguko wa dunia wanajifanya kuwa hawajui kama kuna atmosphere.. Dunia ni ardhi pamoja na atmosphere yake ambayo mzee inaenda mamia ya km above earth.. So MZUNGUKO WA DUNIA SIO MZUNGUKO WA ARDHI PEKE YAKE bali ni mzunguko wa ardhi pamoja na atmosphere yake na ndo maana kila kilichopo ndani yake kama ndege, mvua nk kinamuv pamoja kama ilivyo inzi ndani ya gari hata liwe na speed vipi.. Watu walisema ndege sjui kwa nini haiachwi hakuna ndege inayoruka zaid ya 40kms above earth jamani na atmosphere inakwenda zaid ya 700km above earth sana sana kinachobadilika ni layer za hewa iliyopo kadri unavyopanda juu.. So ndege na vyote vilivyomo ndani ya atmosphere ni kama inzi ndani gari tu..gari inatembea na inzi anaweza kuruka freely ndani ya gari...

Afu mkuu hakuna picha ya satellite inayoonyesha mabara yote kwa pamoja.. Picha zote za satellites huwa zinaonyesha sehem ya dunia ambapo imeelekea mda huo ila sehemu ndogo ya mabara ya pembeni yake tu ndo inaonekana.. Ila hio michoro ya flat earht ndo inaoonyesha mabara yote kwa pamoja..

Hilo swala la milima kuzui jua mzee upo chaka..kwaiyo tanzania ikiwa mchana brazil huko(au nchi nyingine ambayo inakuwa ni usku) kunakuwa usku sababu ya milima? Kama dunia ingekuwa ni flat basi dunia nzima kuna mda tungeweza kuliona jua kwa wakati mmoja hata kungekuwa na milima mirefu kama nini sababu jua linakuwa juu(labda usema kama kuna milima imekaa kama meza na kuna nchi chini yake) zaidi ya hapo mkuu dar ikiwa jua linachomoza ndo maana unakuta kigoma huko bado ni usku sio sababu ya milima kwanza kigoma ipo juu ukilinganisha na dar kama dunia ni flat tulitegemea maeneo yote yalio juu kama kigoma ndo yangeanza kuliona jua.. Badala yake jua likizama tu dar mpigie mtu wa kigoma muulize atakwambia ndo kwanza jua linakaribia kuzama ila bado linaonekana au muulize jua huwa linapotea mida gani afu linganisha na dar..

Flat earthers wengi hawaamini uwepo hata wa satellite angani ila wanaamini events mbalimbali ambzo zinarushwa na satellites hizohizo kama mpira nk ila picha za dunia hawaziamini wanasema za kutengeneza... Ipo siku hata hii mipira tunayoangaliaga kwenye tv tutaambiwa ni ya kutengeneza...
 
Shkamoo!
 
Taratibu Mkuu wataelewa tu. Mimi binafsi nasoma taratiiibu huu uzi ili nielewe zaidi, binafsi namshkuru Mungu akili zangu huwa hazijafungwa ndani ya Box.

Ngoja tusubiri majibu ya maswali uliyomuuluza. Sasa hivi na mimi najiuliza, aliyechora ramani ya dunia na mipaka yake kwa kila nchi alikaa wapi!?

Ngoja tuendelee kujifunza.
 
Mkuu umetoa somo zuri, ila kwemye INTRO umenichanganya! Umewaponda wazungu na elimu waliyotuletea na wanavyoendelea kutudanganya na kutuficha mambo, wakati huo huo unatuelimisha kwa kutumia lugha, vyombo na elimu hiyo hiyo ya hao jamaa..!!
Hadi Wikipedia ni mali yao hao. . . . Internet yenyewe ni yao. . . . Kweli ambaye hakumwelewa Trump kuhusu mtu mweusi atakua anapenda kuishi uwongo kuji please!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…