Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Nimekuambia thibitisha jinsi maji yanavyostick kwenye dunia tufe linalozunguka........

Kusema tu gravity,.haimaanishi umethibitisha "THIBITISHA.........au hujui maana ya kuthibitisha.
Unataka nikuletee GRAVITY unione au? Nimekwambia sababu ni gravity na nimekueleza jinsi gravity in work, au unataka nithibitishe nn kuhusu gravity?
 
Ndiyo nina uhakika 100%,...............hujaleta uthibitisho. yaani wewe ukitamka neno "GRAVITY" ndiyo unaona tayari ushathibitisha hapo?

Unajua maana ya kuthibitisha.
Unataka nithibitishe nini kuhusu gravity? Uwepo wake au?
 
K
hadithi za gravity hazitokuokoa bali you are just beating around the bush.....
Kama hazitoniikoa nijibu ni kwann vitu vinafall😀😀😀, kwann unalikimbia hili swali?? Na Bado hujajibu maswala yako ya Illusion na refraction lkn Bado uko hapa kuuliza maswali yako ambayo nayajibu.
ACHA UOGA.
 
.Badala ya kuleta uthibitisho unaingizia gravity ukiambiwa thibitisha basi gravity inafanya vipi maji yastick kwenye ball 🌎 huwezi.....
Wewe kweli kichwa wazi😀😀,
Kwanza unakubaliana namm Kuna kitu kinaitwa GRAVITY na kinatokea??

Nataka nikufundishe GRAVITY tu kwanza maana nishagundua hujui lolote kuhusu gravity 😀
 
hateeb10 au hapa nilikuwa nimemjibu nani?? Acha Janja Janja kijana😀
 
Hapa kama hukupaona???
 
Unataka maelezo gani zaidi,... Umekubali kwamba technically Jua halizami wala kuchomoza,..that means hicho unachokiona is just an illusion..na sio uhalisia......nikakugusia kuhusu refraction hutaki kwenda kusoma usaidiwe vipi sasa?
Swala la ww kujibu hoja zako limekushinda sasa, naomba nijibu kwanza maswali yangu yote then ndio tuendelee. Mwanzo nilikuambia naomba unieleweshe kuhusu Dunia yako tambarare Kwa unavyojua umerukaruka wee umekomaa kuniuliza mm maswali. Inamaana ww hujui chochote kuhusu unachokitetea??
 
Unataka nikuletee GRAVITY unione au? Nimekwambia sababu ni gravity na nimekueleza jinsi gravity in work, au unataka nithibitishe nn kuhusu gravity?
Yeye kwenye sunset easy tu anakwambia ni illusion,

Na haitolei maelezo yoyote yale
 
NkumbiSon umekuja kushangaa tu, umeshindwa kuleta hoja?
 
katika uzi huu nimejaribu kutumia lugha rahisi na mifano rahisi kuweza kuelewa kwanini naamini tumedanganywa kuwa dunia ni tufe.

kuna mdau kasema nimekimbia, kwa mwandiko huu atajikosoa kauli yake, ni hivi mimi sibishani na sishindani kuwa nani ni mkweli au nani muongo. hapa hoja ni KWAKUTUMIA AKILI ZAKO NA MILANGO YAKO YA FAHAMU Je Unajiona upo katika umbo gani la dunia, je Jua linaonekana likimove au limesimama? je unahisi Dunia inazunguka au imetulia?

Ukija kwakujiandaa kushindani Shinda wewe, ukija kwa nia ya kubishana mimi siwezi, ndio maana kwa sasa sintoreply post ya kutaka tubishane zaidi ya zile za kutaka tuelimishane.

Kwa post hii nitajaribu kuzijibu hoja zilizopo kwa njia rahisi tuu ili tuelimishane.

Ni hivi, dunia ni Kubwa sana kubwa haswa, hapo wote tunakubaliana juu ya ukubwa huo. halafu ni Duara, hapa tuelewane hakuna sehemu FlatEarth tumepinga kua dunia ni Duara so hoja za wanaolikataa umbo hilo zisijikite katika Uduara wa umbo la dunia na hata U flat wake tusiulinganishe na sakau au Tiles. bali ni eneo kubwa sana lenye hali ya utambarare huku milima mito na mabonde vikiwa ndani ya eneo hilo lililozungukwa na maji ya Bahari yanayokingwa na Kingo za Barafu kuizunguka duara la Dunia hiyo.

Hoja ni Tufe na Sahani. kwenye riadha kuna michezo ya kurusha Tufe na Kurusha Sahani so tudeal na shape za vitu hivyo kuwakilisha shape za Dunia tuliyoisoma Darasani na shape ya Dunia isiyofundishwa Darasani. Niliwajibu waliouliza kwanini naamini tunadanganywa namna tunavyofundishwa shape ya dunia kua kama tufe. niliwajibu kwa kifupi kua huo ni Mchongo wa shetani kupitia Elimu kuwalaghai wanadamu wamwabudu yeye na wasiuamini uwepo wa Mungu anaestahili kuabudiwa yeye peke yake.

kuna hoja ya kwanini naipinga Sayansi lakini natumia vitu vitokanavyo na sayansi ambayo ni shetani.
Jibu ni hivi, huu ni mpango System inayotaka kila Mwanadamu amuamini shetani kwa kumwabudu yeye kama ndio Mungu mwenye uweza wa vyote. So ni jukumu la sisi wanadamu kutambua mitego ya Ibilisi na kuiruka kwasababu hana alichokibuni hapa chini ya jua zaidi ya kudanganya, uongo ndio silaha kubwa ya shetani.

so hata hizi device tunazotumia ni moja ya njia ya Ulaghai wa shetani kwa wale wasiomcha Mungu watamuamini yeye na bila yeye hakuna litakalofanyika so unakua umenasa moja kwa moja kwake. SWALI kwa aliyehoji hilo, Je Bila kitu gani kilichotokana na Sayansi na kipo kwa matumizi ya sisi wanadamu, pindi kikikosekana Uhai utakua Basi? Namaanisha kipi ukifanyacho kwa simu au Computer hakiwezi kufanyika bila hivyo vitu? je mwanadamu kazidiwa uwezo wa kiakili na hizi device?

Jibu langu Sasa, Natumia hivi vitu vya kishetani kwasababu natambua namna ya kuukwepa ulaghai wake na Nikabaki namwabudu Mungu kwakua ni Muweza wa vyote na Shetani hajaweza kufanya kitu kinachomzidi uwezo Mwanadamu, bado hajafanikiwa nandio maana kila kilichotokana na Sayansi (Shetani) Kinamhitaji Mwanadamu Kukiendesha. na yule ashindwae kukiendesha na kikawa kinamuendesha basi anakua kanasa katika lengo la shetani kuabudiwa.

Turudi kwenye maswali na majibu sasa.
narudia. Jua ni Dogo kuliko Dunia na ndilo linaloizunguka dunia iliyotulia bila kulizunguka jua au kuzunguka yenyewe kwenye mhimili wake. Nathibitisha hili kwakuliangalia Jua kwa macho yangu nakuliona likiwa linasogea kutoka point moja kwenda nyingine. Nathibitisha Dunia haizunguki kwasababu sijawahi kuhisi hivyo kua nipo katika likitu linalozunguka. Naamini tumedanganywa hayo kwasababu TUMEFUNDISHWA DARASANI... ukweli wa hii hoja yangu ni majibu ya Mtu au Mtoto ambaye hajawahi kufundishwa kabisa, ukimuuliza atakwambia Jua linasogea/kutembea na Dunia imetulia na hawezi kuamini yupo katika Tufe linalozunguka kwa maana anaamini kuna wakati ataanguka tuu.

SWALI. Je Ni kwanini Elimu ni Lazima na Kwanini tufundishwe Habari za Jua kusimama na Dunia Kujizungusha na Huku ikilizunguka Jua ikiwa ni Tofauti na Tulionavyo Jua na Tunavyohisi juu ya Kuzunguka kwa Dunia.? Tusingekua na Elimu hiyo Kipi Kingetokea katika Maisha yetu? The celebrity Utatusaidia majibu tafadhari kwa lengo la kuelimishana na sio kushindana.

Uliuliza inawezekana vipi kwa dunia flat jua kuonekana kama linaibuka au kuzama wakati wa mawio na machweo.
Jibu. Kutokana na ukubwa wa Dunia na Udogo wa Jua na kulingana na namna macho ya mwanadamu yalivyo na uwezo wake wakuangalia vitu, ndio maana taswira hiyo huonekana. Kitu chochote kikiwa mbali Kwa macho yetu huwa yanakusanya uona wa juu na chini wa kulia na kushoto katika mstari mnyoofu na kupata taswira ya kitu kikiwa kidogo au kikiwa nusu umbo lake au kuwa katika umbo tofauti na namna tutegemeavyo, mfano Katika barabara iliyonyooka kama kuna gari mbele unaweza kuzania limejaa barabara yote, na ukiweka meza katikati unaweza ukaliona likiwa nusu hata kama lina uwezo wakuipita hiyo meza juu yake bila kuigusa.

hivyo basi jua linapojkua katika safari yake ya kuizunguka dunia, kwa walio mbali nalo kutokana na ukubwa wa dunia wataliona kama kitu kinachoibuka na likiwapita likaenda mbali wataliona kama kitu kinachozama. kama umewahi kuishi katika mikoa yenye utambarare mawio na machweo unaweza kuyaona katika shape hii. so jibu kwa fflat kuliona jua katika umbo nusu ni sababu ya ukomo wa uono wetu tuu. Nathibitisha hilo kwasababu kama utatumia Darubini kuliangalia Jua uliloliona Nusu utaweza kuliona likiwa zima kutegemea na lens ya hio darubini. hapa unaweza kulithibitisha hili wewe mwenyewe ukipenda.

Umeshawahi kujiuliza kwanini mito hairudishi maji nyuma pamoja na umbo la dunia kua kama mpira?
Umeshawahi kujiuliza kama anga letu lina Ziro gravity kwa umbali flani hivyo vimondo huwa vinavutwa duniani na force ipi ikiwa kuna vitu vikiffika anga la mbali vinaipoteza hiyo nguvu na kuelea angani. Hapa utanielewesha kidogo.

tunakataa hakuna Gravity kwasababu haijawahi kuthibitishwa au kuteengenezwa kitu cha mfano wa Gravity FForce inavyofanya kazi kama mifano ya FForce nyingine inavyopatikana kuthibitisha fforce hizo.
kwa mfano kama hiyo gravitation force ina weza kuyabumba maji yasimwagike inashindwaje kuzuia miguu yetu isitembee ikiwa ni miyepesi kuliko density ya maji ya Bahari. hiyo force inalivuta jiwe kubwa kuelekea katikati ya dunia lakini imeshindwa kuyavuta mapulizo?

ndio maana tunaamini kila kinachoizidi hewa uzito kitatafuta base kitue au kutulia. kuhusu kushoto au kulia, wewe mwenyewe ni shahidi hata ukiisahau ndoo tupu chini upepo ukiizidi nguvu ya kushoyo au kulia itasogea na itabaki ardhini labda ikipatikana nguvu ya upepo wa kuinyanyua ndio itaelea. jr density ya hewa na maji ipi kubwa au gravity imechagua vyakuvivuta tuu.?

Unaamini mwanadamu ni kiumbe halisia ambacho hakikuumbwa jechanzo chake ni kipi.? Mtoto Mchanga au Mtu Mzima.? Namaanisha kabla ya Kuanza kuzaliana?

Nasisitiza nipo hapa kuelimika na kuelimisha wengine, Sishindani nipate ushindi wa hoja maana imeandikwa KILA MTU ATAUCHUKUA MZIGO WAKE MWENYEWE. Na TUNAANGAMIA KWAKUKOSA MAARIFA hapa naweza kua mimi au wewe.
 
NkumbiSon umekuja kushangaa tu, umeshindwa kuleta hoja?
Hoja yako niliijibu hivi. ""KUPITIA SAYANSI TUNAONA KWENYE MOVIE BOMU LIKIUA WATU WENGI, JE TUAMINI WALE WATU WANAKUFA KWELI?" ila haukunijibu kwakua ulijua namaanisha sio kwasababu sayansi inafanya kazi basi ni lazima tuiamini, bado tuna nafasi yakutumia akili zetu za kuzaliwa.
 
Asante sana Kwa majibu yako umejaribu kujibu Kila hoja kadri uwezavyo na Kwa uelewa wako🙏. Nimesoma maelezo yako hapo juu nimekuelewa vzr tu lakini umeniacha na maswali mawili.

1. Kama Jua linaenda mbali hadi kufikia ukomo wa kuweza kuliona kwanini halipungui SIZE? Mfano ndege ikiwa angani mbali tunaiona ikiwa na SIZE ndogo sasa kwann Jua lipotee likiwa na ukubwa wake?. Na point ya Jua kuonekana half sijakuelewa hapo vzr.

2. Kwenye maelezo yako umesema Jua linazunguka Dunia na linajizungusha kwenye muhimili wake, Right? Sasa ningependa kujua ni kitu Gani kinachosababisha Jua lizunguke Dunia na lijizungushe kwenye muhimili wake. Na kwann Hilo Jua lisifall down to the ground yaani limeshikiliwa na nini?
 
namba2 itakua umenisoma vibaya au uandishi wangu haukuacha nafasi ya sentesi moja na nyingine. kwakukujibu sasa. kinachofanya Jua liizunguke dunia ni Nguvu iliyopo kati ya North Pole na South Pole ambayo huzalisha usumaku, naomba nikujibu kifupi ili upate kuuliza mengine yatokanayo na majibu nadhani ndio njia nzuri ya kujifunza..

Na swali namba moja.. ukubwa haupungui kwa sababu hatuwezi kuliona katika umbali wa lenyewe kupungua kwakua litakua limeshapita na mwanga wake na kutuachia giza ambalo tunaseema ni usiku na kwa asubuhi tunaanza kuuona mwanga kwanza na distance ya lenyewe kunekana tayari linakua karibu na eneo letu linaloangaza so tutabaki kuliona katiaka ukubwa wake napo ni kutokana na hali ya nchi milima na mabonde.
Na ila kama utakua eneo lenye tambarare ndefu utaliona likiwa dogo kiumbo maana nafasi ya uono itaongezeka.
 
Kuna kitu unachanganya, phenomenon(observable event) na Theory. Gravity ni phenomenon ambayo tunaiobserve in everyday life, mfano ukiruka utarudi chini, ukirusha kitu juu kitarudi chini na mifano mingine mingi inayofanania.

Sasa hiyo observation au effect ikapewa jina la GRAVITY. Kwahy ukisema unakataa gravity maana yake unapinga ukweli kuwa ukiruka haurudi chini, ukirusha kitu juu kitarudi chini.

Kitu ambacho ulipaswa uhoji ni the THEORY behind gravity. Yaani gravity inavyofanya kazi. Newton baada ya kuobserve apple limeanguka na kujiuliza maswali hakuweza kujua the theory behind gravity kwahy yeye akaconclude ni force ya vitu venye uzito. Einstein akaja kutoa mwanga zaidi kuhusu gravity( Einstein theory of general relativity.
Kwahy nikuweke sawa hapo.

Tukija kwenye jibu lako la DENSITY ndo inasababisha vitu vifall nimekuelewa vzr kabisa hujakosea but Kuna kitu kinamiss, kitu Gani? Soma Kwa makini hapa!!👇

Assume umechukua object fulani ukaiweka hewani at some distance from the ground, technically hiyo object lazima itafall si ndio? Of course yes, utasema hiyo object ni more dense than air. Swali la kujiuliza tu kwanini Downward direction ⬇️??
Kumbuka hiyo object kabla haijafall down ilikuwa imezungukwa na Air pande zote(juu, chini, na pembeni) na pande zote hizo Kuna air ambayo ni less dense than hiyo object Sasa swali Bado linabaki ni kitu Gani kinachagua direction ya chini na sio otherwise??
 
kuhusu kwanini Jua lisianguke chini na limeshiliwa na nini? jua limeshikiliwa/limedhibitiwa na nguvu za usumaku. (ni somo lingine kama tutakubali linazunguka kama tulionavyo) na linazunguka kwa namna ya kiuwezo wa Mungu mwenyewe katika dhana nzima ya Uumbaji wa Mungu katika vitu na Viumbe vyake kua katika shape ya No9 au kama Coil. Ndio maana Jua na Mwezi huzunguka katika Shape hiyo, na ndio tunapata majira ya mwaka.
 
kuhusu kwanini Jua lisianguke chini na limeshiliwa na nini? jua limeshikiliwa/limedhibitiwa na nguvu za usumaku. (ni somo lingine kama tutakubali linazunguka kama tulionavyo) na linazunguka kwa namna ya kiuwezo wa Mungu mwenyewe katika dhana nzima ya Uumbaji wa Mungu katika vitu na Viumbe vyake kua katika shape ya No9 au kama Coil. Ndio maana Jua na Mwezi huzunguka katika Shape hiyo, na ndio tunapata majira ya mwaka.
 
jibu unalipata hivi, kila unapozidi kwenda juu Hewa inakua na nguvu kuliko chini, na kitu kitakachokua kizito kuliko hewa ya chini kitashuka chini maana ndiko palipo na hewa iliyo dhaifu kwa uzito huo. na ndio maana unaweza ukachora duara chini na ukishika jiwe mkononi ukiliachia linatua katika duara uilolichora ila ukiwa gorofani ni ngumu jiwe hilo kutua katia hilo duara hata kama upo katika usawa uleule.
hapo ni kwakua utakua juu na hewa ya huko ina nguvu kuliko ya umbali wa mkono wako so jiwe litapata changamoto ya hewa za pande zote isipokua ya chini. hapa nimewaza kwa akili zangu tuu. utanifundisha ikibidi, kinachosababisha usilenge duara ni nini na upo katika usawa ule ule?
 
tunapinga gavity si term tuu ya kitendo cha vitu kudondoka chini ila kubwa ni kuzuia maji ya bahari maana tunaamini maji hutafuta base yake yenyewe na si sababu ya kuvutwa na force.

hapa mi labda nikuelewa kua kitu kuanguka chini kisayansi inatwa gravity na sio kwamba kimevutwa kalazimishwa kuja chini na nguvu yenye jina hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…