katika uzi huu nimejaribu kutumia lugha rahisi na mifano rahisi kuweza kuelewa kwanini naamini tumedanganywa kuwa dunia ni tufe.
kuna mdau kasema nimekimbia, kwa mwandiko huu atajikosoa kauli yake, ni hivi mimi sibishani na sishindani kuwa nani ni mkweli au nani muongo. hapa hoja ni KWAKUTUMIA AKILI ZAKO NA MILANGO YAKO YA FAHAMU Je Unajiona upo katika umbo gani la dunia, je Jua linaonekana likimove au limesimama? je unahisi Dunia inazunguka au imetulia?
Ukija kwakujiandaa kushindani Shinda wewe, ukija kwa nia ya kubishana mimi siwezi, ndio maana kwa sasa sintoreply post ya kutaka tubishane zaidi ya zile za kutaka tuelimishane.
Kwa post hii nitajaribu kuzijibu hoja zilizopo kwa njia rahisi tuu ili tuelimishane.
Ni hivi, dunia ni Kubwa sana kubwa haswa, hapo wote tunakubaliana juu ya ukubwa huo. halafu ni Duara, hapa tuelewane hakuna sehemu FlatEarth tumepinga kua dunia ni Duara so hoja za wanaolikataa umbo hilo zisijikite katika Uduara wa umbo la dunia na hata U flat wake tusiulinganishe na sakau au Tiles. bali ni eneo kubwa sana lenye hali ya utambarare huku milima mito na mabonde vikiwa ndani ya eneo hilo lililozungukwa na maji ya Bahari yanayokingwa na Kingo za Barafu kuizunguka duara la Dunia hiyo.
Hoja ni Tufe na Sahani. kwenye riadha kuna michezo ya kurusha Tufe na Kurusha Sahani so tudeal na shape za vitu hivyo kuwakilisha shape za Dunia tuliyoisoma Darasani na shape ya Dunia isiyofundishwa Darasani. Niliwajibu waliouliza kwanini naamini tunadanganywa namna tunavyofundishwa shape ya dunia kua kama tufe. niliwajibu kwa kifupi kua huo ni Mchongo wa shetani kupitia Elimu kuwalaghai wanadamu wamwabudu yeye na wasiuamini uwepo wa Mungu anaestahili kuabudiwa yeye peke yake.
kuna hoja ya kwanini naipinga Sayansi lakini natumia vitu vitokanavyo na sayansi ambayo ni shetani.
Jibu ni hivi, huu ni mpango System inayotaka kila Mwanadamu amuamini shetani kwa kumwabudu yeye kama ndio Mungu mwenye uweza wa vyote. So ni jukumu la sisi wanadamu kutambua mitego ya Ibilisi na kuiruka kwasababu hana alichokibuni hapa chini ya jua zaidi ya kudanganya, uongo ndio silaha kubwa ya shetani.
so hata hizi device tunazotumia ni moja ya njia ya Ulaghai wa shetani kwa wale wasiomcha Mungu watamuamini yeye na bila yeye hakuna litakalofanyika so unakua umenasa moja kwa moja kwake. SWALI kwa aliyehoji hilo, Je Bila kitu gani kilichotokana na Sayansi na kipo kwa matumizi ya sisi wanadamu, pindi kikikosekana Uhai utakua Basi? Namaanisha kipi ukifanyacho kwa simu au Computer hakiwezi kufanyika bila hivyo vitu? je mwanadamu kazidiwa uwezo wa kiakili na hizi device?
Jibu langu Sasa, Natumia hivi vitu vya kishetani kwasababu natambua namna ya kuukwepa ulaghai wake na Nikabaki namwabudu Mungu kwakua ni Muweza wa vyote na Shetani hajaweza kufanya kitu kinachomzidi uwezo Mwanadamu, bado hajafanikiwa nandio maana kila kilichotokana na Sayansi (Shetani) Kinamhitaji Mwanadamu Kukiendesha. na yule ashindwae kukiendesha na kikawa kinamuendesha basi anakua kanasa katika lengo la shetani kuabudiwa.
Turudi kwenye maswali na majibu sasa.
narudia. Jua ni Dogo kuliko Dunia na ndilo linaloizunguka dunia iliyotulia bila kulizunguka jua au kuzunguka yenyewe kwenye mhimili wake. Nathibitisha hili kwakuliangalia Jua kwa macho yangu nakuliona likiwa linasogea kutoka point moja kwenda nyingine. Nathibitisha Dunia haizunguki kwasababu sijawahi kuhisi hivyo kua nipo katika likitu linalozunguka. Naamini tumedanganywa hayo kwasababu TUMEFUNDISHWA DARASANI... ukweli wa hii hoja yangu ni majibu ya Mtu au Mtoto ambaye hajawahi kufundishwa kabisa, ukimuuliza atakwambia Jua linasogea/kutembea na Dunia imetulia na hawezi kuamini yupo katika Tufe linalozunguka kwa maana anaamini kuna wakati ataanguka tuu.
SWALI. Je Ni kwanini Elimu ni Lazima na Kwanini tufundishwe Habari za Jua kusimama na Dunia Kujizungusha na Huku ikilizunguka Jua ikiwa ni Tofauti na Tulionavyo Jua na Tunavyohisi juu ya Kuzunguka kwa Dunia.? Tusingekua na Elimu hiyo Kipi Kingetokea katika Maisha yetu?
The celebrity Utatusaidia majibu tafadhari kwa lengo la kuelimishana na sio kushindana.
Uliuliza inawezekana vipi kwa dunia flat jua kuonekana kama linaibuka au kuzama wakati wa mawio na machweo.
Jibu. Kutokana na ukubwa wa Dunia na Udogo wa Jua na kulingana na namna macho ya mwanadamu yalivyo na uwezo wake wakuangalia vitu, ndio maana taswira hiyo huonekana. Kitu chochote kikiwa mbali Kwa macho yetu huwa yanakusanya uona wa juu na chini wa kulia na kushoto katika mstari mnyoofu na kupata taswira ya kitu kikiwa kidogo au kikiwa nusu umbo lake au kuwa katika umbo tofauti na namna tutegemeavyo, mfano Katika barabara iliyonyooka kama kuna gari mbele unaweza kuzania limejaa barabara yote, na ukiweka meza katikati unaweza ukaliona likiwa nusu hata kama lina uwezo wakuipita hiyo meza juu yake bila kuigusa.
hivyo basi jua linapojkua katika safari yake ya kuizunguka dunia, kwa walio mbali nalo kutokana na ukubwa wa dunia wataliona kama kitu kinachoibuka na likiwapita likaenda mbali wataliona kama kitu kinachozama. kama umewahi kuishi katika mikoa yenye utambarare mawio na machweo unaweza kuyaona katika shape hii. so jibu kwa fflat kuliona jua katika umbo nusu ni sababu ya ukomo wa uono wetu tuu. Nathibitisha hilo kwasababu kama utatumia Darubini kuliangalia Jua uliloliona Nusu utaweza kuliona likiwa zima kutegemea na lens ya hio darubini. hapa unaweza kulithibitisha hili wewe mwenyewe ukipenda.
Umeshawahi kujiuliza kwanini mito hairudishi maji nyuma pamoja na umbo la dunia kua kama mpira?
Umeshawahi kujiuliza kama anga letu lina Ziro gravity kwa umbali flani hivyo vimondo huwa vinavutwa duniani na force ipi ikiwa kuna vitu vikiffika anga la mbali vinaipoteza hiyo nguvu na kuelea angani. Hapa utanielewesha kidogo.
tunakataa hakuna Gravity kwasababu haijawahi kuthibitishwa au kuteengenezwa kitu cha mfano wa Gravity FForce inavyofanya kazi kama mifano ya FForce nyingine inavyopatikana kuthibitisha fforce hizo.
kwa mfano kama hiyo gravitation force ina weza kuyabumba maji yasimwagike inashindwaje kuzuia miguu yetu isitembee ikiwa ni miyepesi kuliko density ya maji ya Bahari. hiyo force inalivuta jiwe kubwa kuelekea katikati ya dunia lakini imeshindwa kuyavuta mapulizo?
ndio maana tunaamini kila kinachoizidi hewa uzito kitatafuta base kitue au kutulia. kuhusu kushoto au kulia, wewe mwenyewe ni shahidi hata ukiisahau ndoo tupu chini upepo ukiizidi nguvu ya kushoyo au kulia itasogea na itabaki ardhini labda ikipatikana nguvu ya upepo wa kuinyanyua ndio itaelea. jr density ya hewa na maji ipi kubwa au gravity imechagua vyakuvivuta tuu.?
Unaamini mwanadamu ni kiumbe halisia ambacho hakikuumbwa jechanzo chake ni kipi.? Mtoto Mchanga au Mtu Mzima.? Namaanisha kabla ya Kuanza kuzaliana?
Nasisitiza nipo hapa kuelimika na kuelimisha wengine, Sishindani nipate ushindi wa hoja maana imeandikwa KILA MTU ATAUCHUKUA MZIGO WAKE MWENYEWE. Na TUNAANGAMIA KWAKUKOSA MAARIFA hapa naweza kua mimi au wewe.