Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Hii ni military base ya Chile iliyopo AntarcticaView attachment 2915830
There are no official military bases in Antarctica, regardless of the country. The Antarctic Treaty, signed in 1961, prohibits the establishment of military bases and the use of military force on the continent. This treaty focuses on peaceful scientific research and cooperation among signatory nations.
 
"Hakuna kambi rasmi"


Basi inabidi utambue kuanzia sasa kule kuna kambi za kutosha, Iwe sio rasmi ila kambi zipo.
 
"Hakuna kambi rasmi"


Basi inabidi utambue kuanzia sasa kule kuna kambi za kutosha, Iwe sio rasmi ila kambi zipo.
Na inabidi uelewe zile kambi zipo kwajili ya tafiti tu na sio lengo lingine.

Rejea maelezo yako na usome kwa makini na utulivu wa hali ya juu uelewe kilichomaanishwa kwenye mkataba.
 
"Hakuna kambi rasmi"


Basi inabidi utambue kuanzia sasa kule kuna kambi za kutosha, Iwe sio rasmi ila kambi zipo.
Yes upo sahihi......even though hata huko Antarctica pia hakuna curvature of the earth it's a flat plane all over!
 
Yes upo sahihi......even though hata huko Antarctica pia hakuna curvature of the earth it's a flat plane all over!
Tusubiri Elon amalize project zake.

Tutawachangia Flat Earther muende mkatalii kwenye space muione Dunia jinsi ilivyo.

Ila mkirudi huku mnalipa hela tulizowachangia na faini juu.
 
Tusubiri Elon amalize project zake.

Tutawachangia Flat Earther muende mkatalii kwenye space muione Dunia jinsi ilivyo.

Ila mkirudi huku mnalipa hela tulizowachangia na faini juu.
Wewe kwanini umeamini kabla hata ya Elon kumaliza project zake?!

Si ulipaswa usubiri akamilishe project zake ili akuletee uthibitisho usio na shaka kuhusu Tufe linalozunguka?

NB:- Inashangaza sana kuona huamini kwenye researches ambazo unaweza ukazifanya wewe mwenyewe,.sio mpaka umtegemee Musk
 
Lakini pia fikiria kama usingeambiwa Dunia ni Tufe tokea unaanza kupata akili,...Je wazo kwamba Dunia ni Tufe linalozunguka lingekujia kwenye akili yako?! Chosen Rich
 
Mimi nlishafanya research zangu binafsi muda sana, Kwa akili zangu timamu na uelewa wangu mpana ukiongozwa na fikra mathubuti nlihitimisha pasipo shaka kuwa dunia ni tufe.

Hizi project za Elon musk kwa sisi tunaotambua Dunia ni tufe itakua ni utalii tu, Ila kwa nyinyi watu wa flat itakua ni kujifunza.
 
Lakini pia fikiria kama usingeambiwa Dunia ni Tufe tokea unaanza kupata akili,...Je wazo kwamba Dunia ni Tufe linalozunguka lingekujia kwenye akili yako?! Chosen Rich
Moja kati ya maswali yalikua yanasumbua kichwa changu tangu utoto, ni kuwa mwisho wa Dunia ni wapi ?

Maswali mengine nlikua najiuliza kama kuna binadamu wengine huko juu, hii baada ya kuwa nlikua naona nyota usiku.

Haya na mengine mengi nlikua najiuliza wakati wa utoto wangu kwahiyo sikuwa na jibu kuhusu shape la Dunia.
 
Sasa kama ulifanya research zako binafsi kwanini unaamini kwenye picha za mchongo kama hizi 👉🏼🌍.....

Sidhani kama ukitumia research yako mwenyewe unaweza ukaja na hitimisho kwamba Dunia ni Tufe la namna hii 👉🏼🌍....labda utuambie ulitumia njia gani kwenye research yako mpaka kupata hitimisho hilo.
 
Anhaa vizuri,.. kwahiyo utotoni hukufikiria kabisa kama Dunia ni Tufe?

Ulijiuliza Tu kuhusu mwisho wake, si ndiyo?
 
Anhaa vizuri,.. kwahiyo utotoni hukufikiria kabisa kama Dunia ni Tufe?

Ulijiuliza Tu kuhusu mwisho wake, si ndiyo?
Nlijiuliza kuhusu mwisho wake, maswali yangu yalijibika kwenye Dunia tufe,

Dunia ni tufe.
 
1.Kwenye suala la ramani ya U.N,,wakati wanafanya chaguzi ya ramani,walitaka ambayo ingeweza kuionesha mabara na visiwa vyote ambavyo binadamu wanakaa.

Uduara wa dunia, unafanya ngumu kuichora kwenye karatasi, mfano;ukipewa chungwa/chenza (chungwa ni duara) umenye ,yale maganda yake ukiweka kwenye meza hayawezi yakawa flat,ukilazimisha yatameguka au kukatika, ndiyo hata kwenye dunia kuna mitindo tofauti ya kuiwasilisha kwenye flat surface/karatasi japo kimahesabu nayo haipo sawa mana kuna nchi uonekana kubwa kuliko au ndogo kuliko.

Tukirudi kwenye bendera ya UN,wamechukua mtindo wa Azimuthal equidistant, ambapo North Pole ndiyo kama kitovu, na vipimo vya umbali kutokea hapo kwenda point yoyote vinalingana ila kama wangechukua Mercantile Projection,kuna nchi zisingeonekana.

2.Tukienda kwenye suala la mwendokasi wa Dunia. Katika sheria tatu za Mwendo za Isaac Newton.sheria ya kwanza inasemaan" object will not change its motion unless a force acts on it."yaani "kiumbe hakitobadili mwendokasi wake mpaka kani ya nguvu iingilie "
Mfano:kabla haujapanda lift unakuwa kwenye mwendokasi wako, ili ukiingia na kupanda,lift ikianza kwenda juu au kushuka ghafla unahisi mwili kutaka kuruka au kudidimia, hii ni kwasababu mwendokasi wa Lift ndiyo force inayoingilia mwendokasi wako.
Sasa hauwezi kuhisi huo mwendokasi wa dunia kwasababu umezaliwa Dubai,yaani tangia upo tumboni kama yai tayari uli-adopt mwendokasi wake kama wako.
Wale Astronauts wanaotoka na kuingia dunia ,vyombo vyao kutumia nguvu nyingi ili niweze kutoka au kuingia katika mwendokasi wa dunia.

3.Hapo kwenye kusema Dunia ina eneo la maili 3965,ambazo ni sawa na Km 6381 sasa hapo mbona kimahesabu ni uongo. Kwa maana nchi yetu tu ina zaidi ya huo ukubwa.
Kwa tuliosoma sayansi tunabatilisha mahesabu ya chini yote yaliyofuata

4.Suala la mwanga:
Kama dunia ni tambarare basi hata mwanga wa jua ungemulika kote sawa. Chukua tochi mulika daftari kwenye chumba giza, Utaliona daftari zima,,,aya sasa chukua tochi mulika chungwa kuna upande wa chungwa utakuwa na giza.

Kama dunia haijizungushi na tambarare basi jua linavyochomoza asubuhi kutoka magharibi na kwenda mashariki si lingeenda mona kwa moja ama ? Na ulisema
Jua ndiyo lazunguka basi by the time Jua katika upande wa pili wa kipenzi cha dunia basi baridi lingetuuwa wote.
Na jua linalozunguka dunia inawezaje kuhakikisha kwa masaa 24 kuna upande wa dunia unapata mwanga.

5.Mawingu, always yanaenda upande mmoja,kama dunia tambarare basi inamaana yakifika ukingo wa dunia yanapotea kule.

6.Hesabu ya mwaka: Hivi unajua kuwa hesabu ya siku 365.25 hutokana na mzunguko wa dunia na solar system na katika tenge lake.
Aya,dunia ni tambarare ,hiyo hesabu ya miaka yako uliyonayo, itakuwa imezingatia mahesabu gani.

7. NASA :ushahidi wako mwingi umejikita kwenye kuwasema NASA ni waongo, kwahyo hata Warusi wanshirikiana na NASA,hata Wairan na Wakorea (hawa wote wana satellite angani) wanashorikiana na NASA kwenye uongo.

8.ANTARTICA:Nenda usome wataka wa U.N why wachache wanenda kule.
Kwanza like ndiyo jangwa kubwa dunia kwa mana linaweza kukaa hata miaka mi5 vila mvua. Barafu zina unene mpaka wa km2 ndiyo unagusa ardhi.

9.Toa hoja za kisayansi na kutumia vitabu vya dini na hisia kama sehemu za kujitetea
 
Hata kama sijasoma, hata kama nimelogwa. Kukubali dunia ni tambalale kama Mkeka huo ni Uendawazimu. Labda nikiambiwa nibishe nipate chochote kitu nitasupport mada tena kwa point nzito nzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…