Wazee wa Spinning Ball nina swali hapa. Kama Dunia ni globe maji ya mto nile yanawezaje kupanda mlima kwenda Egypt?? Toka lini maji yakapanda mlima?? Naombeni majibu hapa.
Soma hii halafu ingia Facebook kam follow jamaa anaitwa Cekam cekams
Huu ni walaka nilioandika kwenye comment kufuatia post ya ndugu Comred Mbwana Camerôò Allyamtu alipouliza kuhusu mseleleko wa maji ya mto Nile kuelekea Kaskazini alikopaita "Juu"
Nilianza kwa kusema....
Bro, Kaskazini sio Juu.!
Kaskazini ni moja ya pande nne za Dunia zilizobuniwa kwa ajili ya kuonesha uelekeo, Mashariki ni upande kunakochomoza Jua asubuhi, Magharibi ni upande unaozama Jua jioni.
Ukiweka upande wa Mashariki mkono wa kulia wako, Magharibi itakuwa kushoto, Kaskazini itakuwa mbele na kusini itakuwa nyuma, maana yake Kaskazini imeelekea (Anticlockwise) 90° kwenye "First Quadrant" ya nyuzi, Kusini ikiwa 270° (Anticlockwise) kutokea Mashariki kwenye "Third Quadrant"
Hizi ni pande za kuonesha uelekeo sio kuonesha muinuko, juu wala chini.
Unaweza kuwa unaelekea kasikazini lakini unaingia bondeni, na ukawa unaelekea Kusini huku ukipanda mlima.
"Juu" tunayoitaja ni kile kiwango cha urefu kutoka kwenye kiini cha Dunia, ardhi hii tunayokanyaga ipo karibu kilomita 6400 kutoka kwenye (kokwa) kiini cha Dunia, kilomita zinavyozidi kuongezeka tunasema unaenda Juu.
Hivyo ndege uko Juu kuliko mtu aliye kileleni mwa mlima Kilimanjaro, na kilele cha mlima Kilimanjaro kipo juu ukilinganisha na mtu aliye kwenye usawa wa bahari ya Mediterranea, na usawa wa bahari upo juu ya mashimo kwenye machimbo ya madini, kama atatokea mtu kushuka chini kabisa tutasema yuko chini (Ardhini)
Hivyo kaskazini kule kwenye usawa wa bahari ya Mediterranea kupo "Chini" ukilinganaisha na Safu za milima ya ukanda wa Ikweta, na hii picha yako ndiyo inakufunga kabisa ikidhibitisha dunia kuwa Duara.
Kwa sababu kama Dunia isingekuwa Duara, basi maji yote yangemwagika Kusini kwa namna unavyosema, au kama yote yanaelekea Kasikazini (kulingana na picha yako) tusingetegemea Kusini kuwe kuna Maji.
Ila kwa kuwa Dunia ni Duara, basi gravity imekuwa distributed kila point ya Sphere kuvuta vitu "Chini"
Chini namaanisha kule kwenyemkiini cha Dunia, katikati ya ule "mpira".
Kwa namna mpira ulivyo, ukiukata katika nusu mbili kunakuwa na kipenyo (Diameter) kubwa kuliko ukichana slice ndogo kule Kasikazini.
Hivyo kwenye ukanda wa Ikweta Dunia, kama mpira, **** mnofu mkubwa wa kuunda kipenyo kikubwa, na unavyozidi kwenda Kaskazini au Kusini ule mduara wa Slice unapungua, assume kama unakata mkate wenye umbo la mpira.
Kule unakokuita juu (kaskazini) utaona umbali wake kuelekea kwenye kitovu unapungua, hii inasababisha kwenye eneo la katikati kuwe "juu" wakati kule kwenye ncha kuwe "chini"
Ukiangalia katika tafiti za kisayansi za umbo la dunia, inaonekana urefu wa kutoka kwenye kiini hadi kwenye Ikweta ni kitu kama kilomita 6400 wakati kutoka kwenye kiini kuelekea pole yoyote iwe South au North urefu ule unapungua, kitu kama 6250Km.
Hii inafanya kwenye ukanda wa Ikweta kuwa Juu na kwenye ncha za Kusini na Kasikazini kuwe Chini.
"Chini" ukiwa umesimama ni ile point iliyo chini ya miguu yako, kuelekea ardhini au tuseme kuzimu, kwenye kiini cha Dunia, "Juu" ni ile point ya juu ya kichwa chako kuelekea Angani.
Yes, Ni gravity inayovuta hayo Maji kutoka Victoria kwenda Mediterranea, surprisingly nenda angalia mto Mississippi wa Marekani.! Ili kuchanya zaidi angalia mto Themes wa Uingereza.
Gravity ni kani ya uvutano yenye asili yake kwenye kiini cha Dunia (tutaiongelea kimapana siku nyingine) Kani hii huvuta vitu vyote kwenye kiini cha Dunia, kule Chini.!
Kwa hiyo sehemu yeyote iloyoinuka Juu kidogo ya usawa wa bahari (6400km) basi chini yake ni ile point kuelekea ardhini.
Mediterranean Sea iko chini kuelekea center ya Dunia ukilinganisha na Victoria Highlands zilizo kwenye ukanda wa Ikweta.
Gravity ikianza kuvuta Maji, naturally tu maji yatatafuta mseleleko uko wapi kufuata point ya Chini kuelekea kwenye kiini cha gravity, hii haijalishi kama chini ni Kasikazini au Mashariki.
*****
Niongezee kitu... Dunia ni Duara.!
Vipo vithibitisho vingine vingi kuwa dunia ni Duara kinachoharibu ni watu wanaosema Dunia sio Duara hawana vidhibitisho, wao wanajitahidi kukanusha vithibitisho vinayosema Dunia ni Duara.
Tunataka vithibitisho vya kuwa Dunia ni Bapa (flat) na isewe kusema Dunia sio Duara.
Maana kama Dunia sio Duara (mpira/ Sphere) basi kuna umbo lingine wanalotaja inaweza kuwa pembenne, mche mraba, mche pembetatu, Bapa au vyovyote.
Wao wanasema Bapa, wengine bapa kwa mfumo wa Saani, wengine wanasema ni bapa kwa mfumo wa mcheduara. Sasa tunataka vithibitisho vya Dunia kuwa Bapa.
Sio kuja na namna ya kukanusha.!
Kwa kutumia mseleleko wa maji na mpangilio wa vyanzo vya maji vikubwa Duniani kama bahari Dunia inaonekana kuwa Duara, maana kama ingekuwa Flat basi kuna sehemu tungepata ukingo ulioshikilia maji.
Lakini kwa kuwa Dunia ni Duara, na Kani ya gravity inashikilia kila kitu kuelekea katikati basi maji yote yanavutwa kwenye kiini yasimwagike,
Maji hutoka sehemu iliyoinuka mfano nyanda za Maziwa makuu ya miinuko ya Ikweta na kuvutwa Chini kwenye usawa wa bahari ulio bondeni, usawa wa Bahari haijalishi uko Kasikazini, kusini au Mashariki.
Maji yanafata mseleleko wa gravity.!
Cekam Cekam's