The celebrity
JF-Expert Member
- Jul 9, 2020
- 1,972
- 559
Angalia Kwa umakini huu mchoro hapa chini👇👇Naomba nijibu hizi hoja zako hapa,....
1. Hoja yangu kuhusu umbo la Dunia ni kwamba,..Dunia haina umbo la tufe la namna hii ➡️🌍,..Bali DUNIA Ina umbo lenye flat-surface umbo ambalo linaweza kuwa round kama SAHANI, round kama YAI au vyovyote vile lakini ni flattened.,
2. Majibu yako juu ya ishu ya Alaska,..umecopy sehemu lakini Yana contradict theories za Dunia tufe,. nasema hivyo Kwasababu......Kwa mujibu wa nadharia za Dunia Tufe ni kwamba Dunia inatumia saa 24 kukamilisha mzunguko wake mmoja(kulizunguka Jua)....
Hapo tunapata majibu mawili kwamba maelezo uliyocopy jamaa wameshindwa kutatua hiyo puzzle Kwa kuwa:-
-Kinadharia ya Dunia Tufe,....kila mzunguko mmoja wa Dunia ukikamilika "NDIYO TUNAPATA USIKU/MCHANA,. Hivyo hakuna namna tutapata situation ya Alaska kwenye nadharia ya dunia Tufe linalozunguka Jua kila siku Kwa saa24..
Jiulize mwenyewe Dunia inakamilisha kulizunguka Jua Kila baada ya saa 24,. Je kwa huo mzunguko wa Dunia inawezekana vipi Alaska na maeneo mengine yana experience midnight sun Kwa zaidi ya mwezi mmoja, wakati kila siku Dunia inakamilisha mzunguko wake?
NB:- Kumbuka Jua, kwenye nadharia ya dunia Tufe lipo static halifanyi movement yoyote.
Sasa unaposema kuna kipindi katika mwaka Jua linakua Juu ya upeo wa macho kila mara huoni una contradict nadharia ya kwamba Jua hali move? Yani Kwa mantiki hiyo ili uthibitishe madai yako ilipaswa eneo hilo la Alaska lishuhudie Jua likiwaka mwaka mzima(Usiku na Mchana )kwenye eneo Lao Kwa kuwa Jua lipo fixed kwenye upeo wao wa macho kwenye eneo hilo....
3. Kuhusu gravity,.ngoja nikuulize swali...unahisi kitu chochote kikirushwa juu kinarudi chini Kwasababu gravity inarudisha kila kitu kwenye center ya Dunia?.....Mimi nasema hivi "ukirusha kitu kwa nguvu ya kutosha hakuna force yoyote itakayofanya kitu hicho kirudi chini....kitu kinarudi chini kwa kuwa nguvu iliyotumika ni ndogo kukifanya kitu hicho kiendelee muelekeo uliokusudiwa hivyo kinadondoka chini."
Note: mchoro upo katika top view:
Sasa twende taraibu,
Hapo kwenye mchoro Kuna Jua(kama nilivyoonesha) na Kuna Dunia.
Ukitazama Kwa umakini utaona Kuna mizunguko miwili, 1) ni revolution( ambayo kwenye mchoro nimeandika rotation kimakosa) yaani Dunia kuzunguka Dunia Kwa siku 365 na 2) rotation ambayo ni spinning Dunia kujizungusha kwenye muhimili wake.
Zingatia zaidi kwenye Dunia, Kuna points nimeziweka ambazo ni A,B,C,D na O. Zaidi zingatia point O as Dunia ina-spin kupata usiku na mchana almost point hiyo point O Bado utapata mwanga japo ni partial, sijui unapata picha ya Dunia nilivyoichora hapo? Nimekwambia hiyo ni top view ya Dunia tufe. Zaidi angalia hapa 👇👇
Najua utapata maswali kwanini kusiwe na midnight sun the whole year maeneo hayo? Majibu ya hiyo kasome zaidi na earth tilting.
Sijui umeipata concept yangu?
Sasa, naimani utakuwa umepata mwanga kidogo lakini kasome zaidi naimani utaelewa tu. Naomba naww ulete maelezo ya Alaska kwenye Dunia tambarare.