hateeb10
JF-Expert Member
- Dec 8, 2022
- 2,920
- 1,223
Kama Dunia ni Tufe,...1.Kwenye suala la ramani ya U.N,,wakati wanafanya chaguzi ya ramani,walitaka ambayo ingeweza kuionesha mabara na visiwa vyote ambavyo binadamu wanakaa.
Uduara wa dunia, unafanya ngumu kuichora kwenye karatasi, mfano;ukipewa chungwa/chenza (chungwa ni duara) umenye ,yale maganda yake ukiweka kwenye meza hayawezi yakawa flat,ukilazimisha yatameguka au kukatika, ndiyo hata kwenye dunia kuna mitindo tofauti ya kuiwasilisha kwenye flat surface/karatasi japo kimahesabu nayo haipo sawa mana kuna nchi uonekana kubwa kuliko au ndogo kuliko.
Tukirudi kwenye bendera ya UN,wamechukua mtindo wa Azimuthal equidistant, ambapo North Pole ndiyo kama kitovu, na vipimo vya umbali kutokea hapo kwenda point yoyote vinalingana ila kama wangechukua Mercantile Projection,kuna nchi zisingeonekana.
2.Tukienda kwenye suala la mwendokasi wa Dunia. Katika sheria tatu za Mwendo za Isaac Newton.sheria ya kwanza inasemaan" object will not change its motion unless a force acts on it."yaani "kiumbe hakitobadili mwendokasi wake mpaka kani ya nguvu iingilie "
Mfano:kabla haujapanda lift unakuwa kwenye mwendokasi wako, ili ukiingia na kupanda,lift ikianza kwenda juu au kushuka ghafla unahisi mwili kutaka kuruka au kudidimia, hii ni kwasababu mwendokasi wa Lift ndiyo force inayoingilia mwendokasi wako.
Sasa hauwezi kuhisi huo mwendokasi wa dunia kwasababu umezaliwa Dubai,yaani tangia upo tumboni kama yai tayari uli-adopt mwendokasi wake kama wako.
Wale Astronauts wanaotoka na kuingia dunia ,vyombo vyao kutumia nguvu nyingi ili niweze kutoka au kuingia katika mwendokasi wa dunia.
3.Hapo kwenye kusema Dunia ina eneo la maili 3965,ambazo ni sawa na Km 6381 sasa hapo mbona kimahesabu ni uongo. Kwa maana nchi yetu tu ina zaidi ya huo ukubwa.
Kwa tuliosoma sayansi tunabatilisha mahesabu ya chini yote yaliyofuata
4.Suala la mwanga:
Kama dunia ni tambarare basi hata mwanga wa jua ungemulika kote sawa. Chukua tochi mulika daftari kwenye chumba giza, Utaliona daftari zima,,,aya sasa chukua tochi mulika chungwa kuna upande wa chungwa utakuwa na giza.
Kama dunia haijizungushi na tambarare basi jua linavyochomoza asubuhi kutoka magharibi na kwenda mashariki si lingeenda mona kwa moja ama ? Na ulisema
Jua ndiyo lazunguka basi by the time Jua katika upande wa pili wa kipenzi cha dunia basi baridi lingetuuwa wote.
Na jua linalozunguka dunia inawezaje kuhakikisha kwa masaa 24 kuna upande wa dunia unapata mwanga.
5.Mawingu, always yanaenda upande mmoja,kama dunia tambarare basi inamaana yakifika ukingo wa dunia yanapotea kule.
6.Hesabu ya mwaka: Hivi unajua kuwa hesabu ya siku 365.25 hutokana na mzunguko wa dunia na solar system na katika tenge lake.
Aya,dunia ni tambarare ,hiyo hesabu ya miaka yako uliyonayo, itakuwa imezingatia mahesabu gani.
7. NASA :ushahidi wako mwingi umejikita kwenye kuwasema NASA ni waongo, kwahyo hata Warusi wanshirikiana na NASA,hata Wairan na Wakorea (hawa wote wana satellite angani) wanashorikiana na NASA kwenye uongo.
8.ANTARTICA:Nenda usome wataka wa U.N why wachache wanenda kule.
Kwanza like ndiyo jangwa kubwa dunia kwa mana linaweza kukaa hata miaka mi5 vila mvua. Barafu zina unene mpaka wa km2 ndiyo unagusa ardhi.
9.Toa hoja za kisayansi na kutumia vitabu vya dini na hisia kama sehemu za kujitetea
1. Kwanini kitendo cha maji kustick kwenye round-ball Kisiwe included kwenye Seven wonders of the world?
2. Kwanini kitendo cha maji kustick kwenye round-ball upside down kisiwe kama kivutio cha utalii ambapo watu wanaenda na kufanya observation Kwa kulipia?
Karibu greater than tuchangamshe akili na kujichunguza kama Sisi ni wajinga juu ya umbo la Dunia ama la.