Siri madereva kugomea sheria ya kukatwa alama yajulikana

Siri madereva kugomea sheria ya kukatwa alama yajulikana

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Siku mbili zimekatika tangu nchi itikisike kwa sababu ya mgomo wa madereva wa mabasi katika mikoa mbalimbali nchini wakipinga kukatwa alama kwenye leseni zao wanapofanya makosa ya barabarani, sasa siri ya uwepo wa mgomo huo imebainika.

Kwa mujibu wa dereva mmoja wa kampuni moja ya mabasi yafanyayo safari zake Dar kwenda mikoani (jina lipo), hawatakuja kukubaliana na mpango wa serikali wa kuwakata pointi kwa makosa ya barabarani huku ikijulikana wazi kuwa, barabara za mikoani hazina ubora wa kupitisha mabasi kwa usalama.
Dereva huyo aliongeza kusema kuwa, sipo sehemu nyingi barabara ni nyembamba, hivyo madereva wanaondesha katika mazingira hatarishi sana ili kuzuia ajali ambazo, zikitokea ndiyo serikali ilisema itakata alama madereva.

"Barabara nyingi ni nyembamba sana. Tena pia zina mabonde mabonde. Sasa eti sehemu kama hii ikitokea ajali unakatwa pointi.

"Mfano mzuri, kama unakwenda Tanga kutokea Dar, kuna sehemu barabara ni nyembamba mno. Halafu ina viraka viraka. Maeneo kama hayo, uwezekano wa kutokea ajali ni mkubwa. Basi tu, sisi madereva tunajitahidi sana.

"Mimi ushauri wangu kwa serikali, ianze kwanza kuboresha barabara zetu ndipo watuwekee sheria yao hiyo ya kukata alama. Lakini siyo sasa," alisema dereva huyo ambaye siku ya mgomo anasema alirudi nyumbani kulala huku akiwa amezima simu asipatikane na bosi wake.

Habari zaidi kutoka kwa madereva wengine, zinadai kuwa, askari wa usalama barabarani wamekuwa 'wakiwatafutia' sababu za kuwatia hatiani kwa makosa ambayo yanaweza kuzungumzwa, kutolewa maelekezo au elimu na ndiyo maana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi alisema utaratibu wa kukata pointi haujaanza kutumika.

"Sasa kama waziri mwenye dhamana kasema utaratibu huo haujaanza kutumika. Kwa nini askari wa usalama barabarani walianza kuutumia? Wao waliagizwa na nani?" Alihoji Kinyamkimya, mfanyakazi wa basi moja linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza.

Aliongeza kuwa, kwa tabia ya baadhi ya askari wa usalama barabarani wanaokutana nao kila siku ya Mungu, wao madereva wanaamini kuwa, kutoka Dar hadi Mwanza, ponti zao zinaweza kukatwa zote kwa makosa ya kuwabambikia.

Mgomo huo uliathiri shughuli za usafiri katika vituo mbalimbali vya mabasi, ikiwemo Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (mkoani Dar es Salaam), Msamvu (mkoani Morogoro) na Nane Nane (mkoani Dodoma).
Maeneo mengine yaliyotajwa kufanyika kwa mgomo huo ni Mbeya, Arusha na Kilimanjaro.

Katika Kituo cha Mabasi cha Msamvu, baadhi ya mabasi yaliyotakiwa kuanza safari saa 12:00 asubuhi ya siku ya mgomo, yaligoma kupakia abiria, hivyo, baadhi ya abiria wakirejea majumbani.
Mabasi yaliyoonekana kuendelea kuondoka kituoni ni yale yaliyokuwa yamewasili kutoka safari za masafa marefu na yaliyokuwa yakimalizia safari zao Msamvu.

Baadhi ya madereva hao wamesema kuwa, chanzo kikuu cha mgomo ni faini wanazodai kutozwa na askari wa Usalama Barabarani kwa makosa mbalimbali, ambazo kwa baadhi ya makosa zinaweza kufikia hadi shilingi milioni moja huku hali ya barabara nchini ikichangia makosa hayo.

Mbali na faini, madereva hao wanapinga pia hatua za kusimamishwa leseni, kupunguziwa pointi na hatimaye kupokonywa leseni za udereva baada ya alama kufikia kiwango cha mwisho.

Baadhi yao wameeleza kuwa baada ya kurejeshewa leseni, huagizwa kurejea shuleni kwa mafunzo kabla ya kuruhusiwa kuendelea na kazi, jambo ambalo wanasema linaongeza gharama na muda wa kukaa bila kipato.
Baadhi ya madereva waliyokutwa katika Kituo cha Magufuli waliyokataa kutaja majina yao, walisema wameamua kufanya mgomo huo kwa kuzingatia usalama wa magari wanayoyaendesha.

Walidai kuwa, kuna baadhi ya watu walitoshia kuyapiga mawe mabasi yao endapo yangeondoka kituoni kinyume na makubaliano ya wote kwamba wagome.

Zipo habari zinazodai kuwa, hata baadhi ya wamiliki walikubali madereva wao wasisafiri ili kuyanusuru mabasi yao na hujuma ambazo zingeweza kutekelezwa barabarani yakiwa safarini na baadhi ya watu waliyotishia kufanya hivyo.




Screenshot_20261001_232106_Google.jpg
 
Back
Top Bottom