Siri na fumbo la kifo (Dini & Sayansi) tukishakufa tunakwenda wapi?

Siri na fumbo la kifo (Dini & Sayansi) tukishakufa tunakwenda wapi?

SEHEMU YA I



Wasalaam,


View attachment 2193058



Miaka ile wakati ningali bado vidudu nilikatiza mitaa fulani kule Songea nlipokwenda kumtembelea mjomba (Marehemu) wangu mlevi.

Basi mida ya kila jioni tungevuka Ruhuwiko kushuka mpaka Lizaboni kwa Walevi wenzie wa Pombe za kienyeji.
Hapo angejigamba kwa walevi wenzio kwamba ' nipo na mtoto Pekee wa Dada yangu' , Jembe Langu huku akiwa na sauti yake Mbaya ya Ulevi ambayo sikuwahi kuipenda , Angetumia karibu Pesa yote kwa ajili ya Unywaji na kubakisha kidogo , Pengine ungedhani Aliacha ya Nauli kwa ajili ya daladala wakati wa kurejea nyumbani , Hapana.,
Angemaliza hapo angechukua Pesa iliyobaki na kununua Sigara.

Tungeendelea kukata mitaa kuvuka Mwembechai hadi mfaranyaki, kwenye Disco la Buhemba

Kwa bahati nzuri nlitokea katika familia yenye mafunzo ya kidini ,Basi sikusita kumuuliza Mjomba wangu huyu kuhusu mwenendo wake Huo

Majibu yake yalikuwa ni yale ,Tunatakiwa kuishi kwa Upendo hapo ungenwona akichukua sigara yake na kumpatia mvutaji mwingine alafu angekwambia huu ndio upendo,
Halafu atakujibu tunaishi mara moja tu , Unatakiwa kula Raha hakuna kinachoendelea zaidi ya hapa., hapo angekuongezea mishikaki mingine Uendelee kutafuna.

Kila nikienda kuzuru kaburi lake natamani kuumuliza , vipi kuhusu alichokiona baada ya Hapo ,kwa bahati mbaya sana Imani yangu haikunifundisha alichoamini








View attachment 2193046




Sayansi ya kisasa ina majawabu mengi sana kuhusu kifo na Mafumbo yake, na ndipo nlipochagua kuiweka sayansi kuwa namba mbili baada ya Mwenyezimungu....,imetoa majawabu tata na kugundua muundo wa michakato ya kibaolojia na ya mwili ambayo hutenganisha walio hai na marehemu.
Lakini pamoja na ujio wa uvumbuzi huu ambao umewezesha kutambua mambo kadhaa wa kadhaa , kwa njia fulani tofauti, Lakini kifo kimebaki kuwa Fumbo.



Kuhusu kifo hilo halina mjadala kwamba tutakufa .,sote kwasababu tunaona na tushaandikiwa katika imani zetu, hii ni faradhi (Lazima) ambayo kila mwanadamu ataipitia.











KIFO NI MCHAKATO MREFU


View attachment 2193067


Wengi wetu hufikiri kifo kitakuwa kama usingizi tu. Eti kwamba
Kichwa chako kinakuwa kizito.
Macho yako yanapunguza uwezo wa kuona na kufunga kwa taratibu
Pumzi ya mwisho , kisha…Mtu anakuwa tayari kashakufa.
La hasha! Yawezekana kuna mlolongo mrefu sana juu ya Kifo tusioujua.



View attachment 2193047


Dk. Sam Parnia, mkurugenzi wa utafiti wa huduma za wagonjwa mahututi katika Kituo cha Matibabu cha NYU Langone, anatafiti kuhusu kifo na katika tafiti zake amependekeza kuwa watu tunaendelea kubakiwa na fahamu zetu pindi tunapokufa.

Hii ni kutokana na mawimbi ndani ya ubongo kuendelea kupiga /kurusha kwenye gamba (kuta) la ubongo (sehemu ya fahamu, inayotumika kufikiri katika ubongo) kwa takriban dakika kadhaa baada ya kifo.


View attachment 2193069

Uchunguzi mwingine ulifanywa kwa panya wa maabara na ulionyesha akili zao ziliongezeka kasi na shughuli katika muda mfupi baada ya kifo,
na ilisababisha hali ya kusisimka na mabadiliko tofauti tofauti ya mwili.

Hali kama hizo zikitokea kwa wanadamu, inaweza kuwa uthibitisho kwamba ubongo huendelea kudumisha ufahamu mzuri wakati wa hatua za mwanzo za kifo.

Ikapendekezwa kwamba wakati huu ndiyo , mwanadamu hukumbuka karibu matukio mengi aliyoyafanya kipindi cha Maisha yake.




Jawabu hili linafanana na Jawabu la dini haswa 'Islamic' ya kwamba wakati huu ndiyo mwanadamu hukumbushwa mema yake Na mabaya yake aliyokwishakuyafanya akiwa duniani.






JE,UNAFIKIRIA NINI???


LAKINI KWANINI? TUJIFUNZE KUHUSU KIFO ILHALI HAKUNA KURUDI TENA??

Ingekuwa kuna yoyote alirudi akapata kusema kuna nini huko tungekuwa tumefumbua mafumbo mengi sana juu ya kifo












KIFO PEKEE SIO MWISHO KUNA SAFARI INAENDELEA.


View attachment 2193053

Kwenye dini zetu (Abrahamic Religions) hakuna atakayepinga ya kwamba kuna safari inaendelea baada ya kifo

Kuna maandiko tele yanayoelezea hilo

Mfano

Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa Hukumu

WARAKA WA WAEBRANIA 9:27




Na hata katika Qur'an tukufu yapo maandiko mengi ya dhahiri Yenye uthibitisho kuhusu Life after Death
Lakini vipi kuhusu sayansi


Katika Shule moja ya Tiba (Yale), watafiti walipokea ubongo wa nguruwe 32 waliokufa. Walitaka kufanya utafiti au kuwapa njia moja ya Ufufuo

Watafiti waliunganisha ubongo na mfumo wa wa bandia unaoitwa BrainEx.
Ilionekana kusukuma mtiririko wa damu katika ubongo, kuleta oksijeni , na virutubisho kwenye tishu

Mfumo huu ulihuisha ubongo na kuweka baadhi ya seli zao "hai" kwa muda wa saa 36 baada ya kifo.
Seli zilianza kutengeneza sukari (ya mwilini) na kuitumia hiyo sukari. Mifumo ya kinga ya ubongo pia nayo ilirejea.
Na baadhi ya sample ziliweza kubeba na kusafirisha mawimbi ya umeme.




Lengo la watafiti halisi kabisa lilikuwa kubuni teknolojia ambayo itatusaidia kuchunguza ubongo na utendaji wake wa seli kwa muda mrefu na kwa undani zaidi.
Kwa kutumia hii tunaweza kutengeneza matibabu mapya ya majeraha ya ubongo.
Basi hili likaleta picha kwa wanasayansi ambayo haina uthibitisho, Kwamba yawezekana baada ya teknolojia kukua zaidi kuna uwezekani ya kwamba kifo si tu pekee Safari ya Mwanadamu ya maisha bali., kuna safari nyingine.










JE,KUNA MAISHA BAADA YA KIFO???


View attachment 2193055

Kuna maisha baada ya kifo??
Hapana, sayansi bado haijapata uthibitisho wa maisha ya baada ya kifo au uzito wa roho. Lakini genes zetu huwa zinaendelea kuwa hai baada ya kufa kwetu.


Utafiti uliochapishwa katika Royal Society's Open Biology uliangalia genes za panya na pundamilia waliokwishakufa tayari.
Watafiti hawakuwa na uhakika kwamba Genes zilipungua uwezo(utendaji) polepole au zilikoma (utendaji) kabisa.
Lakini Walichokikuta kiliwashangaza.
Zaidi ya genes elfu moja zilianza kufanya kazi zaidi baada ya kifo.


Hawakutarijia hilo ,mwandishi wa utafiti na profesa wa biolojia katika Chuo Kikuu cha Washington, alisema
Lilikuwa ni jambo la kushangaza baada ya saa 24 baada ya kifo, unachukua sampuli ya Genes inaongezeka kwa wingi na utendaji wake
Hiyo ilikuwa ni jambo lenye kushangaza


Professa huyo na waandishi wenzake wanapendekeza hii inaonyesha kuwa mwili hupitia hatua tofauti tofauti za kuzima(Kufa) ,ikimaanisha kuwa wanyama wenye uti wa mgongo ikihusisha binaadamu hufa polepole na sio wote mara moja, na hivyo pengine kuna kinachoendelea baada ya kifo , Gene za ukuaji na ulinzi zilikonekana kuendelea kuwa Active.


Vitabu vya dini vinatufungulia ya kwamba kuna Ufufuo na Roho zetu zitarudi katika miili yetu ili kupokea malipo yetu vipi kuhusu tafiti hizi zinaleta picha ipi juu ya Maisha ya Baadae????
Baada ya Ufufuo na Maisha ya duniani.







Itaendelea


Da Vinci XV



SEHEMU YA PILI

TUKIFA TUNAENDA WAPI???
VITUO NA SEHEMU ANAZOPITIA MWANADAMU BAADA YA KIFO.


View attachment 2193045

View attachment 2193052
There is a life after death but it beyond a human capacity.Death is real but a riddle than life.
 
Mi naamini nikifa nitarudi duniani kama mtu mwingine tofauti.

Roho yangu ikitoka tu, bila kuchelewa inaenda kutafuta mama mjamzito ambaye kitoto kilichopo tumboni hakijaanza kuonesha uhai.

Hapo roho yangu ndiyo inaingia kwa hicho kitoto na hapo maisha mapya yanaanza.

Ila sidhani kama, nitatafuta mama wa kiafrika.
Maisha ya baadeye ninampango wa kuzaliwa kwa Putin.
Una mawazo kama yangu
NAMI huwa.kuwa Roho ana Nafsi ya Mtu ikitoka TU kwakel inahamia Kwa mtoto anayezaliwa...Kwa maana ukifa TU Ilala Roho Yako inakwenda kumuingia Mtoto anayezaliwa huko Amazon ama Bangladesh ama Kijijini China na Memory card Yako inaanza upya! Unakuwa Machina asijus lolote la Ilala!
Isingekuwa hivyo unadhani Roho Zote kutoka madhlani 1700 TU Mpaka Leo Zote zingeenea wapi!
 
Izi sayari zipo nyingi sana.
Nikifa naweza kuwa alien kwenye sayari ya mbali huko[emoji1787][emoji23]
 
Mi naamini nikifa nitarudi duniani kama mtu mwingine tofauti.

Roho yangu ikitoka tu, bila kuchelewa inaenda kutafuta mama mjamzito ambaye kitoto kilichopo tumboni hakijaanza kuonesha uhai.

Hapo roho yangu ndiyo inaingia kwa hicho kitoto na hapo maisha mapya yanaanza.

Ila sidhani kama, nitatafuta mama wa kiafrika.
Maisha ya baadeye ninampango wa kuzaliwa kwa Putin.
Kwaiyo tuseme roho ya Sulemani ilienda kwa Mswati
 
Mi naamini ukifa umekufa Imagine kifo chako umeliwa na mamba wamekugawana vjpande vipande na kukutafuna hapo hata genes zako zinakuwa hazionekani, ..

Hapa nakubaliana na mdau mmoja hapo juu aliyechangia kuwa, binadamu ama mnyama anapokuwa yupo katika harakati za kukata roho yani kufa roho yake huwa inaruka mahala pengine mfano kwa mama mjamzito na kuanza upya, maana mungu kazi ya uumbaji alisha imaliza kilichobaki cycle system tu

Dunia nimzunguko hata binadamu pia tunazunguka unakufa unazaliwa na roho ni zile zile

Ndugu zangu yote kwa yote hakuna kitu ninachokiogopa duniani kama kifo japo naelewa kufa ni lazima nitakufa ila ile kutangulia tu naogopa sana
Mbona idadi ya watu inaongezeka mkuu?
 
Back
Top Bottom