Siri na fumbo la kifo (Dini & Sayansi) tukishakufa tunakwenda wapi?

Mi naamini nikifa nitarudi duniani kama mtu mwingine tofauti.

Roho yangu ikitoka tu, bila kuchelewa inaenda kutafuta mama mjamzito ambaye kitoto kilichopo tumboni hakijaanza kuonesha uhai.

Hapo roho yangu ndiyo inaingia kwa hicho kitoto na hapo maisha mapya yanaanza.

Ila sidhani kama, nitatafuta mama wa kiafrika.
Maisha ya baadeye ninampango wa kuzaliwa kwa Putin.

Haha umenikumbusha,,,zamani nilikua najua ukifa unazaliwa upya ila sehemu nyingine dah!
 
SEHEMU YA I

Wasalaam,

View attachment 2193058

Miaka ile wakati ningali bado vidudu nilikatiza mitaa fulani kule Songea nlipokwenda kumtembelea mjomba (Marehemu) wangu mlevi.

Basi mida ya kila jioni tungevuka Ruhuwiko kushuka mpaka Lizaboni kwa Walevi wenzie wa Pombe za kienyeji.
Hapo angejigamba kwa walevi wenzio kwamba ' nipo na mtoto Pekee wa Dada yangu' , Jembe Langu huku akiwa na sauti yake Mbaya ya Ulevi ambayo sikuwahi kuipenda , Angetumia karibu Pesa yote kwa ajili ya Unywaji na kubakisha kidogo , Pengine ungedhani Aliacha ya Nauli kwa ajili ya daladala wakati wa kurejea nyumbani , Hapana.,
Angemaliza hapo angechukua Pesa iliyobaki na kununua Sigara.

Tungeendelea kukata mitaa kuvuka Mwembechai hadi mfaranyaki, kwenye Disco la Buhemba

Kwa bahati nzuri nlitokea katika familia yenye mafunzo ya kidini ,Basi sikusita kumuuliza Mjomba wangu huyu kuhusu mwenendo wake Huo

Majibu yake yalikuwa ni yale ,Tunatakiwa kuishi kwa Upendo hapo ungenwona akichukua sigara yake na kumpatia mvutaji mwingine alafu angekwambia huu ndio upendo,
Halafu atakujibu tunaishi mara moja tu , Unatakiwa kula Raha hakuna kinachoendelea zaidi ya hapa., hapo angekuongezea mishikaki mingine Uendelee kutafuna.

Kila nikienda kuzuru kaburi lake natamani kuumuliza , vipi kuhusu alichokiona baada ya Hapo ,kwa bahati mbaya sana Imani yangu haikunifundisha alichoamini

View attachment 2193046

Sayansi ya kisasa ina majawabu mengi sana kuhusu kifo na Mafumbo yake, na ndipo nlipochagua kuiweka sayansi kuwa namba mbili baada ya Mwenyezimungu....,imetoa majawabu tata na kugundua muundo wa michakato ya kibaolojia na ya mwili ambayo hutenganisha walio hai na marehemu.
Lakini pamoja na ujio wa uvumbuzi huu ambao umewezesha kutambua mambo kadhaa wa kadhaa , kwa njia fulani tofauti, Lakini kifo kimebaki kuwa Fumbo.

Kuhusu kifo hilo halina mjadala kwamba tutakufa .,sote kwasababu tunaona na tushaandikiwa katika imani zetu, hii ni faradhi (Lazima) ambayo kila mwanadamu ataipitia.

KIFO NI MCHAKATO MREFU

View attachment 2193067

Wengi wetu hufikiri kifo kitakuwa kama usingizi tu. Eti kwamba
Kichwa chako kinakuwa kizito.
Macho yako yanapunguza uwezo wa kuona na kufunga kwa taratibu
Pumzi ya mwisho , kisha…Mtu anakuwa tayari kashakufa.
La hasha! Yawezekana kuna mlolongo mrefu sana juu ya Kifo tusioujua.

View attachment 2193047

Dk. Sam Parnia, mkurugenzi wa utafiti wa huduma za wagonjwa mahututi katika Kituo cha Matibabu cha NYU Langone, anatafiti kuhusu kifo na katika tafiti zake amependekeza kuwa watu tunaendelea kubakiwa na fahamu zetu pindi tunapokufa.

Hii ni kutokana na mawimbi ndani ya ubongo kuendelea kupiga /kurusha kwenye gamba (kuta) la ubongo (sehemu ya fahamu, inayotumika kufikiri katika ubongo) kwa takriban dakika kadhaa baada ya kifo.

View attachment 2193069

Uchunguzi mwingine ulifanywa kwa panya wa maabara na ulionyesha akili zao ziliongezeka kasi na shughuli katika muda mfupi baada ya kifo,
na ilisababisha hali ya kusisimka na mabadiliko tofauti tofauti ya mwili.

Hali kama hizo zikitokea kwa wanadamu, inaweza kuwa uthibitisho kwamba ubongo huendelea kudumisha ufahamu mzuri wakati wa hatua za mwanzo za kifo.

Ikapendekezwa kwamba wakati huu ndiyo , mwanadamu hukumbuka karibu matukio mengi aliyoyafanya kipindi cha Maisha yake.

Jawabu hili linafanana na Jawabu la dini haswa 'Islamic' ya kwamba wakati huu ndiyo mwanadamu hukumbushwa mema yake Na mabaya yake aliyokwishakuyafanya akiwa duniani.

JE,UNAFIKIRIA NINI???

LAKINI KWANINI? TUJIFUNZE KUHUSU KIFO ILHALI HAKUNA KURUDI TENA??

Ingekuwa kuna yoyote alirudi akapata kusema kuna nini huko tungekuwa tumefumbua mafumbo mengi sana juu ya kifo

KIFO PEKEE SIO MWISHO KUNA SAFARI INAENDELEA.

View attachment 2193053

Kwenye dini zetu (Abrahamic Religions) hakuna atakayepinga ya kwamba kuna safari inaendelea baada ya kifo

Kuna maandiko tele yanayoelezea hilo

Mfano

Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa Hukumu

WARAKA WA WAEBRANIA 9:27

Na hata katika Qur'an tukufu yapo maandiko mengi ya dhahiri Yenye uthibitisho kuhusu Life after Death
Lakini vipi kuhusu sayansi

Katika Shule moja ya Tiba (Yale), watafiti walipokea ubongo wa nguruwe 32 waliokufa. Walitaka kufanya utafiti au kuwapa njia moja ya Ufufuo

Watafiti waliunganisha ubongo na mfumo wa wa bandia unaoitwa BrainEx.
Ilionekana kusukuma mtiririko wa damu katika ubongo, kuleta oksijeni , na virutubisho kwenye tishu

Mfumo huu ulihuisha ubongo na kuweka baadhi ya seli zao "hai" kwa muda wa saa 36 baada ya kifo.
Seli zilianza kutengeneza sukari (ya mwilini) na kuitumia hiyo sukari. Mifumo ya kinga ya ubongo pia nayo ilirejea.
Na baadhi ya sample ziliweza kubeba na kusafirisha mawimbi ya umeme.

Lengo la watafiti halisi kabisa lilikuwa kubuni teknolojia ambayo itatusaidia kuchunguza ubongo na utendaji wake wa seli kwa muda mrefu na kwa undani zaidi.
Kwa kutumia hii tunaweza kutengeneza matibabu mapya ya majeraha ya ubongo.
Basi hili likaleta picha kwa wanasayansi ambayo haina uthibitisho, Kwamba yawezekana baada ya teknolojia kukua zaidi kuna uwezekani ya kwamba kifo si tu pekee Safari ya Mwanadamu ya maisha bali., kuna safari nyingine.

JE,KUNA MAISHA BAADA YA KIFO???

View attachment 2193055

Kuna maisha baada ya kifo??
Hapana, sayansi bado haijapata uthibitisho wa maisha ya baada ya kifo au uzito wa roho. Lakini genes zetu huwa zinaendelea kuwa hai baada ya kufa kwetu.

Utafiti uliochapishwa katika Royal Society's Open Biology uliangalia genes za panya na pundamilia waliokwishakufa tayari.
Watafiti hawakuwa na uhakika kwamba Genes zilipungua uwezo(utendaji) polepole au zilikoma (utendaji) kabisa.
Lakini Walichokikuta kiliwashangaza.
Zaidi ya genes elfu moja zilianza kufanya kazi zaidi baada ya kifo.

Hawakutarijia hilo ,mwandishi wa utafiti na profesa wa biolojia katika Chuo Kikuu cha Washington, alisema
Lilikuwa ni jambo la kushangaza baada ya saa 24 baada ya kifo, unachukua sampuli ya Genes inaongezeka kwa wingi na utendaji wake
Hiyo ilikuwa ni jambo lenye kushangaza

Professa huyo na waandishi wenzake wanapendekeza hii inaonyesha kuwa mwili hupitia hatua tofauti tofauti za kuzima(Kufa) ,ikimaanisha kuwa wanyama wenye uti wa mgongo ikihusisha binaadamu hufa polepole na sio wote mara moja, na hivyo pengine kuna kinachoendelea baada ya kifo , Gene za ukuaji na ulinzi zilikonekana kuendelea kuwa Active.

Vitabu vya dini vinatufungulia ya kwamba kuna Ufufuo na Roho zetu zitarudi katika miili yetu ili kupokea malipo yetu vipi kuhusu tafiti hizi zinaleta picha ipi juu ya Maisha ya Baadae????
Baada ya Ufufuo na Maisha ya duniani.

Itaendelea

Da Vinci XV

SEHEMU YA PILI

TUKIFA TUNAENDA WAPI???
VITUO NA SEHEMU ANAZOPITIA MWANADAMU BAADA YA KIFO.

View attachment 2193045

View attachment 2193052
Illusion
 
Mitume walifanya kosa kubwa ambavyo hawakutuandikia kwenye Biblia au kumhoji Lazaro aliyefufuliwa. Hapo tu walifanya uzembe maana alikuwa na experience.
Lazaro inasemekana alikuwa akiulizwa ila hakuwa na majibu yoyote yeye alikuwa akiwaambia kwamba alikuwa usingizini wala hakumbuki chochote
 
but i can be transformed from one body to another
Energy is transferable to a different location or object, but it cannot be created or destroyed.

Transferable means capable of being transferred or conveyed from one place or person to another.

ROHO ni NISHATI na NISHATI hua haifi wala haiundwi ila ina uwezo wa kusafiri kutoka kwenye MWILI mmoja kwenda kwenye MWILI mwingine.

Km unavyoweza kulivua KOTI moja na kulivaa KOTI jingine, vivyo hivyo kwa ROHO husafiri kutoka MWILI hadi MWILI.

Sawa mkuu?
 
Waislam someni huu uzi kimbelembele chenu cha kuzika mapema mnazika watu walio hai wengi sana. Na sio ajabu wanafufuka tena wakiwa kaburini halafu hufa kwa hofu na kukosa oxjeni siajabu hupiga kelele sana mpaka wanakata roho.

Uko sahihi, kwani wanaocheleweshwa kuzikwa waliwahi kufufuka ili mantiki ya kuwahi kuzikwa ikose nguvu?
 
Soul can neither created nor destroyed but i can be transformed from one body to another and that's the cycle of life.

Zingine ni ngojera za dini ili wapate waumini.

#MaendeleoHayanaChama
Kwanini idadi ya watu duniani tunaongezeka?
 
Kuhusu mtu akifa huenda wapi nitajaribu kukuonyesha kwenye bible,,,Kumbukumbu la Torati 32:48-50 ""BWANA akasema na Musa siku iyo hiyo, akamwambia , 49. Kwea katika mlima huu wa Abarimu, mpaka kilima cha Nebo, kilicho katika nchi ya Moabu, kuelekea Yeriko; ukaangalie nchi ya kanaani niwapayo wana wa Israel Kuimiliki, 50 UKAFE KATIKA KILIMA, HUKO UKWEAKO,,UKUSANYWE UWE PAMOJA NA JAMAA ZAKO; KAMA ALIVYOKUFA NDUGU YAKO HARUNI KATIKA MLIMA WA HORI, AKAKUSANYWA AWE PAMOJA NA WATU WAKE.''''' Na siku ya hukumu kila mmoja atasimama mbele ya kiti cha enzi kwa ajili ya hukumu na kutakuwa na jamaa,kabila na taifa wote wamepangiliwa,,ambao hata katika kukusanywa baada ya kufa wote huwekwa kwa mpangilio huo.
 
SEHEMU YA I

Wasalaam,

View attachment 2193058

Miaka ile wakati ningali bado vidudu nilikatiza mitaa fulani kule Songea nlipokwenda kumtembelea mjomba (Marehemu) wangu mlevi.

Basi mida ya kila jioni tungevuka Ruhuwiko kushuka mpaka Lizaboni kwa Walevi wenzie wa Pombe za kienyeji.
Hapo angejigamba kwa walevi wenzio kwamba ' nipo na mtoto Pekee wa Dada yangu' , Jembe Langu huku akiwa na sauti yake Mbaya ya Ulevi ambayo sikuwahi kuipenda , Angetumia karibu Pesa yote kwa ajili ya Unywaji na kubakisha kidogo , Pengine ungedhani Aliacha ya Nauli kwa ajili ya daladala wakati wa kurejea nyumbani , Hapana.,
Angemaliza hapo angechukua Pesa iliyobaki na kununua Sigara.

Tungeendelea kukata mitaa kuvuka Mwembechai hadi mfaranyaki, kwenye Disco la Buhemba

Kwa bahati nzuri nlitokea katika familia yenye mafunzo ya kidini ,Basi sikusita kumuuliza Mjomba wangu huyu kuhusu mwenendo wake Huo

Majibu yake yalikuwa ni yale ,Tunatakiwa kuishi kwa Upendo hapo ungenwona akichukua sigara yake na kumpatia mvutaji mwingine alafu angekwambia huu ndio upendo,
Halafu atakujibu tunaishi mara moja tu , Unatakiwa kula Raha hakuna kinachoendelea zaidi ya hapa., hapo angekuongezea mishikaki mingine Uendelee kutafuna.

Kila nikienda kuzuru kaburi lake natamani kuumuliza , vipi kuhusu alichokiona baada ya Hapo ,kwa bahati mbaya sana Imani yangu haikunifundisha alichoamini

View attachment 2193046

Sayansi ya kisasa ina majawabu mengi sana kuhusu kifo na Mafumbo yake, na ndipo nlipochagua kuiweka sayansi kuwa namba mbili baada ya Mwenyezimungu....,imetoa majawabu tata na kugundua muundo wa michakato ya kibaolojia na ya mwili ambayo hutenganisha walio hai na marehemu.
Lakini pamoja na ujio wa uvumbuzi huu ambao umewezesha kutambua mambo kadhaa wa kadhaa , kwa njia fulani tofauti, Lakini kifo kimebaki kuwa Fumbo.

Kuhusu kifo hilo halina mjadala kwamba tutakufa .,sote kwasababu tunaona na tushaandikiwa katika imani zetu, hii ni faradhi (Lazima) ambayo kila mwanadamu ataipitia.

KIFO NI MCHAKATO MREFU

View attachment 2193067

Wengi wetu hufikiri kifo kitakuwa kama usingizi tu. Eti kwamba
Kichwa chako kinakuwa kizito.
Macho yako yanapunguza uwezo wa kuona na kufunga kwa taratibu
Pumzi ya mwisho , kisha…Mtu anakuwa tayari kashakufa.
La hasha! Yawezekana kuna mlolongo mrefu sana juu ya Kifo tusioujua.

View attachment 2193047

Dk. Sam Parnia, mkurugenzi wa utafiti wa huduma za wagonjwa mahututi katika Kituo cha Matibabu cha NYU Langone, anatafiti kuhusu kifo na katika tafiti zake amependekeza kuwa watu tunaendelea kubakiwa na fahamu zetu pindi tunapokufa.

Hii ni kutokana na mawimbi ndani ya ubongo kuendelea kupiga /kurusha kwenye gamba (kuta) la ubongo (sehemu ya fahamu, inayotumika kufikiri katika ubongo) kwa takriban dakika kadhaa baada ya kifo.

View attachment 2193069

Uchunguzi mwingine ulifanywa kwa panya wa maabara na ulionyesha akili zao ziliongezeka kasi na shughuli katika muda mfupi baada ya kifo,
na ilisababisha hali ya kusisimka na mabadiliko tofauti tofauti ya mwili.

Hali kama hizo zikitokea kwa wanadamu, inaweza kuwa uthibitisho kwamba ubongo huendelea kudumisha ufahamu mzuri wakati wa hatua za mwanzo za kifo.

Ikapendekezwa kwamba wakati huu ndiyo , mwanadamu hukumbuka karibu matukio mengi aliyoyafanya kipindi cha Maisha yake.

Jawabu hili linafanana na Jawabu la dini haswa 'Islamic' ya kwamba wakati huu ndiyo mwanadamu hukumbushwa mema yake Na mabaya yake aliyokwishakuyafanya akiwa duniani.

JE,UNAFIKIRIA NINI???

LAKINI KWANINI? TUJIFUNZE KUHUSU KIFO ILHALI HAKUNA KURUDI TENA??

Ingekuwa kuna yoyote alirudi akapata kusema kuna nini huko tungekuwa tumefumbua mafumbo mengi sana juu ya kifo

KIFO PEKEE SIO MWISHO KUNA SAFARI INAENDELEA.

View attachment 2193053

Kwenye dini zetu (Abrahamic Religions) hakuna atakayepinga ya kwamba kuna safari inaendelea baada ya kifo

Kuna maandiko tele yanayoelezea hilo

Mfano

Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa Hukumu

WARAKA WA WAEBRANIA 9:27

Na hata katika Qur'an tukufu yapo maandiko mengi ya dhahiri Yenye uthibitisho kuhusu Life after Death
Lakini vipi kuhusu sayansi

Katika Shule moja ya Tiba (Yale), watafiti walipokea ubongo wa nguruwe 32 waliokufa. Walitaka kufanya utafiti au kuwapa njia moja ya Ufufuo

Watafiti waliunganisha ubongo na mfumo wa wa bandia unaoitwa BrainEx.
Ilionekana kusukuma mtiririko wa damu katika ubongo, kuleta oksijeni , na virutubisho kwenye tishu

Mfumo huu ulihuisha ubongo na kuweka baadhi ya seli zao "hai" kwa muda wa saa 36 baada ya kifo.
Seli zilianza kutengeneza sukari (ya mwilini) na kuitumia hiyo sukari. Mifumo ya kinga ya ubongo pia nayo ilirejea.
Na baadhi ya sample ziliweza kubeba na kusafirisha mawimbi ya umeme.

Lengo la watafiti halisi kabisa lilikuwa kubuni teknolojia ambayo itatusaidia kuchunguza ubongo na utendaji wake wa seli kwa muda mrefu na kwa undani zaidi.
Kwa kutumia hii tunaweza kutengeneza matibabu mapya ya majeraha ya ubongo.
Basi hili likaleta picha kwa wanasayansi ambayo haina uthibitisho, Kwamba yawezekana baada ya teknolojia kukua zaidi kuna uwezekani ya kwamba kifo si tu pekee Safari ya Mwanadamu ya maisha bali., kuna safari nyingine.

JE,KUNA MAISHA BAADA YA KIFO???

View attachment 2193055

Kuna maisha baada ya kifo??
Hapana, sayansi bado haijapata uthibitisho wa maisha ya baada ya kifo au uzito wa roho. Lakini genes zetu huwa zinaendelea kuwa hai baada ya kufa kwetu.

Utafiti uliochapishwa katika Royal Society's Open Biology uliangalia genes za panya na pundamilia waliokwishakufa tayari.
Watafiti hawakuwa na uhakika kwamba Genes zilipungua uwezo(utendaji) polepole au zilikoma (utendaji) kabisa.
Lakini Walichokikuta kiliwashangaza.
Zaidi ya genes elfu moja zilianza kufanya kazi zaidi baada ya kifo.

Hawakutarijia hilo ,mwandishi wa utafiti na profesa wa biolojia katika Chuo Kikuu cha Washington, alisema
Lilikuwa ni jambo la kushangaza baada ya saa 24 baada ya kifo, unachukua sampuli ya Genes inaongezeka kwa wingi na utendaji wake
Hiyo ilikuwa ni jambo lenye kushangaza

Professa huyo na waandishi wenzake wanapendekeza hii inaonyesha kuwa mwili hupitia hatua tofauti tofauti za kuzima(Kufa) ,ikimaanisha kuwa wanyama wenye uti wa mgongo ikihusisha binaadamu hufa polepole na sio wote mara moja, na hivyo pengine kuna kinachoendelea baada ya kifo , Gene za ukuaji na ulinzi zilikonekana kuendelea kuwa Active.

Vitabu vya dini vinatufungulia ya kwamba kuna Ufufuo na Roho zetu zitarudi katika miili yetu ili kupokea malipo yetu vipi kuhusu tafiti hizi zinaleta picha ipi juu ya Maisha ya Baadae????
Baada ya Ufufuo na Maisha ya duniani.

Itaendelea

Da Vinci XV

SEHEMU YA PILI

TUKIFA TUNAENDA WAPI???
VITUO NA SEHEMU ANAZOPITIA MWANADAMU BAADA YA KIFO.

View attachment 2193045

View attachment 2193052
Kwa uelewa wangu ni niliyofundishwa.

Kama mtu kazaliwa ina maana ipo siku atakufa na kuna maisha baada ya kifo mtu mwenye Mungu wa kweli hapaswi kuogopa kifo maana kifo ni njia ya mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine .

Wakati mtu anazaliwa anakuwa na nafsi ,roho na namba. Nafsi itafanya yote wakati wa uhai wa mtu na roho kazi yake ni ku record matendo yote yanayofanywa na binadamu huyo yawe mabaya au mazuri,hivyo mtu akifa wanabaki roho na roho inakuwa na tabia zote ambazo alikua nazo mtu huyo wakati wa uhai wake. Mtu akifa anakua amechana na uchafu wote wa mwili hapa ndio mtu huitwa mtakatifu yani ametakata hana uchafu wowote. Utukufu maana yake utu=mtu kufu=kufa hivyo mtu kama ni mtukufu tayari ameshakufa na kila kiumbe mfu ni kitukufu hata kama ni majini au watu au msimu. Ila kutukuza hufanyika kwa kiumbe kilichokufa ambacho kilitenda mema wakati wa uhai wake kama kusaidia watu na vinginevyo na kutukuza hufanyika katika kaburi la huyo mtu

Hivyo mtu akifa kama alitenda mabaya anaenda sehemu yake na kama alitenda mazuri anaenda sehemu ambayo watu walitenda mazuri ila inshort ni mada ndefu sana hapa ila kifupi ni hivyo!
 
Soul can neither created nor destroyed but i can be transformed from one body to another and that's the cycle of life.

Zingine ni ngojera za dini ili wapate waumini.

#MaendeleoHayanaChama

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ulishawahi Kufa Janja ?
Ww kabla ya kuja Duniani unajua ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nn? Lkn ww unazokumbukumbu zozote za maisha ya Tumboni kwa mzazi? Ulijua unafanya nn huko?

Ukitulia kwa umakini utaelewa dhana ya kifo ni Safari nyingine juu ya yule aliyetuumba.
 
Hata wewe jiulize hivyo hivyo, why uniulize mimi ?

Mi nawaza ni sawa na umeme kukatika na Kurudi , anyway am joking .

I have no Idea and I am grateful Kuwa arrive mpaka sana na sijui ni kwa nini.

Mungu anirehemu.
 
Kama ingekuwa hivyo basi dunia ingebaki na idadi ileile ya watu. Maana ingekuwa na kwenye mpira wachezaji 11 tu, hivyo akitoka mmoja anaingia mmoja.
Na ndivyo ilivyobanazaliwa mmoja anakufa mmoja , ila kuna soul nyingne zimetekwa
 
Mfano wa kifo ni usingizi. Baada ya kutolewa roho mtu aliyekufa anakuwa anafeel kama yuko kwenye ndoto
Naungana na huyu
Ukifa unakuwa Kama umelala, na unakuwa unaota ndoto za Kama vile umepotea na uko ardhi ya mbali ambako huwezi kurudi sehemu unayo ishi, au uko porini ambako huwezi kufika eneo la mjini.
Ukifa pia unaenda kuishi maisha ya kidogo roho na watu wengine waliokufa. Mwanzo utakuwa mpweke kwa sababu utakuwa unapambana kurudi eneo lako la makazi, badae utagundua kuwa haiwezekani kuwa hivo na hiyo itapelekea uanze kuzoea maisha mapya.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu mtu akifa huenda wapi nitajaribu kukuonyesha kwenye bible,,,Kumbukumbu la Torati 32:48-50 ""BWANA akasema na Musa siku iyo hiyo, akamwambia , 49. Kwea katika mlima huu wa Abarimu, mpaka kilima cha Nebo, kilicho katika nchi ya Moabu, kuelekea Yeriko; ukaangalie nchi ya kanaani niwapayo wana wa Israel Kuimiliki, 50 UKAFE KATIKA KILIMA, HUKO UKWEAKO,,UKUSANYWE UWE PAMOJA NA JAMAA ZAKO; KAMA ALIVYOKUFA NDUGU YAKO HARUNI KATIKA MLIMA WA HORI, AKAKUSANYWA AWE PAMOJA NA WATU WAKE.''''' Na siku ya hukumu kila mmoja atasimama mbele ya kiti cha enzi kwa ajili ya hukumu na kutakuwa na jamaa,kabila na taifa wote wamepangiliwa,,ambao hata katika kukusanywa baada ya kufa wote huwekwa kwa mpangilio huo.
Sawa
Lakini umesoma Andiko lote mkuu??
 
Back
Top Bottom