Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
Mjadala huu utakuwa na sehemu kuu NNE.
SEHEMU YA KWANZA: Msingi Wa Mkataba Ulikiukwa, Woga Wa CCM Serikali Tatu.
Mchakato wa Katiba Mpya ulitoa fursa pekee kwa CCM kurekebisha kasoro zilizojitokeza huko nyuma ambazo ndio zimezaa "kero sugu" za muungano. Iwapo CCM ingekiri makosa hayo huku ikitoa sababu mbalimbali za kihistoria na mazingira ya dunia ya wakati ule kwa ujumla, wananchi wengi wangesema "Yaliyopita Si Ndwele, Tuyagange Yaliyopo na Yajayo". CCM ingepata fursa ya kuaminiwa na sehemu kubwa ya umma na kushirikiana na chama hiki katika uzinduzi wa Tanganyika.
Hii ilikuwa ni fursa adimu ya chama (CCM) kuhakikisha kwamba: (1) inarithisha vijana wake Chama ambacho kimemaliza kazi ya kulimaliza ‘jinamizi' lililosumbua chama na taifa kwa miaka zaidi ya 30; (2) Chama kinajenga mazingira ya kukomesha "Suala la muungano" kuwa ni "suala la vyama vya siasa" bali suala la "kitaifa"; (3) Chama kinalinda na kuboresha muungano kwa kufuata mapendekezo ya tume ya mabadiliko ya Katiba. Hatua ya chama kuendelea kutetea serikali mbili katika mchakato wa Katiba, ni sawa na kuamua kuendelea kulea Kero za Muungano, na sio kuzipunguza kero hizi kama chama kinavyodai [rejea kauli za CCM za hivi karibuni kupitia Katibu Mkuu Taifa (Abdurahaman Kinana), na Katibu wa CCM NEC Taifa (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye].
Mkataba wa Muungano (1964) ulitoa sura ya kuwepo kwa shirikisho la serikali tatu [Masuala kumi na moja ya Muungano, huku masuala nje ya haya kumi na moja yakibakia kwa serikali za nchi shiriki za muungano (Yani Serikali Ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar)]. Chini ya mfumo huu wa serikali tatu, kati ya serikali hizi mbili shiriki (Tanganyika na Zanzibar), hakuna Serikali iliyopangwa na Mkataba wa Muungano kuwa na madaraka makubwa kuliko serikali nyenzake. Kilichobadilisha yote haya ilikuwa ni chama cha TANU kuingilia suala la muungano kinyume na mkataba wa muungano (1964).
MKATABA WA MUUNGANO: Vyanzo (Sources):
1. Jumbe, A (1995): The Partner - Ship: Muungano Wa Tanganyika na Zanzibar: Miaka 30 Ya Dhoruba.
2. Shivji, I (2008): Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika and Zanzibar Union.
Inaendelea bandiko linalofuata (#2).
Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.
cc Nguruvi3, @FJM,@ tpaul, @Mag3, @JokaKuu, @Mwigulu Nchemba, @Nape Nnauye, @MwanaDiwani,@zomba, @Ritz, @ZeMarcopolo, @Gamba la Nyoka, @Mtanganyika , @Mzee Mwanakijiji, @Pasco, @Kitila Mkumbo, @EMT, @MTAZAMO, @Kobello, @Jasusi, @zumbemkuu, @Mimibaba, @Zakumi, @Invisible, Kurugenzi ya Habari, @mnyepe, @Yericko Nyerere, @FaizaFoxy, @Dingswayo, @Makusudically, @Tumaini Makene, @Nicholas, Mtu wa Pwani, jmushi1, Mwita Maranya, Ngongo, zumbemkuu, Mzawa Halisi, Barubaru, Mindi, Kiganyi, Communist

MKATABA WA MUUNGANO
Baina ya
JAMHURI YA TANGANYIKA
Na
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR
Kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zinafahamu uhusiano wa muda mrefu watu wake na mshikamano na kukuza uhusiano huo na kuimarisha mshikamano na kukuza umoja wa watu wa Afrika, zimekutana na kutafakari Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.
Na kwa kuwa Serikali za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, zinapendelea ya kwamba Jamhuri hizi mbili ziungane kuwa Jamhuri moja huru moja kwa amasharti ya makubaliano yafuatayo:
Kwa hiyo IMEKUBALIWA baina ya Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar kama ifuatavyo:-
(i) Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa Jamhuri huru moja.
ii) Katika kipindi cha kuanza kwa Muungano mpaka Baraza la Kutunga katiba lililotajwa katika ibara ya (vii) litakapokutana na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano (Kuanzia hapa kitaitwa kipindi cha mpito), Jamhuri ya Muungano itaongozwa kwa masharti ya ibara ya (iii) mpaka ya (vi).
(iii) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kuweka:
a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho katika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa Zanzibar;
c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano;
d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.
(iv) Mambo yafuatayo yatakuwa chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano:-
a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
b) Mambo ya nchi za nje
c) Ulinzi
d) Polisi
e) Mamlaka yanayohusika na hali ya hatari
f) Uraia
g) Uhamiaji
h) Mikopo na biashara ya nchi za nje
i) Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
j) Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha
k) Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu
v) Bunge na Serikali vilivyotajwa vitakuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano na kuongezea mamlaka juu ya mambo yote yahusuyo Tanganyika.
Sheria zote zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yao bila kuathiri:-
a) Masharti yoyote yatakayowekwa na chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria.
b) Masharti yatakayowekwa kwa amri ya Rais wa Zanzibar juu ya sheria yoyote inayohusu jambo lolote lililotajwa kwenye ibara ya (iv), na kufuta sheria yoyote inayolingana Zanzibar.
c) Mabadiliko yoyote kama yataonekana yanafaa au kuhitajika ili kufanikisha Muungano na mkataba huu.
(vi) (a) Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano atakuwa ni Mwalimu J. K. Nyerere na ataongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kufuata masharti ya mkataba hu na kwa kusaidiwa na maofisa wengine atakaowateuwa toka Tanganyika na Zanzibar na watumishi wa Serikali zao.
b) Makamo wa kwanza wa Rais kutoka Zanzibar aliyeteuliwa kwa kufuata marekebisho kama yalivyoelezwa na ibara ya 3, atakuwa Sheikh Abeid Karume.
(vii) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar
a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.
(viii) Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.
KWA KUSHUHUDIA HAPA Julius K. Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na abeid Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wametia saini nakala mbili za mkataba huu, hapa Zanzibar siku ya tarehe Ishirini na mbili ya mwezi Aprili, 1964.
___________________________
Umepitishwa katika Bunge siku ya tarehe Ishirini na Tano ya Aprili, 1964.
P. MSEKWA
…………………..Karani wa Bunge
Nathibitisha kwamba Muswada wa Sheria hii ulipitishwa na Bunge kwa mujibu wa ibara ya 35 ya katiba.
A.S. MKWAWA
..........………………………..Spika
25, Aprili 1964.