Siri Ya Hati Ya Muungano Na Njama Za Kuuficha

Siri Ya Hati Ya Muungano Na Njama Za Kuuficha

MAJI SHINGONI, 'MKATABA' WAPELEKWA DODOMA
NI BAADA YA UDANGANYIFU, HAKUNA AJUAYE NI UDANGANYIFU PART II?
NGUVU YA UMMA HAIJWAHI KUSHINDWA. CCM HAIONI MAONYO 10 YALIYOPITA.

Sehemu ya I

Bandiko la Mchambuzi limetukokota kuanzia safari ya Tanganyika hadi Tanzania na leo 'Tanzania mkanganyiko'

Ktibu mkuu kiongozi na waziri wameahidi kuufikisha 'unaoitwa mkataba wa muungano bungeni'. Pamoja na yote hayo ukweli unabaki kuwa 'uhuni wa mwanzo' hautoi nafasi kuaminika tena.
Sote tunafahamu mkataba feki umekanushwa na wahusika akina Msekwa na wazee wengine.

Balozi Sefue ametoa maelezo akililia lia kuhusu wananchi kushindwa kuwaelewa wanaohoji mkataba. Balozi Sefue na serikali ni kama wamechanganyikiwa.

Hoja za Lissu, Tundu hazijajibiwa, kilichofanyika ni kulia lia.
Wananchi kwa miaka mingi wamedai hati ya mkataba kwa kilio, leo wapi serikali ya CCM inapata ushujaa na mshipa wa kuwasemea eti wamefedheheshwa

Maswali yanayobaki kutojibiwa ni haya yafuatayo
1. Kwanini kwa miaka mingi serikali iligoma kuutoa na leo unapelekwa Dodoma kirahisi?
2. Kwanini serikali ilipeleka mkataba feki ikijua mkataba halisi upo na unatakiwa ?
3. Je, ni kweli kuwa UN iliwahi kuleta telex za kuomba mkataba, na majibu yake yalikuwa ni nini?
4. Je, mkataba umesajiliwa UN kwa mujibu wa taratibu kama ulivyombwa na maafisa wa UN?

Maswali hayo ndiyo yataka kiu ya wananchi na wala si kupeleka mkataba.
Tayari serikali imeshaonyesha udanganyifu nani wa kuamini tena karatasi kutoka Ikulu.
Hili si tatizo la wananchi ni tatizo la Ikulu.

Nafasi ya kuongelea mkataba alikuwa nayo Rais. Suala la mkataba si la leo au jana.
Rais akachagua njia ya kumshambulia Warioba ili kujenga uhalali wa anachOkitaka na si kile wananchi wanachotaka.

Leo Warioba amesimama akizungukwa na nyota zinazo ng'aa, giza nene likimgubika Rais wetu.

Swali lianalogonga vichwa vya watu ni hili, je, kuna nini kimefanya CCM iachie mkataba hata pale ilipogoma baada ya amri ya mahakama? Je, kweli ni mkataba halali au ni part II ya feki lingine?

Kwamba hili laweza kuwa ni mkataba feki, hilo halina shaka.
Kama waliweza kughushi wiki moja iliyopita, 'wahuni' hawawezi kubadili tabia siku 7 baadaye. Huu ni uhuni wa miaka 50 hivyo unahitaji rehabilitation nzito si program ya siku 7

Kwanini CCM wameamua kuutoa?
Kuna sababu kadha wa kadha
1. Kwamba, hoja walioijenga ya rasimu feki ya CCM ya serikali 2 itakufa kama mkataba hautoki.
Hoja ya CCM ni kuwa, msingi wa mkataba ni serikali 2.

Ingawa hoja halisi ni serikali 3 kama tulivyoonyeshwa na Mchambuzi hapo juu, kwa ulaghai wa kughushi maneno, wanakamati wa kamati za CCM bungeni wamelishwa maneno ya msingi wa mkataba ni serikali 2.

Kama CCM hawatoa mkataba uwe halali au feki, hoja yao itakosa mashiko.
Hoja itakayokuwa mbele ni moja, tuanze upya au jahazi livunjwe tugawane mbao.
Sisi wameshikwa kunako, na hakika wanatamani maliwato.Tumbo limevurugika.

2. CCM wasipotoa mkataba uwe halali au feki, hii itaanzisha mtinange (cascade of reactions) na hivyo kupelekea umoja wa mataifa kuhoji kuhusu uhalali wa muungano.
Hapo kunaweza kuibuka yasiyotarajiwa. CCM wanaepusha shari.

3. Nguvu ya umma: CCM imeshindwa kukabliana na nguvu ya umma.
Umma unaamini kuwa kinachosemwa na watu wengine ni ukweli vinginevyo hakukuwa na sababu za kupeleka mkataba feki.

Umma unaamini kuwa Makamu wa Rais na waziri mkuu mstaafu Warioba, Waziri mkuu mstaafu na katibu mkuu wa OAU Salim, Katibu myeka wa Nyerere mzee Butiku, Maprofesa na tume, wana sababu za msingi na za maana kuutaja mkataba katika rasimu.

Wana nia njema na walitaka jambo hilo likamilike kwa kupitia rasimu ya serikali 3 ambayo leo kungekuwa hakuna hoja hiyo.

CCM kwa kutotambua nguvu ya umma na kwa uzoefu wa udanganyifu wakajua kila jambo litapita kama upepo.
Tumeandika mara saba sabini kuwa hakuna mahali popote duniani dola iliwahi kushinda nguvu ya umma.
Kinachotokea sasa hivi ni nguvu ya umma kuanza kujidhihiri.

CCM kwa kuto ona maonyo bado wanaendelea na kiburi chao. Licha ya binu zao kufeli huko nyuma, CCM hawaonekani kujifunza lolote.

Hebu tuangalie dalili za nguvu ya umma, sehemu ya II

Inaendelea....
 
Last edited by a moderator:
Muungano uko kizimbani, utasurubiwa neno kwa neno na utageuzwa kila upande,

Tanganyika imezikwa kwa mabavu, itarejeshwa kidemokrasia.

Mabadiliko ya katiba ya 1984 ndio yaliyoizika rasmi Tanganyika na hili lilitukia kama jibu kwa Abdul Jumbe.
 
i am very privileged kujifunza toka kwa MCHAMBUZI

nadhani ni wachahce sana nchini waliokua na knowledge iliyotolewa humu... unfortunately siasa zimetawala, na ni kitu kibaya sana kwani hata mambo muhumu yatavalishwa jezi yaonekani yana sura z vyama

NAONA SIASA ZIMESHASHIKA HATAMU NA KUACHA FACTS ZIWE KAMA USHABIKI
 
Sehemu ya II

Nguvu ya umma ilianza katika mtiririko huu

1. Makundi na watu kuhoji muungano
Akina Jumbe, G55 , vyama vya siasa na wanataaluma.
CCM ikaunda tume 8 zilizokutana na nguvu ya umma na kuishauri ibadili mfumo wa muungano

2. Kuanzishwa kwa vyama vingi
CCM ikatumia white paper iliyokuja na majibu ya 20 Vs 80 ikipendelea chama kimoja
CCM ya wazee wenye busara ikajua ni nguvu ya umma inajijenga, mbele ya safari haizuiliki

3. Wananchi kudai haki, uwepo wa tume huru ya uchaguzi ili kuleta usawa katika demokrasia
CCM na serikali yake zikatumia ubabe wa katiba iliyopo kujenga uhalali wa uharamu.

2. Wananchi wakadai kuandikwa katiba mpya kupitia mchakato wa mkutano wa kitaifa
CCM ikaunyakua mchakato na kuunda tume yake yenyewe

3. CCM na Rais wakaandaa mswada wa kuzuia muungano usizungumzwe kabisa
Samwel Sitta akakutana na nguvu ya umma mswada ukachomwa moto akiona kwa macho yake

Nguvu ya umma ikatamka, mabadiliko hayaepukiki.
Warioba na tume wakaandika rasimu kutokana na hoja za nguvu ya umma.

4. CCM ikaunda mabaraza ya kata ili kujaza watu wake
Nguvu ya umma ikashinda pale pesa ilipotumika. Umma ukasema mabadiliko ni wakati wake sasa.

5. CCM ikatumia mbinu za kuchagua wabunge kupitia mwenyekiti wao Rais wa JMT
Nguvu ya umma ikaelekeza miongoni mwa hao wajumbe wengi wanaona mabadiliko hayaepukiki

5. CCM ikaandika mswada uliopitishwa na 1/3 ya bunge kufuta tume ya Warioba isiingie bunge ili wachakachue.Sauti ya umma bado ikawa inaita kutoka nyikani.

6. CCM na Samwel John Sitta wakapanga mbinu za kumdhalilisha Warioba
Warioba akazungukwa na nguvu ya umma ikimtetea bila yeye kutamka neno hata moja

7. CCM ikamfanya Warioba public enemy number 1
Warioba akawa kipenzi cha wananchi hata kusahau makando kando yake ya nyuma.

8. Samwel Sitta akabadili kanuni ili kupata wajumbe wa kamati anaowataka na CCM
Nguvu ya umma ikamsota kidole hadi akabadili mawazo kwa aibu na haya

9. CCM wakasomeshana kuhusu msimamo wa serikali 2
Umma umegoma kuwaelewa na kilichobaki ni kusukumiza hoja.
Hoja za muungano kwasababu tumeoeleana.

10. CCM ikachomeka hoja za gharama
Umma ukauliza hizo ni za wenzenu, zenu zipo wapi?

11, CCM ikaandika rasimu ya mafichoni ili vifungu 1 na 6 vitenguliwe
Umma ukasema miaka 50 hamjaweza, leo mna dawa gani mpya zaidi ya ile tuliyozoea?

12. CCM ikaanza kualika vikongwe na maajuza kwenda kula mikate Ikulu kuunga mkono hotuba
Hakuna anayesikiliza wala kuangalia picha.
Nguvu ya umma inasema chai na juisi si tatizo la nchi hii

13. CCM ikaanza kuwashambuliwa wanaopinga ikiwemo kuwatisha wabunge wake.
Sauti ya umma kutoka nje inawanyooshea vidole na kusema hiyo si hoja tulioiambia tume.

14. CCM ikapeleka mkataba feki wa muungano
Umma ukasema mwaka 1964 bill gate alikuwa mtoto, Computer gani iliandika mkataba.

15. CCM ikaunda kamati za wengi na wachache
Wachache wamesema na wanasikika, CCM imetoka mafichoni.

Wanasayasansi wanasema vitu vina 'yield point' kwamba ukikivuta kitu zaidi ya hapo hukatika au kuharibika. CCM inauvuta umma hadi yield point, sijui nini kitatokea yarabi!

Wanamazingira wanasema wingu na upepo hutangulia mvua

Waumini wanasema mungu akileta heri zake huzileta kwa namna tofauti lakini pia hutoa maonyo.
Kwa mfano, mtu anapotoka mvi au kibiongo ni dalili kuwa muda wa kurejea kwa muumba upo karibu.

Dalili zote hapo juu zinaashiria kuwa CCM imeshindwa na nguvu za umma.
Kwamba, kama yalivyo mataifa duniani CCM haiwezi kukabiliana na nguvu ya umma.

Ni suala la muda tu kama Shah wa Iran alivyolindwa na vifaru na mwisho wa siku akaingia mtaroni kwenda uhamishoni. Ndivyo alivyokuwa Fernandis Macos na Ceuscu wa Romania.

Nini mkakati wa CCM kupingana na nguvu ya umma siku zijazo? Tuataeleza mkakati wa kura ya maoni na tume itakayosimamia.

Tutaendelea, kwasasa tusemezane kidogo.
 
MAPITIO MUHIMU YA HATI YA MUUNGANO

Sehemu ya kwanza kabisa ya mkataba wa muungano inasema hivi

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Zinaungana na kuwa JAMHURI HURU MOJA.

Mkataba hausemi NCHI MOJA. Umuhimu wa neno "Jamhuri" ni kwamba, matumizi ya neno hili kikatiba ni kwamba Jamhuri hufuata mfumo wa kisiasa wa URAIS, na sio Mfalme au Sultani. Chini ya mfumo huu, supreme power zipo kwa wananchi ambao huchagua maafisa na wawakilishi wa kuwatumikia katika nafasi mbalimbali za umma.

Swali linalofuatia ni je, kwanini Mkataba wa muungano (1964), katiba ya muda (1965) zote zilitumia maneno - "jamhuri moja ya muungano", na hazikutaja nchi?

Jibu ni kwamba, chini ya Jamhuri, mbali ya mamlaka ya mwisho kuwa kwa wananchi (sio mfalme), pia kikatiba, unaweza kuwa na nchi zaidi ya moja. Hapa nikisema nchi, nina maana "state". Kwa mfano, marekani ni a constitutional republic yenye "states" 50, kila moja ikiwa na serikali yake zikiwa na autonomy katika mambo kadhaa nje ya yale chini ya shirikisho (federal government). Kwa mantiki hii, hata mkataba wa makubaliano uliheshimu dhana hii ya kishirikisho ambapo the states of Tanganyika and Zanzibar ilikuwa ziungane katika mambo machache tu.

Baada ya muungano kuishi kwa miaka kumi na tatu kwa utambulisho wa "jamhuri huru moja", toleo la awali kabisa la Katiba ya JMT (1977) likabadilisha maneno ya awali ya mkataba wa muungano (1964) na Katiba ya muda ya JMT (1965) kwa kuondoa neno "huru" na kutamka haya:

Tanzania ni Jamhuri ya Muungano

Kwanini neno "huru" liliondolewa? Je, hali hii iliathiri vipi makubaliano ya mkataba (1964)? Jibu rahisi ni kwamba uhuru wa jamhuri hizi kabla ya muungano, utambulisho wa uhuru wao/sovereignty (as individual states) ukaanza kuchakachuliwa. Hali hii ilienda sambamba na ongezeko la orodha ya mambo ya muungano kila kukicha, kinyume na yaliyotamkwa ndani ya hati ya muungano (1964), lengo likiwa kujenga mazingira ya kuizika kabisa Tanganyika, na pia kuipa mamlaka zanzibar - yale ya kiasi tu/semi-autonomous status.

Miaka saba baada ya toleo la kwanza la katiba ya JMT (1977) kutoka, Katika toleo lake la pili, katiba ya JMT (1977) kupitia sheria namba 15 ya mwaka 1984, ikafanya mabadiliko mengine muhimu ambapo sehemu ya kwanza ya katiba ikasomeka ifatavyo:

Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano
.

Je, nini kilipelekea mabadiliko haya? Jibu ni kwamba, utambulisho wa awali chini ya toleo la kwanza la katiba ya JMT (1977), kwa vile haukuzungumzia Tanzania kama nchi moja, kulitokea upenyo wa kisheria kwa Zanzibar kurudi katika mkataba wa muungano (1964) kutambua states zilizopo and their corresponding governments katika masuala nje ya muungano, hivyo mantiki ya shirikisho la serikali tatu. Lakini baada ya harakati hizi za Jumbe na serikali tatu kushindwa, ndipo haraka haraka sheria namba 15 ikapitishwa na bunge la muungano kuibadilisha Tanzania kuwa nchi moja, miaka 20 baada ya mkataba wa muungano. Kwa maana nyingine, mkataba wa muungano uliheshimu uwepo wa nchi mbili zitakazounda shirikisho, kama ilivyo kwa dhana ya "united states" of america.

Rasimu ya katiba (2014) inatamka kwamba:

Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi na shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanziba ambazo kabla ya hati ya makubalianno ya muungano, 1964, zilikuwa nchi HURU.

Tume ilijisahau katika hili:

Tukitazama rasimu katika nukuu hiyo, kitendo cha rasimu kuweka maneno muungano (unitary) na shirikisho (federal) kwa pamoja inaleta mgongano wa katiba juu ya mfumo wa serikali/utawala. Kwa maaa nyingine, unitary and federal can't go together kikatiba. Hili ni moja ya mapungufu kadhaa ya rasimu. Kamati ya Lissu imependekeza mabadiliko ya kipengele hiki lakini sio kwa hoja hii bali kwa hoja kwamba hati ya makubaliano bila ya kujalisha kama ni genuine au sio haiweze kuwa ni msingi wa muungano kwa vile haikutekelezwa (ilichakachuliwa katika miaka yote 50). Lakini pamoja na hayo, bado mabadiliko ya kifungu hiki kupitia wajumbe wachache kupitia Tundu Lissu wamefanya mabadiliko yanayo tatua tatizo nalojadili. Lissu kama msemaji msemaji wao amependekeza mabadiliko ili sehemu hiyo isomeke kwamba:

Shirikisho la jamhuri za Tanganyika na Zanziba ni shirikisho ambalo limetokana na muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa zanzibar.

Maoni ya wengi (CCM) katika kamati zote ni kwamba neno "muungano" liendelee kuwepo. Likibakia, basi unitary system will prevail kwani itakuwa rahisi kwa ccm na serikali yake kuendeleza hoja yao juu ya "maboresho". Na kwa bahati mbaya sana, tume ya katiba ilijisahau na kuliacha neno "muungano". Kwahiyo hoja ya wachache kwamba sehemu ya kwanza haiwezi fumuliwa kwani ndio msingi wa rasimu yenyewe, halafu hapo hapo kina Lissu kubadili kwa nia njema tu, itakumbana na hoja kali ya CCM kwamba neno "muungano" lililetwa na rasimu hivyo libaki kama lilivyo.

For Lissu et al, The Devil is in the details.
Nadhani the best way out of this trap kwa kundi "wachache" ni kurudi katika hoja ya rasimu kwamba mkataba wa muungano ndio msingi, tofauti na msimamo wa Lissu tuliojadili hapo juu. Kwa maana hii, kuna haja ya kushinikiza ibara ile ile Lissu anaipinga 1(3) ya rasimu ndio itoe mwongozo. Kwa maana nyingine, maoni ya wachache yanawezwa kulindwa na ibara ya 1(3) ya rasimu inayosema:

Hati ya makubaliano ya muungano iliyorejewa katika ibara ndogo ya (1) ndio msingi mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na katiba hii, kwa kadri itakavyo rekebishwa, itakuwa ni muendelezo wa makubaliano hayo.

Pia kuna uwezekano kwamba ibara hii 1(3) ya rasimu (2014) inagongana na kilichokubaliwa kwenye mkataba wa muungano (1964) kwamba:

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Zinaungana na kuwa JAMHURI HURU MOJA.

Kwani rasimu inasema:

Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi na shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanziba ambazo kabla ya hati ya makubalianno ya muungano, 1964, zilikuwa nchi HURU.

Kwahiyo ibara ya 1(3) ya Rasimu kutamka maneno husika hapo juu inaenda nje kidogo ya mkataba wa muungano (rejea rasimu inavyotambulisha muungano, halaf fananisha na utambulisho ndani ya hati ya muungano, 1964 hapo juu) - hasa neno "muungano" kuingizwa kwenye utambulisho ndani ya rasimu, hivyo kuleta mgongano na nguzo ya shirikisho iliyokusudiwa. Lakini rasimu imerudisha neno moja muhimu ambalo katika ya JMT (1977) kama tulivyojadili, ililiondoa - yani maneno "Jamhuri huru".

Lakini tatizo la rasimu ni kwamba imeongeza neno "nchi", ambalo halikuwepo katika mkataba wa muungano (1964), na awali tumejadili significance ya neno hili la "nchi".

Matumizi ya neno "nchi" kwa upande wa tume, na upande wa maoni ya wachache BLK ni tatizo kwani haiendani na yaliyotamkwa ndani ya mkataba wa muungano (1964) ambao unasema katika sehemu yake ya kwanza:

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Zinaungana na kuwa JAMHURI HURU MOJA.

Awali tulijadili madhara ya utangulizi wenye maneno haya kwa kulinganisha na katiba ya JMT toleo la kwanza 1977 na marekebisho ya katiba hiyo (1984).

Tutaendelea kuchambua hati ya muungano na kuitazama kwa sura ya katiba ya sasa (1977), pamoja na rasimu ya katiba (2014), huku tukitazama kwa ukaribu pia maoni ya wengi na wachache kwenye kamati mbali mbali pamoja na michango ya wajumbe wa BLK kwa ujumla.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Unaweza kufafanua kidogo hoja hii? Inaonekana kusheheni vitu muhimu sana kwa ajili ya mjadala.



kama nilivyojadili kule kwenye mdahalo juu ya nini bora kati ya maboresho ya serikali mbili au azimio la arusha, bila ya kujalisha mapungufu ya azimio hili for a second, framework ya implementation zote za development policies and planning, injection ya state capital and AID katika ujenzi wa uchumi kupitia state led development, na pia provision za huduma za msingi za afya (elimu, afya, maji), framework iliyotumika katika kipindi cha 1967-1995 ilikuwa ni Azimio La Arusha. Kuanzia 1995, new framework imekuwa ni vision 2025.

Nikirudi kwenye hoja yako ya msingi katika nukuu yako hapo juu, nakubaliana nawe kwamba Azimio la arusha halikufika zanzibar. Swali linalofuatia ni je, nini ilikuwa ni madhara ya azimio kutofika kule kwa miaka 28 ya development planning nchini? In other words, Kuna hoja kwamba Tanzania bara ilirudi nyuma kimaendeleo kutokana na azimio hili (mimi na wewe -pia Nguruvi3 na wengine - tumeshajadiliana sana suala hili huko nyuma), je zanzibar ilirudi nyuma zaidi kwa kutolitambua azimio hili? Ilienda mbele? Ilibakia ilipo?

Chini ya vision 2025 as a new framework, does Zanzibar share the same vision? Why?why not?

Tukumbuke pia moja ya makosa makubwa huko nyuma kikatiba ilikuwa ni kwa katiba ya JMT kutoweka kwa uwazi masuala ya social justice and economic justice kwa wananchi ndani ya washirika wa muungano. Kwahiyo ingawa azimio declared hiki na kile kwa miaka 28, huku fedha za walipa kodi zikitumika under azimio as a framework of implementation for 28 years, social and economic justice hazikuwa zikitambulika kikatiba.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums


Mchambuzi:

Umeniomba nifafanue, ukweli sina cha muhimu cha kuongezea. Hila kati ya moja ya sheria ulizotoa (bandiko # 21), inaonyesha kuwa mkataba huu kwa muda fulani ulikuwa the supreme law of the union. Kwa mfano kuna vipengele vinaanza:

2. Bila ya kuathiri masharti ya Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ...

3. Bila ya kuathiri masharti ya Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ...


Je ni lini vipengele kama hivi vilianza kukiukwa?

Tukirudi kwenye Azimio la Arusha. Inawezekana lilikuwa na manufaa au halina manufaa. Huo ni mjadala wenye sehemu yake.

Katika masuala ya maendeleo ya katiba. Azimio la Arusha lina mchango wake. Tanganyika ilikuwa ni constitutional Republic wakati inapata uhuru (Serikali iliyochaguliwa na watu kwa kufuata misingi ya katiba).

Kuanza kwa mfumo wa chama kimoja 1965 na kutangazwa kwa Azimio la Arusha, Tanzania ikawa republic ya wakulima na wafanyakazi (soviet republic). Katika muundo huu wa soviet republic, Kamati na Halmashauri za chama zina maamuzi makubwa kuliko bunge. Vilevile miongozo ya chama na katiba ya chama inakuwa na nguvu kuliko katiba ya nchi.

Mabadiliko makubwa ya katiba ya Tanzania yaliotuondoa kutoka kwenye constitutional republic kwenda republic ya wakulima na wafanyakazi (soviet republic) yalitokea baada ya maamuzi makubwa ya chama au kisiasa yakiwemo ya azimio la arusha na kuzaliwa kwa CCM.

Tatizo kubwa lililopo sasa sio kuwa watu wengi hawaifahamu Tanganyika. Tatizo kubwa ni kuwa Tanganyika ili-practise constitutional republic kwa muda mfupi sana. Na Zanzibar haiku-practise kabisa. Hivyo watu wengi wanaofanya maamuzi ya kisiasa bado wana fikra na mazoea ya soviet republic. Wakiachana na fikra hizo basi hawatakuwa na tatizo la kuusoma mkataba na wapi ulikiukwa.
 
ANGALIZO MUHIMU KUHUSU RATIFICATION YA HATI YA MUUNGANO NA BARAZA LA MAPINDUZI ZANZIBAR.

Suala hili linazidi kujaa utata kila kukicha. Kwanza, uachama wa Tanganyika, Zanzibar, na Tanzania kwenye UN unaelezwa hivi:

Tanganyika was admitted to the UN on 14 December 1961, and Zanzibar was admitted to the UN on 16 December 1963. Following the ratification on 26 April 1964 of the Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar, the two states merged to form the single member "United Republic of Tanganyika and Zanzibar", with its name changed to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964.

Uanachama wa Tanganyika - nadhani huu ni straight forward kwani any sovereign state inaweza apply for UN membership na kukubaliwa kwa utaratibu uliopo. Ndio maana tunaona Tanganyika ikikubaliwa uanachama muda sio mrefu baada ya uhuru wake.

Uanachama wa Zanzibar - ingawa nao unafuata maelezo na mchakato kama wa Tanzania hapo juu, kuna tofauti ndogo. Kwa maelezo ya kwenye nukuu pale juu, sovereignty ya Zanzibar inayotambuliwa ni Uhuru wa 1963, sio Mapinduzi ya Mwaka 1964. Kwa maana hii, wakati wa mapinduzi, zanzibar tayari mwanachama wa UN.

SWALI:
Je, mkataba wa muungano (1964) pamoja na kubeba sifa za makubaliano kimataifa, unatambulika kimataifa? Tulidhania hivyo, lakini taarifa za hivi karibuni kutoka Umoja wa Mataifa kukana kwamba hawajawahi kupata nakala ya hati ya muungano unaleta mashaka kuhusu muungano huu kutambulika na sheria za Kimataifa. Lakini mashaka hayo yanapatiwa mwanga ingawa kidogo na Makomenn(1984) hapo chini pale anaposema:

Zanzibar existed as an independent state only for four and a half months (December 10, 1963 to April 26, 1964), and there is no doubt that Nyerere's formula which was devised for Tanganyika was equally responsible for external affairs.

Tutaona umuhimu wa hoja hii hapo chini. Kwa sasa, tuangalie swali lingie.

SWALI:
JE, Vipi Kuhusu Muungano Kutambulika na Sheria za ndani ya nchi shiriki za muungano (Tanganyika na Zanzibar)?

It gets even more interesting:

Yilma Makonnen (1984) katika kitabu chake titled: "The Nyerere Doctrine of State Succession and the New States of East Africa", anasema hivi:

Upon its independence from Great Britain, Zanzibar did not make any official declaration explaining its position with regard to the effect of state succession on international rights and obligations of the colonial predecessor state which applied or extended to or contracted on behalf of Zanzibar. Even upon the request of the Secretary General of the United Nations, zanzibar refrained from making any statement clarifying its position.

Makonnen anaendelea kusema:

However, the most important factors here are, first, that zanzibar did not sign the usual inheritance agreement with Britain and did not unilaterally declare that it was bound by the treaties and other obligations of the predecessor state.

This is where it gets even more interesting:

Second, before making any clarification on this subject Zanzibar UNITED with Tanganyika, forming the United Republic of Tanganyika. Zanzibar existed as an independent state only for four and a half months (December 10, 1963 to April 26, 1964), and there is no doubt that Nyerere's formula which was devised for Tanganyika was equally responsible for external affairs. This is evidenced by the Union and Tanganyika Act, 1964, and by the note sent by President Nyerere after the unification adopting a single formula except for specific provisions identified with one or the other territory. President Nyerere's note to the Secretary General declared that all treaties "remain in force within the regional limits prescribed on their conclusion and in accordance with the principles of international law.

The total silence of Zanzibar during its brief existence as an independent state, surely could have created some problems though in retrospect and from the practice we saw, there was no sign of such problem. It is in reference to a situation identified to zanzibar that professor Lissizyn correctly commented:

"Some new states seem to have continued to apply certain pre-existing treaties de facto without any declarations or agreement...although avoiding sudden discontinuity leaves the international legal effect of the treaties in question quite uncertain. It leaves the new states free in commitments by the same token provides no assurance of reciprocity"

Zipo hoja kwamba baraza la mapinduzi halikuthibitisha mkataba wa muungano (1964) kwa theluthi mbili kama ilivyotakiwa.

Katika kitabu chake cha Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika and Zanzibar Union (2008), Issa Shivji anajadili nyaraka moja ya CIA titled - "The Current Disarray in Zanzibar, 2, December 1968. Lengo la ripoti hii ya CIA ilikuwa ni kufanya tathmini ya muungano miaka minne baada. Katika ripoti hiyo, CIA ikasema kwamba kwa upande wa Zanzibar, muungano haukuwa popular, kiasi kwamba hata ratification ya Baraza La Mapinduzi haikufika 2/3, bali iliyopatikana ilikuwa ni1/3.

SWALI:
Kwa vile kanuni ya 2/3 majority inatokea British Parliamentary System. Lakini hapo awali, tumeona kwamba Zanzibar mara tu baada ya uhuru na mapinduzi, haikusema lolote iwapo itarithi na kuheshimu treaties and conventions za mwingereza. Je, hoja ya zanzibar and ratifications by 2/3 ina mashiko gani iwapo kufikia siku ya Mkataba, zanzibar haikuwa ime-declare kwamba it was bound by the treaties and other obligations of the predecessor state (Great Britain), hasa kanuni ya 2/3 majority katika chombo cha kutunga sheria (Bunge)? Katika hali hii, je itakuwa sahihi tukisema kwamba -basi hata 1/3 ilitosha for ratification? Au hata uamuzi wa mtu mmoja (Karume) ulitosha?

Pengine wenye uelewa wa masuala ya sheria watasaidia kutuelimisha kwani kwa mtu wa kawaida asiye na uelewa husika, it gets very confusing.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
kp16042014.jpg


Mchambuzi

Tatizo la nchi nyingi zilizo katika kundi la nchi zinazoendelea hasa za kiafrika uwazi katika uendeshaji wa serikali haupo, hali kadhalika kukosekana kwa reflection ndio kunakofanya mambo kutoyaweka sawa na kuishia kutumia ujanjaujanja wakati jibu lingekuwa rahisi mno kama ulivyosema.

Kama ilivyo taswira ya mwana kartoon Kipanya hapo juu, enzi hizo zilikuwa za kisultani na kitemi, wakishaamua wa juu hakuna kupinga vinginevyo ni kukosa heshima, ndio maana watu maarufu kama akina hayati Kambona, na Mzee Edwin Mtei walipohoji na kutaka yale wanayofikiri yanafaa walionekana kwa wakati huo ni kukosea kutomsikiliza mzee wa nchi.

Kuna viashiria kwamba kwa upande wa bara walao jambo hilo lilifikishwa bungeni ingwa si kwa taratibu zinazotakiwa lakini kulikuwa na dalili za ushirikishwaji tofauti na huko Visiwani ambako usultani ulikuwa bado haujatoweka Karume aliweza kujichukulia jukumu bila kushirikisha hata kupata maoni kutoka baraza la wawakilishi.

Jambo la msingi serikali kama ulivyoainisha ilikuwa na nafasi tele kujenga utetezi wa mazingira na mazingara ya wakati huo na mambo yangeeleweka kuliko kuendeleza usaiii ambao kwa kizazi cha dot com si rahisi kukisadikisha.

Pengine ni aibu kwa kiongozi kama Kikwete ambaye ulimwengu unamwona kama anamwelekeo wa kupokeleka kimataifa kushindwa kukishawishi chama chake CCM na hivyo kufikia hali hii ya wajumbe walio wachache ambao wana uwakilishi mpana zaidi katika taifa kususia bunge la katiba mpya.
 
Back
Top Bottom