Siri Ya Hati Ya Muungano Na Njama Za Kuuficha

Siri Ya Hati Ya Muungano Na Njama Za Kuuficha

Inatoka bandiko #16


UNDANI WA SHERIA NAMBA 18 YA MWAKA 1964.

Awali tulijadili moja ya nyaraka za Muungano ziliyowasilishwa Dodoma – yani Sheria Namba 22, ya April 25, mwaka 1964. Tuliona kwamba, licha ya nyaraka iliyowasilishwa kuchakachuliwa saini za Nyerere na Msekwa, bado nyaraka hii sio Msingi wa Muungano bali Mkataba/Hati Ya Muungano (1964) ambayo hadi sasa kinachoendelea juu ya upatikanaji wake ni mazingaombwe. Rasimu Ya katiba (2014) imeweka wazi katika sura yake ya kwanza kwamba msingi wa Muungano uliopo ni Hati ya Makubaliano (1964). Rasimu Ya Katiba hii haijataja Sheria Za Muungano zilizofuatia baada ya HATI YA MUUNGANO, kutiwa Saini. Sababu za Rasimu kutofanya hivyo ni za wazi, hivyo hatuna haja ya kujidaili kwa sasa.

Katika sehemu inayofuata tutaitizama nyaraka nyingine iliyowasilishwa Dodoma – yani Sheria Namba 18, ya Machi 24, Mwaka 1965, kisha tutajadili kwanini, kama ilivyoile nyaraka nyingine (sheria namba 18, 1965), Nyaraka hii (Sheria namba 22, 1965), pia ni batili kwa matumizi ya Muungano .

UMUHIMU WA sheria namba 18 ulikuwa ni kuichakachua ibara ya ibara ya (7) ya Mkataba wa Muungano ambayo ilielekeza Rais Wa Muungano na Makamu wake (Rais wa Zanzibar) katika kipindi cha mpito (Mwaka Mmoja), waunde TUME YA KATIBA na BARAZA LA KUTUNGA KATIBA. Ibara hii ya (7) ya Mkataba wa Muungano inasema hivi:

(vii) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar
a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.

b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Lakini kilichotokea MWEZI MMOJA tu kabla ya kipindi cha mpito (mwaka mmoja) kuisha muda wake, Bunge la Muungano likapitisha sheria tajwa hapo juu (Sheria Namba 18 ya Mwaka 1965). Lengo la Sheria ilikuwa ni kuhairisha masharti ya ibara ya ibara hii (7) ya Mkataba wa Muungano kwa muda usiojulikana, hivyo kwenda kinyume na maelekezo ya Mkataba wa Muungano (1964).

Sheria Namba 18 ya Mwaka 1965 ilieleza yafuatayo:



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Sheria Namba 18 ya 1965




NAKUBALI


J.K NYERERE


Rais


MACHI 24, 1965


Sheria ya Kuongeza Muda Wa Kuitisha Baraza La Kutunga Katiba

Jina Fupi na Tafsiri Sheria Na. 22 1964 GN. Na 243 1964
IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


1. Sheria hii inaweza ikaitwa Sheria ya Baraza la Kutunga Katiba ya 1965 na itasomwa kama sheria moja na Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Kuongeza muda wa kuteua Tume ya Kuitisha Baraza la Kutunga Katiba
2. Bila ya kuathiri masharti ya Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar au yale ya Mkataba wa Muungano baina ya jamhuri ya zamani ya Tanganyika na Jamhuri ya zamani ya watu wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano hatalazimika kuteua Tume ya kutoa mapendekezo ya katiba kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano, au kuitisha kikao cha Baraza la Kutunga Katiba kwa ajili ya kuyatafakari mapendekezo hayo na kupitisha Katiba, katika kipindi cha mwaka mmoja toka kuanza kwa Muungano isipokuwa Rais kwa kukubaliana na makamu wa Rais ambae ndiye Mkuu wa Serikali ya Zanzibar atateua Tume hiyo na kuitisha kikao cha Baraza la Kutunga Katiba wakati atakaoona unafaa.





3. Bila ya kuathiri masharti ya Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar marejeo ya Sheria hizo kuhusu Baraza la kutunga Katiba lililoitishwa kwa mujibu wa kifungu cha (2) cha sheria hii lakini kuyafanya yawe yametolewa na Mkataba wa Muungano na kipindi cha mpito kiichoelezwa humi kitaongezwa muda itakavyokuwa.





Nathibitisha kuwa Muswada kuwa Sheria hii ulipitishwa na Bunge kwa mujibu wa masharti ya ibaraya 35 ya Katiba.





Dar-es-salaam
A.S MKWAWA

MACHI 24, 1965
Spika




Umepitishwa na Bunge siku ya Kumi na Nane Ya Mwezi wa Machi, 1965.






P. MSEKWA


Karani wa Bunge




Source: [Source: Jumbe, A (1995): The Partner-ship – Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Miaka 30 Dhoruba.

Kufuatia sheria hii, Muungano ukakosa fursa muhimu ya kupata katiba yake ya kudumu kwa mujibu wa matakwa ya ibara ya (7) ya mkataba wa muungano (1964), na badala yake muungano ukaingizwa chini ya Katiba ya muda kwa muda usiojulikana. Huu ulikuwa ni mwanzo wa tatizo kubwa mbeleni kama Shivji (1990, 2005 &2008) anavyolijadili.

Sambamba na Sheria hii namba 22 ya Mwaka 1965, MIEZI MINNE baadae, Bunge la Muungano pia likapitisha sheria nyingine – tarehe 11, Julai 1965, sheria iliyojulikana kama "KATIBA YA MUDA YA TANZANIA (Sheria no. 43) ambayo ilitengeneza madaraka kwa serikali ya jamhuri ya muungano na pia kwa serikali za nchi washiriki wa muungano.

  • Je, Katiba Ya Muda (1965) ilitambua uwepo wa TANGANYIKA?



Inaendelea bandiko linalofuatia…
 
inatoka bandiko #21

KATIBA YA MUDA YA MUUNGANO (1964) NA UTAMBULISHO WA TANGANYIKA

Pamoja na kwamba sheria Namba 43 ya Mwaka 1965 ambayo ndiyo iliyozaa Katiba ya muda (1965) ilikuwa ni kinyume cha Mkataba wa Muungano (1964), lakini bado Katiba hii ya muda iliweka misingi ya serikali TATU, sio serikali MBILI, wala sio serikali MOJA.

Tuitazame Sheria Namba 43 - Katiba ya Muda(1965) kama ilivyowasilishwa na [Source: Jumbe, A (1995): The Partner-ship – Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Miaka 30 Dhoruba.

KATIBA YA MUDA, 1965

Sheria ya kutangaza Katiba ya Muda ya Tanzania

(11 Julai, 1965)
Sheria Na. 43, 1965
KWA KUWA uhuru, haki, udugu na amani vinapatikana kwa kutambua haki za watu wote na heshima yao ya asili, na kutambua haki za watu wote kupata hifadhi ya maisha, uhuru na mali, uhuru wa dhamiri, uhuru wa kutoa mawazo na kujiunga katika vikundi, kushiriki katika serikali yao, na kupata ujira wa haki kutokana na kazi:

NA wakati watu wanapoungana pamoja katika jamii ni wajibu wao kuheshimu haki na heshima za watu wengine, kuheshimu sheria za nchi, na kufanya shughuli za nchi ili kuhifadhi maliasili, kuziendeleza na kuzitumia kwa faida ya raia wote kwa ujumla na ili kuepusha unyonyai wa mtu na mtu:

NA KWA KUWA hazi hizo zinadumishwa na kulindwa vizuri na wajibu huo kutimizwa kwa haki katika jamii ya kidemokrasi ambapo serikali inawajibika kwa bunge huru lililochaguliwa kuwakilisha wananchi na ambapo mahakama zipo huru na zisizopendelea:

KWAHIYO BASI KATIBA HII, ambayo inaunda Serikali ya Tanzania kama jamii ya kidemokrasia hapa INATUNGWA NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.


SURA KWA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO, CHAMA NA WATU
SEHEMU YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO NA CHAMA

1. Tanzania ni Jamhuri Huru ya Muungano.

2. (1) Eneo la Tanzania ni eneo lote la Tanganyika na Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo inapakana nayo.


(2) Mamlaka ya kisheria inayohusika inaweza kuigawa Tanzania katika mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo.

3. (1) Kutakuwa na Chama Kimoja Cha Siasa katika Tanzania.

(2) Mpaka hapo Tanganyika African National Union (TANU) itakapoungana na Afro Shiraz Party (ASP), chaka hicho kwa Tanganyika kitakuwa Tanganyika African National Union (TANU) na kwa Zanzibar kitakuwa Afro Shiraz Party (ASP).

(3) Shughuli zote za kisiasa katika Tanzania, isipokuwa zile za vyombo vya dola ya Jamhuri ya Muungano, vyombo vya serikali na chombo cha Kutunga Sheria kwa Zanzibar au vya serikali za mitaa kama vitakavyoundwa kwa au chini ya sheria ya mamlaka husika, zitafanywa chini ya usimamizi wa chama.

(4) Katika ilionyesha katika Nyongeza ya kwanza ya katiba hii itakuwa katiba ya Tanganyika African National Union (TANU), na katiba hiyo inaweza kurekebishwa wakati wowote (na masharti yaliyomo ndani yake na baada ya Muungano wa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shiraz Party (ASP), kwa mujibu wa masharti yaliyomo ndani ya katiba hiyo.


KATIBA INAENDELEA….




Itaendelea bandiko linalofuata ambapo pia tutajadili jinsi gani Katiba ya muda (1965) bado ilitambua shirikisho la serikali tatu. Hii ni kinyume na kauli ya waziri mkuu pinda kwamba Tanganyika ilitoweka mwaka 1964.
 
Inaendelea toka bandiko namba 22

HATA KATIBA YA MUDA (1965) ILILINDA MFUMO WA SERIKALI TATU

Pamoja na makiuko kadhaa ya mkataba wa muungano 91964) yaliyojitokeza ndani ya katiba ya muda (1965), kwa mfano Katiba ya Muda (1965) Kuifanya Katiba ya chama cha TANU, kuwa ni sehemu ya Muungano/Katiba ya Jamhuri ya Muungano, lakini bado katiba hii ya muda ilitoa heshima iliyostahili kwa Tanganyika. Katiba hii iliweka wazi kwamba Katiba hiyo ni ya Tanzania nzima, ikiwa ni jamii ambayo imeungana na kuwa mamlaka moja ya Jamhuri ya Muungano na kwamba ilikuwa lazima katika hali hiyo kutengeneza kanuni za haki na wajibu wa jamii husika.

Ibara ya (1) ya Katiba hii ya Muda inatamka wazi wazi kuwa “Tanzania ni nchi iliyoungana na kuwa mamlaka moja”. Huu ulikuwa ni msisitizo kwamba muungano ulihusisha taifa au nchi zaidi ya MOJA. Ibara ya (2) ya katiba hii inaenda mbali zaidi na kutaja wazi majina ya nchi au mataifa yaliyoungana kuwa ni “TANGANYIKA NA ZANZIBAR”. Swali linalofuata ni je:

· Inakuwaje watu waanze kusema kwamba Tanganyika ilitoweka mwaka 1964? Huu ni uthibitisho kwamba kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hivi karibuni kwamba Tanganyika ilitoweka mwaka 1964 sio kweli kwani bado tunaiona Tanganyika ndani ya Katiba ya Muda (1965), na ikaendelea kutambulika kwa miaka mingine miwili zaidi hadi pale ilipokuja futwa na Sheria Namba 24 ya Mwaka 1967, sheria ambayo ilikuwa ni kinyume na mkataba wa muungano (1964).[B/]

Tutajadili hili baadae kwa undani.

Kama zilivyo ibara za Mkataba wa Muungano (1964), Katiba ya muda (1965) pia ina vifungu vinavyoelekeza serikali tatu (Tanganyika, Zanzibar, na Muungano), na serikali za Tanganyika na Zanzibar zinatajwa kwa majina yake kamili kama nchi zilizoungana kutengeneza mamlaka moja ya jamhuri ya muungano. Ibara ya 12(1) kwa mfano inasema:

Mamlaka ya kiserikali juu ya muungano na kuhusu Tanganyika yanawekwa katika mikono ya Rais.

Kama tulivyoona jadili awali, mamlaka kuhusu Tanganyika kuwa katika mikono ya Rais wa Muungano ilikuwa ni suala la muda mfupi – kipindi cha mpito kuelekea katiba mpya nay a kudumu ya Jamhuri ya Muungano. Tukirudi kwenye hoja yetu ya msingi juu ya Tanganyika kutambuliwa na katiba ya muda (1965), ibara ya (130) ya katiba hii inasema kwamba kutakuwa na makamu wawili wa Rais ambao wataitwa “Makamu wa kwanza wa Rais” na “Makamu wa pili wa rais”. Ibara hii inaendelea kueleza kwamba “mmoja wa makamu wa rais atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa Rais wa Muungano wakati akitekeleza kazi zake kuhusiana na Zanzibar. Huyu atakuwa ni Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Serikali ya Zanzibar.

Makamu mwingine atakuwa ni “msaidizi mkuu wa Rais katika utekelezaji wa kazi kuhusiana na Tanganyika”. Ibara hii ni ushahidi wa wazi kabisa kwamba mfumo wa serikali uliokusudiwa hata chini ya katiba ya muda (1965) ulikuwa ni mfumo wa shirikisho la serikali tatu.
· Je, tunahitaji ushahidi gani zaidi kuelewa Katiba ya Muda (1965) ilikusudia kuwepo kwa mamlaka tatu tofauti zenye uhusiano – nazo ni serikali ya Muungano na Serikali za Tanganyika na Zanzibar?

MUHIMU

1. Katiba ya Muda (1965) inahimiza juu ya umuhimu wa makamu wawili wa rais (Tanganyika na Zanzibar) kumsaidia Rais wa Muungano katika uendeshaji wa masuala yaliyo nje ya yale yaliyoorodheshwa kuwa ni ya muungano (masuala kumi na moja). Kwa maana hii, ni wazi kabisa kwamba Katiba ya muda hii iliwekeza juhudi kubwa kuhakikisha kwamba kunakuwepo na “USAWA” wa hadhi baina ya Tanganyika na Zanzibar kama nchi shiriki katika jamhuri ya muungano.

2. Chini ya Katiba ya muda (1965), bado tunaona Tanganyika ikitajwa na kutambuliwa kwa mujibu wa sheria. Hii ni tofauti na kauli ya Waziri Mkuu Pinda kwamba Tanganyika ilitoweka mwaka 1964.

Ibara ya (49) ya Katiba ya muda (1965) pia inasema kwamba:

Mamlaka ya kutunga sheria kuhusiana na mambo yote ya muungano kwa ajili ya jamhuri ya muungano na kuhusiana na mambo mengine yote ndani na juu ya Tanganyika, yanawekwa katika bunge.

· Ibara ya (53) ya katiba hii pia inazungumzia suala hili kwa upande wa Zanzibar. Yote hii juhudi kubwa za katiba hii kuhakikisha kwamba kunakuwepo na “USAWA” wa hadhi baina ya Tanganyika na Zanzibar kama nchi shiriki katika jamhuri ya muungano.

Pia kama bado tunakumbuka vyema (rejea mkataba wa muungano), ibara ya (5) ya mkataba wa muungano (1964), ibara hii ilithibitisha kuendelea kuwepo kwa sheria za Tanganyika na Zanzibar katika maeneo yanayohusika. Ibara ya 53(3) ya katiba ya muda (1965) inaendelea kutoa uthibitisho juu ya suala hili, ikilenga kubakisha dhana ya kuwa na mfumo wa shirikisho katika mgawa wa maeneo ya kuendesha utawala.

Ibara ya 23(3) ya katiba ya muda inazidi kuthibitisha mfumo wa shirikisho la serikali tatu ambapo mambo yanayoangukia katika maeneo ya muungano na Tanganyika na yale yanayoangukia ndani ya mamlaka ya Zanzibar yanaainishwa pale ibara ya 23(3) katiba hii inapotamka kwamba:

Ibara hii itawahusu watu waliotiwa hatiani na kuhukumiwa na hukumu hizo kutekelezwa Zanzibar chini ya sheria ya bunge la muungano au sheria ifanyayo kazi Zanzibar, na juu ya watu waliotiwa hatiani na kuhukumiwa na hukumu kutekelezwa Tanganyika.


inaendelea katika bandiko linalofuata



Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla
 
Inatoka bandiko #24


KUPOTEZWA KWA TANGANYIKA

Mkataba wa Muungano (1964) haukulenga kuifuta au kuipoteza Tanganyika bali kuiacha iwepo na serikali yake na mfumo wake wa utawala kwa hali ya usawa kama ilivyokuwa kwa Serikali ya Zanzibar na mfumo wa utawala wake. Kama tulivyoona awali, vifungu mbali mbali vya Mkataba wa Muungano (1964) pamoja na Katiba ya Muda (1965) vinathibitisha ukweli huu.

Kwa mfano, awali tuliona kwamba jaribio la kwanza la kuifuta Tanganyika lilifanyika kupitia sheria ya namba 22 ya mwaka 1964 au Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sheria hii ilikuja siku moja tu baada ya Makubaliano ya Muungano kusainiwa. Hii ni moja ya nyaraka zilizowasilishwa Dodoma hivi karibuni. Ibara ya 7 ya sheria hii namba 22, ya mwaka 1964, inasema kwamba(tunajikumbushia tena):

Wakati wa katiba ya muda ya jamhuri ya muungano itakapoanza kutumika, Katiba ya Tanganyika itakoma kuwa na nguvu kwa ajili ya serikali ya Tanganyika kama sehemu tofauti ya jamhuri ya muungano.

Kama tulivyojadili, hii ilikuwa ni kinyume cha mkataba wa muungano (1964) kwani kwa mujibu wa mkataba huu, nchi mbili huru (Tanganyika na Zanzibar) zilikubaliana na hiyari yao kuungana katika masuala machache tu huku mengine kila nchi ikibakia na mamlake yake ya kuyaendesha na kuyasimamia. Muhimu zaidi ni kwamba, ilikubaliwa kwamba katika kipindi cha mpito – kwa maana – kutoka siku ya muungano hadi pale baraza la kutunga katiba litakapoitisha Katiba mpya na ya kudumu ya Tanzania, serikali na bunge la Tanzania (muungano) litaifanyia kazi pia serikali ya Tanganyika. Lakini haikutakiwa suala hili lidumu zaidi ya mwaka mmoja. Kipengele hiki ndani ya Mkataba wa muungano kilikuwa ni muhimu kwa vile:

Tanganyika ilikuwepo, Tanganyika ilikuwa na Serikali yake kamili, watumishi wake, na mamlaka yake juu ya eneo lote la Tanganyika juu ya masuala yasiyo ya muungano. Mkataba wa muungano haukutoa ruhusa kwa katiba ya Muungano kuiendesha Tanganyika. Badala yake, ilielekeza kwamba Katiba ya Tanganyika irekebishwa ili itumike kama Katiba ya Muungano katika kipindi cha mpito (mwaka mmoja) huku ibara ya (7) ya mkataba wa muungano (1964), ikisubiri kutekelezwa. Kwa maana hii, ili kusimamia mambo ya Tanganyika, Rais wa muungano ambaye ndiye alipewa mamlaka ya kusimamia Tanganyika katika kipindi cha mpito kuelekea katiba mpya, alitakiwa arudi katika "Sheria zilizokuwepo Tanganyika", au tuseme, katiba ya Tanganyika (halisi/original) ambayo ilikuwa haijafanyiwa marekebisho yaliyolenga kwa ajili ya matumizi ya masuala kumia na moja ya Muungano.

Muhimu hapa pi ni kwamba – Ingawa Rais wa Muungano pia alikuwa na kofia ya Urais wa Tanganyika katika kipindi hiki cha mpito, lakini kwa kofia ya "URais wa Tanganyika", hakuwa na uwezo au mamlaka ya kisheria katika utawala wa masuala ya muungano. Rais wa Muungano aliendesha serikali ya muungano kama rais wa muungano, sio kama Rais wa Tanganyika. Serikali ya Tanganyika na Zanzibar zilielekezwa na mkataba wa muungano kupatiwa wasaidizi wake ambao wangekuwa ni makamu wawili wa rais kutoka pande zote mbili.

Lakini kama Pius Msekwa anavyojadili katika Kitabu chake cha: "50 years of Independence: A Consice Political History of Tanzania", Tanganyika ilifutwa KWA AMRI TU.

SHERIA YA KUIFUTA RASMI TANGANYIKA

Mbali na amri (Dikrii) za kuifuta Tanganyika kwa mujibu wa msekwa ambazo tumezijadili huko nyuma, Mwaka 1967, bunge lilipitisha sheria namba 24 ambayo ilimuwezesha Rais kubadilisha neno "TANGANYIKA" na kuweka jina jipya la "TANZANIA BARA". Huu ulikuwa ni ukiukwaji wa mkataba wa Muungano kwa maana ya kwamba:

Jina la Tanganyika lilikuwa ni jina la mmoja wa washiriki katika mkataba wa muungano (1964). Jina hili halikuwa suala la muungano kwani halitajwi katika orodha ya masuala ya muungano (rejea ibara ya nne ya Mkataba wa Muungano). Kwa maana hii, haikuwa Serikali ya Muungano wala Bunge la Muungano ambayo yalikuwa na mamlaka ya kushughulikia masuala yasio ya Muungano, kwa mfano majina ya TANGANYIKA na ZANZIBAR. Badala yake, Serikali ya Tanganyika na Bunge lake (bunge la Tanganyika) ndivyo vilikuwa ni vyombo ambavyo vilikuwa na mamlaka/uwezo wa kuamua jina gani vinataka "Tanganyika Yao", ilitumie.

Tumalizie bandiko hili kwa kunukuu toka kwa Issa Shivji inayojadili jinsi gani katiba ya JMT (1977) ilivyokosa uhalali wa kisheria: Let the People Speak: Tanzania Down the Road to Neo Liberalism (2005), pag 94-95, paragraph 7:

If one was to judge by the standards of constitutionality, which are proclaimed today, our union and country has hardly had a constitutional government for the last 30 years. There were many breaches – including surreptitious manipulations of the constitution – that in reality we did not live by our constitution. We even forgot to swear by it. We, at the HILL, stopped teaching Constitutional Law in 1971 or 1972!

Itaendelea ambapo katika sehemu ya mwisho, tutajadili jinsi gani Katiba ya Kudumu ya JMT (1977), ilivyochochea badala ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza kufuatia kukiukwa kwa mkataba wa muungano (1964). Pia tutajadili mapendekezo mbalimbali juu ya nini kifanyike ili kuliepusha taifa lisiingie katika machafuko kutokana na mgogoro wa kikatiba/muungano uliodumu kwa miaka zaidi ya 30, mgogoro ambao hauna dalili ya kupatiwa ufumbuzi kufuatia CCM kuamua kuendelea kusimamia sera yake ya serikali mbili katika katiba mpya.


Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.
 
Mchambuzi
Ahsante sana kuonyesha jinsi Tanganyika ilivyotoweka.
Hakuna mahali ambapo wananchi kwa ujumla wao waliulizwa kuhusu kufutika kwa Tanganyika.

Dhana kuwa bunge lilipelekewa na kuridhia haikidhi haja ya kufanya mabadiliko makubwa kama hayo.Lakini pia hakuna mahali ambapo Tanganyika ilifutwa kwa kutumia mkataba wa muungano.

Hawa wanaosema kuna nchi ya Tanzania bara, sasa ni wakati wao waje na nyaraka za kuonyesha jinsi ambavyo Tanzania bara imezaliwa na kwamba kwanini hawaijui Tanganyika.

Hapo awali tulikuwa na makamu wawili wa Rais, kama ilivyoandikwa na Mchambuzi.
Makamu wa pili alimsaidia rais kwa mambo ya Tanganyika.
Makamu wa kwanza alikuwa ni rais wa znz ambaye ni msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya muungano.

Wale wanaosema uwepo wa shrikisho utaongeza gharama, ni wakati pia waje na kutuambia huko nyuma ilikuwaje na kama kulikuwa na ongezeko la gharama.

Labda nichangie tena kwa kusema, nembo ya taifa inayotumiwa sasa ni nembo ya Tanganyika.
Iweje mtu aseme haijui Tanganyika?

Hebu tuendelee kuangalia zaidi nyaraka zilizoekwa kwa macho mawili na angavu.
 
SEHEMU YA NNE NA YA MWISHO

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977

· Katika Sheria za katiba, Katiba hii ni Batili na Haramu

Awali tulijadili Sheria mbalimbali “haramu” na jinsi zilivyo vuruga Muungano uliokusudiwa chini ya Mkataba wa Muungano (1964). Lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba, baada ya muungano kuongozwa na Katiba ya Muda (1965) kwa miaka Kumi na Mbili (1965-1977), watungaji wa katiba ya Kudumu ya Mwaka 1977 (Viongozi wa CCM) walishindwa kutumia fursa ile adimu kurekebisha makosa yaliyojitokeza, kwa manufaa ya muungano.

Inasikitisha kuona kwamba Katiba ya JMT (1977), CCM iliamua kwa makusudi kurudisha nyuma juhudi na maendeleo ya mabadiliko ya kikatiba. Msingi wa katiba hii ulikuwa na nguzo kuu mbili:

· Mfumo wa chama kimoja cha siasa
· Muungano wa serikali mbili.

Nguzo zote hizi mbili ZIMESHAMOMONYOKA katika nyakati za sasa. Lakini pamoja na ukweli huu, bado makada wengi wa ccm wanakuwa “kichwa ngumu” kusoma na kuelewa alama za nyakati zinasema nini. Samuel Sitta, Mwenyekiti wa BLK, amenukuliwa hivi karibuni akiwaambia makada wenzake kwamba:
Serikali Tatu Hazikwepeki, CCM acheni kuwa vichwa ngumu
Cc Nape Nnauye.

Kinyume na Mkataba wa Muungano (1964) na vile vile kinyume na Katiba ya Muda (1965), katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), hakuna sehemu ndani ya Katiba hii inayosema kwa uwazi kuhusu kuundwa kwa “serikali ya Tanganyika”, lakini cha ajabu zaidi, haimpi Rais wa muungano, mtu, watu au chombo chochote madaraka au mamlaka ya kusimamia mambo ndani ya Tanganyika - mambo yasiyokuwa ya muungano. Hii ni tofauti na hali ilivyo kwa mshirika mwingine wa muungano – Zanzibar. Pamoja na mapungufu haya, bado makada wa CCM, tena wengine wakiwa ni vijana wenye nafasi katika vyombo vya maamuzi ya chama, wanaikana Tanganyika waziwazi, huku wakijenga hoja jinsi gani Katiba ya sasa (1977) ni katiba yenye misingi bora ya utawala, na yenye manufaa kwa wananchi. Wakiulizwa – je hayo ni manufaa kwa wananchi wepi? Je ni manufaa yepi chini ya mfumo wa serikali mbili – kijamii na kiuchumi? Ni kawaida ya makada hawa kukimbia mijadala. Ni vigumu kubaini umma utawaamini vipi katika ujenzi wa Tanganyika mpya, Tanganyika ambayo vijana hawa wameamua kuikana.

Tatizo la Katiba ya Muungano (1977) kutoituambua Tanganyika limekuwepo kwa miaka zaidi ya thelathini, bila ya bidii au juhudi zozote hata kwa kizazi kipya cha uongozi ndani ya chama kusahihisha kosa hili. Matokeo yake, kwa akili za wananchi wengi, suala hili limekuwa likichukuliwa kijuu juu tu kama vile lilikuwa ni kosa la bahati mbaya wakati kiukweli ni kwamba hali hii ni matokeo ya jitihada za makusudi kabisa za kuifuta Tanganyika moja kwa moja. Pengine, ingeeleweka kwa wengi iwapo pia upande wa pili (Zanzibar) nao ungefuta utambulisho wao ndani ya muungano moja kwa moja kama ilivyotokea kwa upande wa Tanganyika. Sio vinginevyo.

Chini ya mazingira ya sasa (Katiba ya 1977), Rais wa Muungano na Serikali ya Muungano vinaendelea kuwa vyombo vikuu vinavyohusika na uendeshaji wa Tanganyika, na kazi hii imekuwa ikifanyika kwa miaka hamsini sasa – yani tokea Aprili 1964. Chini ya Mkataba wa Muungano (1964) na Katiba ya muda (1965), tuliona jinsi gani vyombo hivi viwili (Rais wa Muungano na Serikali ya Muungano ) vilipewa madaraka ili kutekeleza jukumu hilo, lakini cha ajabu ni kwamba madaraka hayo hayakutengwa kwa vyombo hivyo na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), pale katiba hii ilipoanza kufanya kazi ili vyombo hivi viweze kusimamia na kuendesha Tanganyika katika MASUALA YASIYOKUWA YA MUUNGANO.

Je – Madhara Yake Yamekuwa ni Yepi?

· Kwanza, ni madhara ya KISHERIA NA KIKATIBA. Hatua zozote ambazo MaRais wa Muungano na Serikali ya Muunganow amekuwa wakizichukua kuhusu mambo yote yasiyo ya muungano (hivyo ya Tanganyika) kwa miaka 37 sasa - (1977 – 2014), hatua husika zimekuwa hazina nguvu za kisheria, achilia mbali nguzu za kikatiba.

· Pili, ni madhara KISIASA NA KIDEMOKRASIA. Hatua zote, Maamuzi yote, na Matendo yote ya Marais wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Muungano kwa miaka zaidi ya thelathini, yamefanya hali mbela ya wananchi ionekane kwamba – TANZANIA NI TANGANYIKA NA TANGANYIKA NI TANZANIA. Hili ndio koti ambalo Tume ya katiba imependekeza kwamba livuliwe sasa kwa manufaa ya muungano uliopo.

Madhara haya ya pili - yamefanya baadhi ya watu kujenga hoja kwamba, tena kwa kujiamini kwamba – “hakuna haja ya kuwa na serikali zaidi ya moja kwa nchi nzima. Aidha tuendelee na serikali mbili, au tuwe na moja.”

Tunakumbuka hoja ya G55 ilipotinga Bungeni mwaka 1994, hoja ambayo kama ingefanyiwa kazi, basi bila ya shaka tungesahihisha makosa mengi ya kikatiba yaliyojitokeza huko nyuma. Lakini kama kawaida, “sikio la kufa huwa halisikii dawa”, kama kawaida yake, CCM ikaamua kupuuzia tatizo hili. Lakini ilikuwa bayana kwamba kwa kufanya hivyo, CCM haikuwa imetoa tiba ya tatizo, badala yake, tatizo hili likaishia tu kuweka chini ya “zulia”. CCM imeshindwa kabisa kutumia fursa, kila zilipojitokeza, kurudisha mkondo wa maendeleo ya Katiba katika taifa letu, hivyo kuibuka kama kinara wa harakati hizo.Badala yake, leo CCM inazidi kujionyesha, tena wazi wazi kwamba chama hiki ni “kinara wa kurudisha nyuma mkono wa maendeleo ya katiba katika taifa letu.”

TUJIKUMBUSHE JUU YA UAMUZI WA KUZIMA HOJA YA G55

Hoja ya G55 ilizimwa kwa hoja kwamba BUNGE na RAIS havikuwa na mamlaka ya kuchukua hatua husika. Cha ajabu ni kwamba, wengi ndani ya CCM, ikiwa ni pamoja na waziri wa sheria na katiba wa wakati ule (Samuel Sitta), ambae alishaanzisha mchakato wa kura ya maoni juu ya Tanganyika, wakakubaliana na hoja hii. Swali linalofuatia ni je:

· Ni wapi katika Mkataba wa Muungano (1964), Chama Cha Siasa, kiwe TANU au CCM, kimetajwa kuwa na mamlaka ya kufanyia maamuzi suala la Tanganyika?

· Na katika hali ya sasa, Chama kinapata wapi mamlaka na madaraka ya kuingilia mambo ya kikatiba nchini katika zama hizi za mfumo wa vyama vingi vya siasa?

CCM inataka kujenga mazingira ya hatari ndani ya taifa letu.

· Taifa letu litakuwa linaelekea wapi ikiwa Vyama Vya Siasa, tena bila ya nguvu za kisheria wala Kikatiba vitakuwa vinaingilia katika mwenendo wa kikatiba nchini?

Taifa lipo katika hatari ya kuingia katika machafuko makubwa sana. Kwa uchache wetu, ingawa tunasemwa kwamba hatuna nia njema na chama na muungano kwa ujumla, bado tunajitahidi na tutaendelea kujitahidi kushauri nini kifanyike, kwa maslahi ya taifa, na hata ya CCM yenyewe. Bila ya uangalifu, CCM itaingiza taifa letu katika mtafaruku mkubwa sana, na waathirika watakuwa sio tu wananchi wa leo, bali na vizazi vyao vya baadae.

Inaendelea bandiko linalofuata...
 
Last edited by a moderator:

KATIBA YA JMT (1977) NA UCHAKACHUAJI WA MKATABA WA MUUNGANO (1964).

Katiba ya JMT (1977), katika ibara ya kwanza juu ya “kutangazwa jamhuri ya muungano inasema kwamba”:
Tanzania ni Jamhuri Huru iliyoungana

Kinacho kusudiwa kuelezwa hapa ni kwamba – “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Jamhuri ya Mamlaka Zilizoungana.” Lakini kama tulivyokwisha ona, Mkataba wa Muungano (1977), haukusema kwamba jina rasmi litakuwa ni “Tanzania”, bali “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar”. Ni kupitia katiba hii ya (1977), utambulisho huu ukabadilishwa na kuwa “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. Wananchi wanahitaji kufahamu jina sahihi la muungano ni jina gani, na kwa kufanya hivyo, ndiyo tutaweza kukumbushwa juu ya mizizi na asili ya Muungano uliopo. Hili litawezekanika iwapo Mkataba wa Muungano (1964), utawekwa wazi kwa wananchi.

Tukiangalia ibara ya 2(1) ya Katiba ya JMT (1977), ibara hii inataja juu ya nchi ambazo zilikubali kuja pamoja na kuungana kuwa ni “Tanzania Bara na Zanzibar”. Kama tulivyojadili awali, Tanzania Bara ni jina lililoletwa kufuatia AMRI kwamba jina la Tanganyika lifutwe, AMRI! Lakini mbali ya kukusudia kuinyima Tanganyika utambulisho wake ambao uliheshimika ndani ya Mkataba wa Muungano (1964) na Katiba ya Muda (1965), bado maana inayopatikana chini ya katiba ya sasa (1977) ni sawa na ile ile iliyokusudiwa na jina rasmi lililokubaliwa mwaka 1964, yani – “ Jamhuri Ya Muungano Ya Tanganyika na Zanzibar”. Awali tulijadili kwamba waliobadilisha jina la Tanganyika kuwa Tanzania Bara hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.

Ni muhimu tukafahamu kwamba pia jina la Zanzibar lilichakachuliwa katika katiba hii ya JMT (1977), ambapo jina hili (Zanzibar) lilibadilishwa na kuwa “Tanzania Visiwani. Hivyo katiba ya JMT (1977) ikasomeka hivi:

Muungano baina ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani

Kilichorudisha jina la Zanzibar katika katiba yake ilikuwa ni jitihada za utawala wa mzee Aboud Jumbe, ambapo kwa hoja ambazo zilikuwa wazi kabisa, kitendo cha kufuta utambulisho wa Zanzibar uwe “Tanzania Visiwani”, kilikuwa ni kinyume cha Mkataba wa Muungano (1964). Kwahiyo mshirika mmoja wa Muungano (Zanzibar) akafanikiwa kurudisha utambulisho wake kwa mujibu wa mkataba wa muungano (1964), lakini mshirika mwingine wa muungano (Tanganyika) ambayo ilifutwa kwa amri, na baadae amri hizi kutekelezwa kupitia sheria namba 24 ya 1967, na kuzalisha jina jipya la “Tanzania Bara”, mshirika huyu bado hajaweza kurudi katika hali inayotajwa na Mkataba wa Muungano (1964).

Tume ya katiba imejaribu kurekebisha makosa yaliyojitokeza huko nyuma, kwa maslahi ya muungano uliopo. Lakini, badala ya CCM kutumia fursa iliyopo kuokoa muungano na pia chama chenyewe (CCM), kwa kuazima lugha ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba - Samuel Sitta, CCM imeamua kuwa “Kichwa Ngumu”. Tume ya Katiba ilipendekeza yafuatayo baada ya kujiridhisha na maoni ya wananchi walio wengi:

SEHEMU YA KWANZA: Jina, Mipaka, Alama, Lugha na Tunu Za Taifa.
(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi na shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, ambazo kabla ya hati ya makubaliano ya muungano, 1964, zilikuwa nchi huru.

(3) HATI YA MAKUBALIANO YA MUUNGANO iliyorejewa katika ibara ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na katiba hii, kwa kadri itakavyo rekebishwa, itakuwa ni muendelezo wa makubaliano hayo.

Badala ya maneno haya kuwa ndio kichocheo kwa wawakilishi wetu ndani ya BLK kurekebisha kasoro za huko nyuma, lakini pia kwa wale wa upande wa Tanganyika kutumia fursa hii “kuizindua Tanganyika”, leo tunashuhudia jinsi gani maneno haya yamezua kizaa zaa Dodoma, na kufikia hatua hata ya nyaraka za muungano kuchakachuliwa, ili mradi tu, muungano uendelee kuishi na kasoro zilizofanyika huko nyuma. Kama tunavyojua, popote palipo na Kasoro, lazima kuna watu/upande unaofaidika kutokana na uwepo wa kasoro husika, lakini pia wapo watu/upande unaoumizwa na kasoro husika. Swali linalofuatia ni je - CCM inalenga kumnufaisha nani? Kwa gharama za nani?

Hatimaye, BLK limefikia hatua ya kuhairishwa, kwa sababu tu, CCM imekataa kurudi katika asili na mizizi ya muungano wetu.

itaendelea ambapo tutajadili:

*Makosa ya msingi ndani ya katiba ya JMT (1977) yanayohataisha uhai wa muungano.
*Dhana ya CCM kushika hatamu kupitia katiba ya JMT (1977), na jinsi gani suala hili limeathiri sana matumaini ya Tanganyika, na afya ya muungano uliopo kwa ujumla.



Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.
 
KATIBA YA JMT (1977) NA UCHAKACHUAJI WA MKATABA WA MUUNGANO (1964).

Katika bandiko lililotangulia tulijadili baadhi ya kasoro za waziwazi zilizomo ndani ya Katiba ya JMT (1977), hasa jinsi katiba hii ilivyo kiuka mkataba wa muungano (1964), pamoja na athari zilizo jitokeza.

MUSWADA WA KATIBA YA JMT (1977).

Muswada wa Katiba ya sasa (1977) ulipelekwa bungeni asubuhi ya tarehe 25 Aprili, 1977, na ukapitishwa kuwa sheria jioni ya siku hiyo hiyo, na kuwa Katiba ya Kudumu Ya Jamhuri Ya Muungano. Mbali ya Katiba hii kukiuka maelekezo ya mkataba wa muungano, 1964), muswada huu ulipitishwa bila ya kuwashirikisha wananchi ili upate maoni yao.

Katiba ya JMT (1977) ina makiuko mengi, lakini muhimu kuliko yote ni lile linalohusu Tanganyika, kama vile:

· Katiba hii kutoweka wazi suala la uendeshaji wa Serikali ya Tanganyika.
· Katiba hii kutoweka vifungu vinavyozungumzia masuala ya kifedha kwa ajili ya Serikali ya Tanganyika.
· Katiba hii kuruhusu Chama (CCM) kuwa mamlaka juu ya Tanganyika kwa sera, itikadi na utashi wa chama, badala ya kwa mujibu wa Sheria na Katiba inayoitambua Tanganyika kama moa ya nchi shiriki ya muungano wa 1964.
· Katiba hii kuhalalisha jina la "Tanzania Bara" kuchukua jina la "Tanganyika".
· Na Pia Katiba hii kuhalalisha Jina la "Zanzibar" kuwa "Tanzania Visiwani" kabla ya Zanzibar kudai utambulisho wake kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano (1964), na Zanzibar kufanikiwa kurudisha hadhi na utambulisho wao kupitia katiba ya Zanzibar.

Awali tuliona kwamba, chini ya Mkataba wa Muungano (1964), ilikubaliwa kwamba hadi pale katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano itakapopatikana na kupitishwa na bunge, Katiba ya Tanganyika ndiyo itakayotumika kwa ajili ya muungano, lakini kwa masharti kadhaa, muhimu likiwa ni pamoja na:

Katiba Ya Tanganyika ieleze juu ya uwepo wa SERIKALI YA ZANZIBAR Ndani ya Muungano.

Chini ya makubaliano ya Mkataba wa Muungano (1964), pia ilikubaliwa wamba katika kipindi hicho cha mpito cha mwaka mmoja kuelekea mchakato wa katiba mpya (tarehe 26 Aprili 1964 hadi tarehe 26 Aprili 1965) Jamhuri ya Muungano pia isimamie Tanganyika (katika kipindi cha mpito tu ). Suala hili lipo wazi katika ibara ya (4) ya mkataba wa muungano (1964).

Ibara ya (2) ya mkataba wa muungano (1964) iliweka wazi kwamba:
Katika kipindi cha kuanza kwa muungano mpaka baraza la kutunga katiba lililotajwa katika ibara ya (7) litakapokutana na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano (kuanzia hapa kitaitwa kipindi cha mpito), jamhuri ya muungano itaongozwa kwa masharti ya ibara ya (3) mpaka (6)
Rejea bandiko #1 kwa maelezo zaidi juu ya Mkataba wa Muungano (1964).

Mbali ya Mkataba wa Muungano kuelekeza hayo, pia Katiba ya Muda (1965), katika ibara yake ya 12(1) ilisema kwamba:

Mamlaka yote ya serikali juu ya mambo ya muungano kuhusu na mengine ya Tanganyika yamewekwa chini ya Rais.

Katika hili, tulijadili kwamba kwa mujibu wa mkataba wa muungano (1964), mamlaka ya Rais juu ya masuala ya Tanganyika yalihusisha kofia ya Rais wa Muungano tu, mamlaka hayo hayakuhusisha kofia ya Urais wa Tanganyika. Kwa maana nyingine, mambo ya Tanganyika yasiyo ya muungano yalielekezwa yasimamiwe na Rais kwa kofia yake ya URAIS WA MUUNGANO, sio URAIS WA TANGANYIKA. Na ikaelekezwa kwamba (rejea ibara ya 3b na 4a ya Mkataba wa Muungano, 1964), kama itakavyofanyika kwa Zanzibar, Tanganyika itapatiwa makamu wake wa Rais ambae ndiye atakayekuwa msaidizi wa Rais wa Muungano katika kusimamia masuala ya Tanganyika tu (masuala yaliyosalia nje ya yale kumi na moja ya muungano). Mkataba wa Muungano ukaelekeza pia kwamba "Sheria zilizokuwa Tanganyika kabla ya Muungano ziendelee kutumika katika masuala ya Tanganyika yasiyokuwa ya Muungano".

Kufuatana na maelekezo haya ya Mkataba wa Muungano (1964), ilitarajiwa kwamba ndani ya mwaka mmoja, sheria za kudumu zingechukua nafasi ya sheria hizi za muda/dharura – juu ya masuala yote yasiyokuwa ya muungano kwa pande zote mbili yani – Tanganyika na Zanzibar – kwa maana ya kwamba, Katiba ya Muungano ingepatikana kwa mujibu wa ibara ya (7) ya mkataba wa muungano (1964), Katiba ya Tanganyika ingerekebishwa ili itambue serikali ya Zanzibar (rejea ibara ya 3a ya mkataba), na Katiba halisi ya Tanganyika itaendelea kutumika katika masuala ya Tanganyika yaliyopo nje ya masuala ya Muungano. Kwa maana nyingine, kama ilivyo kwa upande mmoja wa muungano - Zanzibar, upande mwingine wa Muungano - Tanganyika nao ulistahili kupewa haki zake za kusimamia na kuendesha mambo yasiyo ya muungano juu na kuhusu Tanganyika tu.

Badala ya Muungano masharti haya kuanza kutekelezwa ndani ya kipindi cha mpito kama Mkataba wa muungano ulivyoelekeza, ili Muungano ujipatie Katiba yake ya Kudumu kwa masharti ya ibara ya (7) ya mkataba wa muungano (1964), tunaona ibara hii ikichakachuliwa kupitia "sheria namba 18 ya mwaka 1965", Sheria ambayo ililenga kuchakachua ibara ya (7) ya Mkataba wa Muungano (1964). Ni Sheria hii ndio ilipelekea Muungano kuishi chini ya Katiba ya Muda kwa kipindi kisichojulikana. Tukumbuke kwamba "Sheria namba 18 ya 1965", ni moja ya nyaraka zilizowasilishwa Dodoma hivi karibuni. Tukumbuke kwamba Nyaraka hii ni batili, na ubatili wake hautokani na sababu ya "saini zake kuchakachuliwa", bali ni kwa sababu lengo la Nyaraka hii lilikuwa ni kuichakachua ibara ya (7) ya Mkataba wa Muungano (1964), moja ya ibara muhimu, kama sio ibara muhimu kuliko zote ndani ya Mkataba wa Muungano.

Wajumbe wa Bunge la Katiba na wananchi kwa ujumla inapaswa waelewe kwamba – kuruhusu sheria hii iwe ni sehemu ya mjadala wa kuboresha muungano itakuwa ni kosa kubwa sana kwani moja ya malengo ya sheria, lakini hasa sheria namba 22 ya mwaka 1964 ambayo pia imewasilishwa Dodoma, yalikuwa ni kuupoteza mkataba wa muungano (1964), ili sheria hizi (hasa sheria namba 22) iwe ndio nguzo kuu ya muungano kisheria – badala ya mkataba wa muungano.

Baada ya Muungano kuishi chini ya Katiba ya Muda (1965) kwa miaka kumi na mbili, ndipo TANU ikaona kwamba sasa mazingira ya kuandika katiba ya Kudumu yalikuwa mazuri kwa chama na hii ilikuwa ni mwaka 1977, muda mfupi baada ya vyama vya TANU na ASP kuungana na kuzaa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tofauti na Mkataba wa Muungano (1965) na pia tofauti na Katiba ya muda (1965), Katiba ya JMT (1977) iliingiza vifungu ambavyo havikuitambua kabisa Tanganyika. Kwa mfano, ibara 11(1) ya katiba ya JMT (1977) ikasema kwamba:

Mamlaka ya serikali ya Jamhuri ya muungano kuhusiana na jamhuri ya muungano na mambo yote ya muungano yanawekwa kwenye mikono ya rais.

Lakini kwa upande wa Zanzibar, ibara ya 102(1) ikasema kwamba:

Kutakuwa na serikali ya Zanzibar itakayojulikana kama "Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar", ambayo itakuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya muungano kwa mujibu wa masharti ya katiba hii

Pia tukitazama jinsi gani Katiba ya JMT (1977) inavyotoa mamlaka ya kutunga sheria, tunaona wazi kabisa kwamba Tanganyika iliachwa, kinyume na masharti ya Mkataba wa Muungano (1964) kama tulivyokwisha jadili. Kwa mfano, suala la mamlaka ya kutunga sheria kwa jamhuri ya muungano ibara ya (50 inasema:

Mamlaka ya kutunga sheria juu ya mambo yote ya muungano katika jamhuri ya muungano, yatakuwa mikononi mwa bunge.

Katika suala hili, Tanganyika haitajwi, lakini Zanzibar inatajwa. Kwa mfano, juu ya Zanzibar, ibara ya 106 (3) inasema kwamba:

Madaraka yote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
.

Tumeona jinsi gani Mkataba wa Muungano (1964) unaitambua Tanganyika kama mshirika mwenza wa muungano, na inaelekeza mfumo wa serikali tatu, sasa kwanini katiba ya JMT (1977) inamwacha mshirika mwenza wa muungano YATIMA? Katiba hii ilitakiwa pia iseme hivi:

Madaraka yote ya kutunga sheria katika Tanganyika juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Bunge la Tanganyika
.

Lakini kinyume cha haya, katiba ya JMT (1977) haisemi lolote juu mamlaka ya utungaji wa sheria kwa Tanganyika kwa mambo yote yasiyokuwa ya muungano. Kwanini iwe hivi kwa Tanganyika na sio kwa Zanzibar?

Inasemekana kwamba mapendekezo ya CCM juu ya rasimu ya kariba ni pamoja na kuanzishwa kwa Baraza la wawakilishi la Tanzania Bara ili liende sambamba na uwepo wa baraza la wawakilishi la Zanzibar ndani ya muungano. MaSwali ya kujiuliza ni je:

*Ina maana kwamba CCM haikuona hili ni tatizo tangia mwaka 1977?

*Je, kwa CCM kukubali uwepo wa chombo cha kutunga sheria kwa upande wa Tanzania bara kama ilivyo kwa Zanzibar, uamuzi huu utakuwa na manufaa gani iwapo Tanzania Bara haitakuwa na serikali yake kwa ajili ya kusimamia na kutekeleza sheria za Tanzania Bara zisizohusu masuala ya muungano kama ilivyo kwa zanzibar?


Bandiko linalofuata litahitimisha mada hii...
 
DHANA YA CCM KUINGILIA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO

Utamaduni wa CCM kuingilia masuala ya Muungano, hivyo katika ya Jamhuri sio mgeni kwani ulianzia ndani ya Katiba ya Muda (1965), kitendo ambacho kilikuwa ni kinyume na masharti yaliyowekwa ndani ya mkataba wa muungano (1964).

CCM (TANU Kwa Kuanzia), ilijihalalishia mamlaka haya mwaka 1965, kupitia "Sheria ya Baraza la Kutunga Katiba ya mwaka 1965). Lengo la sheria hii ilikuwa ni kukipatia Chama Mwanya wa kufanya katiba ya Chama (TANU) kuwa ni sehemu ya katiba ya Muungano. Sheria hii ilikuwa ni kinyume na Mkataba wa Muungano (1964), kama tutakavyojadili punde.

Awali tulijadili kwamba Mkataba wa Muungano (1964) haukutaja maneno "chama au vyama vya siasa", na wala haukutaja "TANU, ASP, au CCM". Tunaweza kuthibitisha ukweli huu kwa kuangalia Mkataba wa Muungano (1964), ibara kwa ibara, mstari kwa mstari, kwenye bandiko #1 la mjadala huu. Lakini kinyume na matakwa ya Mkataba wa Muungano (1964), Katiba ya JMT (1977) ikakiuka suala hili waziwazi na kuingiza siasa za CCM ndani ya katiba ya nchi, hasa juu ya nafasi na uwezo wake juu ya taasisi za dola.

Ibara ya (3) ya katiba ya JMT (1977) ililazimisha kuingiza vitu vilivyoleta mchanganyiko (confusion) mkubwa wa Kikatiba, na katika mfumo wa serikali na utawala kwa ujumla. Ibara ya 3(2) ya Katiba ya JMT (1977) ilisema hivi:

3(2)shughuli zote za kisiasa nchini Tanzania zitaendeshwa ama na chama chenyewe au chini ya uongozi na usimamizi wa Chama.

Pia ibara ya 3(3) ikasema:
Shughuli zote za vyombo vyote vya umma katika jamhuri ya muungano zitaendeshwa chini ya uongozi na usimamizi wa Chama.

Katika kipindi hiki ambapo mchakato wa katiba mpya unaelekwa kuvurugwa na CCM, inatupasa tuelewe kwamba haikuwa ASP wala TANU ambazo zilihusika katika kuleta muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar mwezi Aprili, 1964. Badala yake, ilikuwa ni uamuzi wa marais wawili (sio wenyeviti wa vyama vya TANU na ASP).

Kwa kutumia mamlaka waliyokuwa nayo, na kwa niaba ya watu wao, viongozi hawa (marais wa jamhuri huru mbili) ndio walioamua kuunganisha nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Ndio maana katika moja ya hatua za awali kabisa walizochukua, moja wapo ilikuwa ni kuhakikisha kwamba Mkataba wa Muungano (1964) hautaji wala hauingizi maneno "vyama vya siasa" au majina ya vyama "TANU au ASP". Ni muhimu tukalitazama suala kwa maana ya kipekee, na hata katika mchakato wa sasa wa katiba mpya, suala hili ndio liwe ni msingi mkuu wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Tanzania, lakini pia Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika.

Tukiutazama Mkataba wa Muungano (1964), hatuoni sehemu inayosema "chama kushika hatamu katika muungano", lakini pia hakuna sehemu mkataba huu unasema "chama kushika hatamu Tanganyika au Zanzibar". Kama tulivosema awali, kutajwa kwa vyama vya siasa katika suala la muungano kulianza kujitokeza kwenye katiba ya muda (1965) ambapo upande mmoja wa muungano (Tanganyika), bila ya kushirikisha upande mwingine wa muungano (Zanzibar), kwanza ulipitisha "Sheria ya Baraza la Kutunga Katiba (1965)", na kuanza kuchakachua urataribu wa uliowekwa na Mkataba wa Muungano (1964, ibara ya 7) juu upatikanaji wa Katiba ya Kudumu ya Muungano. Kilichofuatia Mwaka huo huo wa 1965, ikawa ni hatua ya TANU kufanya chama hiki kuwa ni "sehemu ya Katiba ya muda ya JMT (1965)". Katiba ya Muda (1965) ilikuwa na sura ifuatayo:

SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO, CHAMA, NA WATU
SEHEMU YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO NA CHAMA

3 (1) Kutakuwa na Chama Kimoja Cha Siasa katika Tanzania.

(2) Mpaka hapo Tanganyika African Union (TANU) itakapoungana na Afro Shiraz Party (ASP) na kufanya chama kimoja cha siasa, chama hicho kwa Tanganyika kitakuwa Tanganyika African National Union (TANU) na kwa Zanzibar kitakuwa ni Afro Shiraz Party (ASP).

(3) Shughuli zote za kisiasa katika Tanzania, isipokuwa zile za vyombo vya dola ya Jamhuri ya Muungano, vyombo vya serikali na chombo cha kutunga sheria kwa Zanzibar au vya serikali za mitaa vitakavyoundwa kwa au chini ya sheria ya mamlaka inayohusika, zitafanywa chini ya usimamizi wa chama.

(4) Katiba ilionyeshwa katika Nyongeza ya kwanza ya Katiba hii itakuwa Katiba ya Tanganyika African National Union (TANU), na katiba hiyo inaweza kurekebishwa wakati wowote (na masharti yaliyomo ndani yake na baada ya muungano wa Tanganyika National African Union (TANU) na Afro Shiraz Party (ASP) kwa mujibu wa masharti yaliyomo ndani ya katiba hiyo.

Hapa tunaona kwa wazi kabisa kwamba, licha ya hatua hii ya TANU kwenda kinyume na Mkataba wa Muungano (1964), hata kwa mtazamo wa haraka haraka tu tunagundua kwamba vipengele hivi havikuwa vikilingana, na havikuwa vinakubaliana. Kwa mfano, Katiba hii ya muda (1965) inatamka kwamba Tanzania ni nchi yenye chama kimoja cha siasa (TANU), wakati ukweli wa mambo ni kwamba, Zanzibar pia ilikuwa na chama chake cha Siasa cha ASP. Kwa maana nyingine, Katiba ya Muda (1965) haikutambua chama cha ASP bali chama cha TANU kwa miaka 12 mfululizo hadi pale TANU na ASP vilipokuja ungana mwaka 1977.

Ni hali ya mgongano wa vipengele hivi ndani ya Katiba ya Muda (1965) ndiyo iliopelekea TANU na ASP kuamua kuungana. Kwa maana hii, kabla ya Muungano wa vyama hivi viwili, kwa kiasi kikubwa, ni TANU peke yake ndiyo ilikuwa inaendesha muungano kwa matakwa ya TANU kwa miaka kumi na mbili. Hili lilikuwa ni doa kubwa sana kwa muungano kwani tunaona mwaka 1984, Aboud Jumbe akiingia matatani kwa ku-challenge party's supremacy kwenye suala la muungano, huku akiweka msimamo wa muungano kurudia kwenye msingi ya mkataba wa muungano (1964), hasa juu ya muundo wa serikali tatu.

Mchakato wa Katiba ya JMT (1977) uliendeshwa kichama zaidi. Na hata ndani ya chama chenyewe, demokrasia haikuzingatiwa, kwani maamuzi yalifanyika katika ngazi za juu pekee. Katika mchakato huo, CCM ikaingia jikoni na kuendeleza uchafuzi wa hewa "kikatiba". Chama kikaunda kamati iliyokanana wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (taifa) yani (NEC), na kazi yao kubwa ilikuwa ni kushauriana juu ya hatua za kufuata juu ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, kufuatia kuungana kwa TANU na ASP. Hapo ndipo msimamo juu ya serikali mbili ukafanywa kuwa ni wa kudumu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano (1977).

Hatua hii ilikuwa ni nje ya misingi iliyowekwa na Mkataba wa Muungano (1964). Kwa mfano, tofauti na masharti ya Mkataba wa Muungano (1964) kwamba "Tume ya Katiba" na "Baraza la Kutunga Katiba", ndio iwe vyombo vya kuandaa katiba ya muungano, Katika mchakao wa katiba ya JMT (1977), kamati ya CCM ikachukua nafasi ya Tume ya Katiba, na Bunge la Muungano, likachukua nafasi ya baraza la kutunga katiba. CCM ilifanikisha kufanya uchakachuaji huu kupitia Sheria ya Baraza la Kutunga katiba (1965), kama tulivyojadili awali.

Sio tu kwamba "Sheria ya Baraza la Kutunga Katiba (1965)" ilikuwa ni kinyume cha mkataba wa Muungano (1965), lakini pia sheria hii ilikosa sifa zote za Kidemokrasia kwa maana ya kwamba - Chama (CCM) kilijinyakulia uwezo wa kuhalalisha mamlaka kutoka kwa wananchi na kuyarundika katika mamlaka ya Chama.

Kwa CCM, historia ina tabia ya kujirudia. Mchakato wa Katiba ya JMT (1977) ulitawaliwa na uchakachuaji wa Mkataba wa Muungano (1964). Kuelekea Katiba Mpya, mchakato wote umetawaliwa na uchakachuaji wa CCM. Hali hii inauweka Muungano uliopo katika hali ya mashaka makubwa sana, hasa ikizingatiwa kwamba CCM imeamua waziwazi kupuuzia maoni ya wananchi juu ya aina ya muungano ambao wananchi walio wengi wanaona unawafaa. Ni vigumu kubaini CCM inajaribu kujenga taifa la namna gani katika zama hizi za vyama vingi, hasa iwapo huko mbele kila chama kitachoingia madarakani kitaamua kuandika katiba inayokidhi matakwa ya Chama husika.

Njia pekee iliyobaki ya kudumisha na kuboresha muungano ni mfumo wa serikali tatu kama rasimu ilivyowasilisha maoni ya wananchi walio wengi. Hata kama mfumo wa serikali mbili utaboreshwa namna gani, mfumo huu utavunja muungano (tutajadili athari za mapendekezo ya CCM juu ya maboresho husika). Serikali moja pia ni suala ambalo haliwezekani kwani kwa miaka 50 sasa, upande mmoja wa muungano (Zanzibar) umekuwa ukilalamika kwamba muungano unaimeza Zanzibar kwa hoja ambazo tutazijadili pia. CCM lazima ikubali ukweli mchungu kwamba – Kamwe Zanzibar haitarudi nyuma na maamuzi yake ya Kikatiba (2010). Kilichobakia ni kwa upande wa pili wa Muungano (Tanzania Bara) kuelewa ukweli huu, hivyo kuizindua Tanganyika, kwa manufaa ya Muungano na washirika wake.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa BLK, Samuel Sitta amenukuliwa na vyombo vya harari akiwaasa wana ccm wenzake kwamba – "Serikali tatu hazikwepeki, CCM waache kuwa kichwa ngumu". Hii ni fursa pekee iliyobakia kwa Sitta kuandikwa na wanahistoria kama mmoja wa mashujaa wa Tanzania. Ikumbukwe kwamba Sitta akiwa waziri wa sheria na katiba, alishaanzisha mchakato wa Kuizindua Tanganyika baada ya hoja ya "G55" kupata Baraka za chama na serikali mwaka 1994. Kilichozuia utekelezaji wa hili ilikuwa ni CCM kuingilia suala hili kwa hoja ambazo kwa kiasi Fulani zilikuwa na mashiko kwa nyakati zile, hasa suala husika kuwa kinyuma na Katiba ya Muungano. Safari hii, hali imebadilika. Hatuna tena Serikali Mbili, Nchi Moja ndani ya muungano na kwa mujibu wa Katiba ya JMT, bali sasa tuna Nchi mbili, Serikali mbili.
Tusemezane.

Kama anavyosema Samuel Sitta - "Serikali tatu hazikwepeki, CCM waache kuwa kichwa ngumu."



Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.
 
JE NI KWELI HATI YA MUUNGANO IPO IKULU ZANZIBAR?


Mwaka jana (2013) kwenye uzinduzi wa sherehe za miaka 36 ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dr. Ali Shein alinukuliwa akisema maneno yafuatayo:

Ati wanauliza hati ya muungano iko wapi. Waje kule ikulu mimi nilipoingia nimeiona...kuna kiti kizuri na meza kwenye chumba...na wakitaka kopi nitawapeleka Umoja wa Mataifa.

Mimi nashangaa sana kuona baadhi ya watu wanataka kujua ilipo hati ya muungano lakini hawajafanya juhudi za kuitafuta kwa sababu serikali inayo, na nakala yake ipo umoja wa mataifa.

Hati ya muungano ipo pale Ikulu kuna chumba na meza inayotumika kuwekea saini anaetaka kuiona aende Umoja wa Mataifa wanayo kopi. Hakuna haja ya kuhangaika.

Cc PAUL C. Makonda


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mzee Salim Rashid, Katibu Mkuu wa Kwanza wa Baraza La Mapinduzi alitumwa kwenda ikulu Dar-es-salaam kwa ajili ya kufuatilia suala la hati ya muungano. Hii ilikuwa ni kabla ya tarehe 25 Aprili, 1964. Mzee Rashid anasema alikutana na Mwalimu ikulu na yafuatayo yakajiri:

Mwalimu: Umekuja bila kunyoa vizuri kijana, ebu chupa haraka ukanyoe ndipo urudi hapa

Mzee Rashid anasema:

Nilichupia Baiskeli na kukimbia hadi KARIAKOO nikanyoa vizuri. Niliporudi Ikulu, nilishtuka kuambiwa hafla niliyoitiwa imekwisha na viongozi wametawanyika. Nikatafuta ndege kurudi Zanzibar. Hivi ndivyo mazingira ya wakati wa kuunda muungano yalivyotengenezwa.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mzee Salim Rashid, Katibu Mkuu wa Kwanza wa Baraza La Mapinduzi alitumwa kwenda ikulu Dar-es-salaam kwa ajili ya kufuatilia suala la hati ya muungano. Hii ilikuwa ni kabla ya tarehe 25 Aprili, 1964. Mzee Rashid anasema alikutana na Mwalimu ikulu na yafuatayo yakajiri:



Mzee Rashid anasema:




Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mkuu Mchambuzi, hebu endelea zaidi, nadhani sijakuelewa vzr unachowasilisha.
 
Last edited by a moderator:
Pius Msekwa:

*Karani wa Kwanza wa Bunge.
*Mtendaji Mkuu wa Kwanza wa CCM (TANU).
*SPIKA wa pili wa bunge la jamhuri ya muungano.

Ananukuliwa na gazeti la M.A.W.I.O la tarehe 10-16 Aprili akisema:

Sitta ana lengo gani la kutilia shaka, ana lengo gani la kusema imechakachuliwa, kinachotakiwa ni HATI Original ambayo ipo ofisi ya Katibu wa Bunge, itolewe, kwanini tuendelee kuandikia mate wakati wino upo?

Kwa utaratibu ambao Msekwa anaujadili hapo juu, anayetakiwa kuagizwa awasilishe hati husika ni Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahya Hamis Hamad. Lakini hadi sasa hajaagizwa kufanya hivyo. Yahya Hamis Hamad ananukuliwa akihoji:

Mimi sijaombwa iletwe hiyo sheria, lakini huyo alisema hati ipo Zanzibar anajua ipo wapi?

Hapa tunagundua kwamba:
*Bado hakuna nia ya dhati ya kuileta hati husika mbele ya BLK.
*Kuna matatizo ya mawasiliano baina ya Mwenyekiti wa BLK na Katibu wake.
*Muda unazidi kwenda, shughuli zinakwama, fedha za walipa kodi zinateketea.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hatimaye baada ya miaka 50 ya ujanja ujanja, mkataba wa muungano ambao ndio cheti cha kuzaliwa cha muungano wa 1964 unaletwa hadharani. Huu ndio mwanzo wa siri zilizofichwa kwa miaka 50 kuwekwa hadharani. Je, hatua ya CCM kuuleta hadharani sasa hivi baada ya shinikizo kubwa italeta tofauti gani kwa ccm na muungano kwa ujumla? Katika sehemu ya utangulizi wa bandiko #1 tulisema kwamba CCM imechelewa kujinasua katika tatizo hili. Tutazidi kujadili sakata hili pale nakala ya hati hiyo itakapowekwa hadharani.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hatimaye baada ya miaka 50 ya ujanja ujanja, mkataba wa muungano ambao ndio cheti cha kuzaliwa cha muungano wa 1964 unaletwa hadharani. Huu ndio mwanzo wa siri zilizofichwa kwa miaka 50 kuwekwa hadharani. Je, hatua ya CCM kuuleta hadharani sasa hivi baada ya shinikizo kubwa italeta tofauti gani kwa ccm na muungano kwa ujumla? Katika sehemu ya utangulizi wa bandiko #1 tulisema kwamba CCM imechelewa kujinasua katika tatizo hili. Tutazidi kujadili sakata hili pale nakala ya hati hiyo itakapowekwa hadharani.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi;

Hii ni quote ya Nyerere ambayo ni signature yako"

In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU.


Hii kauli ilitolewa mwaka mmoja baada ya muungano, 1965. Kwa kuchambua hii kauli, inaonyesha wazi kabisa kuwa Tanganyika ilikuwepo mpaka 1965 na sio muungano ulioua Tanganyika. Kwani muungano ulikuwa 1964.
 
Mchambuzi;

Hii ni quote ya Nyerere ambayo ni signature yako"




Hii kauli ilitolewa mwaka mmoja baada ya muungano, 1965. Kwa kuchambua hii kauli, inaonyesha wazi kabisa kuwa Tanganyika ilikuwepo mpaka 1965 na sio muungano ulioua Tanganyika. Kwani muungano ulikuwa 1964.

Mkuu Zakumi:

Naunga mkono hoja. Kama unavyoelewa, mfumo wa vyama vingi Tanzania ulifutwa mwaka 1965, na kauli hii ya Mwalimu ilitoka katika kipindi kile kile. Source ya nukuu hii kama ifuatavyo:

Socialism and Participation: Tanzania's 1970 National Elections:The Election Study Committee, University of Dar-es-salaam (1974)

Nikirudi kwenye hoja yako ya msingi, tofauti na hoja za Viongozi kama Mizengo Pinda na wengine kwamba Tanganyika ilikoma kuwa Tanganyika mwaka 1964, hoja hii inapingana hata na Katiba ya muda (1965) ambayo bado iliendelea kuitambua Tanganyika kwa sura ile ile ya Mkataba wa Muungano (1964). Pamoja na Amri kadhaa kutolewa na Rais Nyerere kuifuta Tanganyika katika kipindi cha 1964-1965, bado hapakuwa na sheria ya kuhalalisha suala hilo hadi mwaka 1967 ambapo bunge la Muungano lilipitisha sheria namba 24 ya Mwaka 1967 ya kufuta jina "Tanganyika" na kuleta "Tanzania Bara". Lakini pamoja na hayo, katiba ya nchi iliendelea kutumia jina la Tanganyika (katiba ya muda ya JMT, 1965). This is interesting kwani katiba ya nchi ndio sheria mama za nchi. Jina la Tanganyika liliachwa rasmi (kikatiba) mwaka 1977 baada ya katiba mpya na ya kudumu ya JMT kupatikana mwaka huo (1977). Hii ilikuwa ni miaka 13 baada ya muungano. Pengine kilichofanikisha hilo ilikuwa ni muungano wa TANU na ASP kwani nje ya hapo, ilikuwa ni vigumu kufuta jina au neno Tanganyika ambayo ndio ilibeba liberation movement kama "TANGANYIKA African National Union".

Muhimu zaidi ni kwamba, tofauti na katiba ya muda (1965) kuitaja wazi Tanganyika na kutambua sheria zake na mamlaka yake, ghafla bin vu, mamlaka ya Tanganyika pamoja na sheria zake, zikawekwa gizani kupitia katiba ya JMT (1977). Kuanzia hapo, Tanganyika ikawa Tanzania Bara, na Tanzania Bara ikawa ndio TANZANIA.

Tukumbuke pia kwamba Zanzibar nayo ilifutwa na katiba ya 1977, ambapo katika nyakati tofauti iliitwa Tanzania Visiwani na Tanzania Zanzibar. Zanziba ilipopata katiba yake ya kwanza mwaka 1979, ikaanza kushughulikia uchakachuaji huu ambapo tunaona kwamba ikafanya mabadiliko ya katiba na kufuta Tanzania Zanzibar na kurudisha "zanzibar". Tanganyika haikujali sana kwani ilikuwa imevaa "joho" la muungano.
Zakumi,
Mwisho, tusisahau kwamba maneno kwenye katiba ya JMT (1977) kwamba Tanzania ni NCHI MOJA na ni jamhuri ya Muungano, maneno haya yaliletwa kupitia marekebisho ya katiba kupitia sheria namba 15 ya Mwaka 1984, baada ya sakata la Jumbe. Kwa maana nyingine, wakati katiba ya JMT inaundwa 1977, na CCM kuzaliwa, Katiba hii haikusema Tanzania ni nchi moja kwenye kipengelea cha "kutangazwa kwa jamhuri ya muungano", badala yake katiba ya 1977 awali ilisema "Tanzania ni jamhuri huru ya Muungano".

Kwa maana hii, Tanzania ilitambulika kama nchi moja kikatiba mwaka 1984, miaka 20 baada ya Muungano, miaka 30 iliyopita, na msukumo wa hili ilikuwa ni kukabiliana na nguvu ya hoja za jumbe juu ya serikali tatu.
Zakumi - sasa ni dhahiri kwamba hoja za ccm kwamba tangia 1964 Tanzania ilitambulika kama nchi moja, hoja hiyo goes to the rubbish bin. Hoja kwamba Tanganyika ilikoma mwaka 1964 pia goes to the rubbish pit, na vile vile hoja kwamba Muungano ulidhamiria serikali mbili, nayo gets flushed in the toilet kwani kwa ushahidi wa mkataba wa muungano ulioratibiwa na uliosimamia na chama hiki hiki (TANU/CCM), kwa katiba ya muda ya 1965, na ya kudumu 1977, ambazo pia ziliratibiwa na chama hiki hiki, tunaona kwamba madai yote hapo juu HAYANA UKWELI.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Zakumi:

Naunga mkono hoja. Kama unavyoelewa, mfumo wa vyama vingi Tanzania ulifutwa mwaka 1965, na kauli hii ya Mwalimu ilitoka katika kipindi kile kile. Source ya nukuu hii kama ifuatavyo:



Nikirudi kwenye hoja yako ya msingi, tofauti na hoja za Viongozi kama Mizengo Pinda na wengine kwamba Tanganyika ilikoma kuwa Tanganyika mwaka 1964, hoja hii inapingana hata na Katiba ya muda (1965) ambayo bado iliendelea kuitambua Tanganyika kwa sura ile ile ya Mkataba wa Muungano (1964). Pamoja na Amri kadhaa kutolewa na Rais Nyerere kuifuta Tanganyika katika kipindi cha 1964-1965, bado hapakuwa na sheria ya kuhalalisha suala hilo hadi mwaka 1967 ambapo bunge la Muungano lilipitisha sheria namba 24 ya Mwaka 1967 ya kufuta jina "Tanganyika" na kuleta "Tanzania Bara". Lakini pamoja na hayo, katiba ya nchi iliendelea kutumia jina la Tanganyika (katiba ya muda ya JMT, 1965). This is interesting kwani katiba ya nchi ndio sheria mama za nchi. Jina la Tanganyika liliachwa rasmi (kikatiba) mwaka 1977 baada ya katiba mpya na ya kudumu ya JMT kupatikana mwaka huo (1977). Hii ilikuwa ni miaka 13 baada ya muungano. Pengine kilichofanikisha hilo ilikuwa ni muungano wa TANU na ASP kwani nje ya hapo, ilikuwa ni vigumu kufuta jina au neno Tanganyika ambayo ndio ilibeba liberation movement kama "TANGANYIKA African National Union".

Muhimu zaidi ni kwamba, tofauti na katiba ya muda (1965) kuitaja wazi Tanganyika na kutambua sheria zake na mamlaka yake, ghafla bin vu, mamlaka ya Tanganyika pamoja na sheria zake, zikawekwa gizani kupitia katiba ya JMT (1977). Kuanzia hapo, Tanganyika ikawa Tanzania Bara, na Tanzania Bara ikawa ndio TANZANIA.

Tukumbuke pia kwamba Zanzibar nayo ilifutwa na katiba ya 1977, ambapo katika nyakati tofauti iliitwa Tanzania Visiwani na Tanzania Zanzibar. Zanziba ilipopata katiba yake ya kwanza mwaka 1979, ikaanza kushughulikia uchakachuaji huu ambapo tunaona kwamba ikafanya mabadiliko ya katiba na kufuta Tanzania Zanzibar na kurudisha "zanzibar". Tanganyika haikujali sana kwani ilikuwa imevaa "joho" la muungano.
Zakumi,
Mwisho, tusisahau kwamba maneno kwenye katiba ya JMT (1977) kwamba Tanzania ni NCHI MOJA na ni jamhuri ya Muungano, maneno haya yaliletwa kupitia marekebisho ya katiba kupitia sheria namba 15 ya Mwaka 1984, baada ya sakata la Jumbe. Kwa maana nyingine, wakati katiba ya JMT inaundwa 1977, na CCM kuzaliwa, Katiba hii haikusema Tanzania ni nchi moja kwenye kipengelea cha "kutangazwa kwa jamhuri ya muungano", badala yake katiba ya 1977 awali ilisema "Tanzania ni jamhuri huru ya Muungano".

Kwa maana hii, Tanzania ilitambulika kama nchi moja kikatiba mwaka 1984, miaka 20 baada ya Muungano, miaka 30 iliyopita, na msukumo wa hili ilikuwa ni kukabiliana na nguvu ya hoja za jumbe juu ya serikali tatu.
Zakumi - sasa ni dhahiri kwamba hoja za ccm kwamba tangia 1964 Tanzania ilitambulika kama nchi moja, hoja hiyo goes to the rubbish bin. Hoja kwamba Tanganyika ilikoma mwaka 1964 pia goes to the rubbish pit, na vile vile hoja kwamba Muungano ulidhamiria serikali mbili, nayo gets flushed in the toilet kwani kwa ushahidi wa mkataba wa muungano ulioratibiwa na uliosimamia na chama hiki hiki (TANU/CCM), kwa katiba ya muda ya 1965, na ya kudumu 1977, ambazo pia ziliratibiwa na chama hiki hiki, tunaona kwamba madai yote hapo juu HAYANA UKWELI.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi:

Thanks kwa kuongozea vizuri na kwa vithibitisho. Kwa mtu yoyote mwenye akili ataelewe kuwa kuanzia 1967-1977, kulitokea transformations za kisiasa ambazo zimesababisha muundo wa serikali wa sasa. Tanganyika iliacha kuwepo sio kwa sababu ya muungano, bali za kisiasa.

Azimio la Arusha lilitangazwa tarehe 5 mwezi wa pili siku ya kuzaliwa ASP. Azimio la Arusha lilikuwa ni la Tanganyika, na siku ya kuzaliwa kwa ASP ilikuwa haina maana yoyote Tanganyika. Lakini kwa juhudi za watanganyika wenyewe, jitihada zilifanyika za ku-align mambo ya Tanganyika na Zanzibar hili kutengeneza history.
 
Mchambuzi:

Tanganyika iliacha kuwepo sio kwa sababu ya muungano, bali za kisiasa.

Unaweza kufafanua kidogo hoja hii? Inaonekana kusheheni vitu muhimu sana kwa ajili ya mjadala.

Azimio la Arusha lilitangazwa tarehe 5 mwezi wa pili siku ya kuzaliwa ASP. Azimio la Arusha lilikuwa ni la Tanganyika, na siku ya kuzaliwa kwa ASP ilikuwa haina maana yoyote Tanganyika. Lakini kwa juhudi za watanganyika wenyewe, jitihada zilifanyika za ku-align mambo ya Tanganyika na Zanzibar hili kutengeneza history.

kama nilivyojadili kule kwenye mdahalo juu ya nini bora kati ya maboresho ya serikali mbili au azimio la arusha, bila ya kujalisha mapungufu ya azimio hili for a second, framework ya implementation zote za development policies and planning, injection ya state capital and AID katika ujenzi wa uchumi kupitia state led development, na pia provision za huduma za msingi za afya (elimu, afya, maji), framework iliyotumika katika kipindi cha 1967-1995 ilikuwa ni Azimio La Arusha. Kuanzia 1995, new framework imekuwa ni vision 2025.

Nikirudi kwenye hoja yako ya msingi katika nukuu yako hapo juu, nakubaliana nawe kwamba Azimio la arusha halikufika zanzibar. Swali linalofuatia ni je, nini ilikuwa ni madhara ya azimio kutofika kule kwa miaka 28 ya development planning nchini? In other words, Kuna hoja kwamba Tanzania bara ilirudi nyuma kimaendeleo kutokana na azimio hili (mimi na wewe -pia Nguruvi3 na wengine - tumeshajadiliana sana suala hili huko nyuma), je zanzibar ilirudi nyuma zaidi kwa kutolitambua azimio hili? Ilienda mbele? Ilibakia ilipo?

Chini ya vision 2025 as a new framework, does Zanzibar share the same vision? Why?why not?

Tukumbuke pia moja ya makosa makubwa huko nyuma kikatiba ilikuwa ni kwa katiba ya JMT kutoweka kwa uwazi masuala ya social justice and economic justice kwa wananchi ndani ya washirika wa muungano. Kwahiyo ingawa azimio declared hiki na kile kwa miaka 28, huku fedha za walipa kodi zikitumika under azimio as a framework of implementation for 28 years, social and economic justice hazikuwa zikitambulika kikatiba.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kuna hoja inayojengwa kwamba "hoja juu ya hati halisi ya muungano" sasa itakufa kwani hatimaye inaletwa bungeni. Wanaojenga hoja hii wanazidi kusema kwamba katika hili, Tundu Lissu na wengine wa upande wake wa hoja wamepatikana.

Hii sio kweli, bali badala yake, ni CCM ndio imepatikana. Imeingia katika mtego wa Lissu na haitapona katika hilo. Hii ni kwa sababu, Lissu katika uwasilishaji wa maoni ya wajumbe wachache wa kamati yake bungeni, Lissu alisema hivi:

Hata kama tukikubali, in arguendo, kwamba kile kilichopo kwenye Sheria za kuthibitisha Mapatano ya Muungano ndio hati yenyewe ya makubaliano ya muuungano, bado kuna hoja kubwa na ya msingi kwamba Hati hiyo haiwezi kuwa msingi wa shirikisho la jamhuri za Tanganyika na zanzibar tunalolipendekeza. Hii ni kwa sababu, katika miaka 50 tangu kusainiwa kwa Hati ya makubaliano ya muungano na kuzaliwa kwa muungano, Makubaliano hayo yamechakachuliwa na kuvunjwa karibu kila mahali na kwa kipindi chote cha kuwepo kwa jamhuri ya muungano. Kabla hatujaanika uchakachuaji huu, ni muhimu tuyarejee masharti yaliyomo kwenye hiyo inayoitwa Hati ya Makubaliano ya Muungano....

Lissu anaendelea kuanika masharti ya muungano na jinsi gani masharti haya yalichakachuliwa. Wiki iliyopita, tulijadili mengi ya uchakachuaji anaouzungumzia Lissu.

Kwa sasa, macho yetu yarudi katika ibara ya 1(3) ya rasimu ya katiba inayosema kwamba:

Hati ya Makubaliano...ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba hii, kwa kadri iyakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa Makubaliano hayo.

Kisha tujiulize:

*Je, serikali kutoa hati (assuming kweli ni hati halisi ya muungano), hatua hii itaboresha hoja ipi kati ya ile ya serikali mbili na serikali tatu?

*Je, hatua ya serikali kuleta hati (again assuming its authentic), is it a deliberate move on part of CCM katika ku-defend kile inachokiamini (serikali mbili), au ni mwanzo wa alternative strategy ya CCM kukubali yaishe ndani ya bunge la katiba, kisha kuhamishia nguvu za chama mitaani to campaign against serikali tatu kuelekea kura ya maoni, na ikiwezekana kuchakachua mchakato wa kura ya maoni?

Tusemezane.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom