Siri ya kuishi maisha marefu

Siri ya kuishi maisha marefu

Kula chakula vizuri kwa manufaa ya mwili ni bora lakini kuishi miaka mingi pia inategemea mazingira, tiba bora , utajiri wa nchi na bahati.

Sisi hapa tukiumwa, ujuzi wetu ni mdogo sana wa kujitibu. Kwa mfano, ukipata ugonjwa wa moyo ghafla, ni muhimu ukimbizwe hospitali. Ukiwa na kisukari, lazima utumie vidonge au insulin na kujua jinsi ya kula kama mgonjwa. Hapa, kwa mwanakijiji wa kimasikini umeshamuua. Kuna Watanzania wachache tu wana uwezo wa kwenda nje kujitiibu au wanaopata tiba ya kutosha kutokana wa uwezo mdogo. Hata ukikimbizwa Muhimbili, kama mzazi wangu alivyopata mshituko wa moyo, wanakuacha katika benchi badala ya kukutibu haraka iwezekanavyo. Ukiumwa siku za mapumziko pia ni hatari kwa Maisha yako. Hapa ndio watu wanakufa hata wakila vizuri vipi.

Pia, ukiangalia uzee kiuchumi, ni ghali mno kugharamia. Hata Japan, inahangaika kutafuta pesa za kuwahudumia wazee. Asilimia 20% ya wananchi wake wa milioni 127 wana umri zaidi ya 65 na wananchi wengi hawazai. Wafanyakazi wanalipishwa kodi zaidi ili kuwahudumia wazee.

Pia, tunaambiwa, samaki ni bora kwa mwili lakini kama unakula kwa wingi, hasa wabichi, kama Wajapani ( wanakula samaki na wali asubuhi na ni soko kubwa duniani la tuna), unapata Kansa ya tumbo kwa kuwa mazingira ya bahari ni chafu na samaki wengine wanakuwa na zebaki (Mercury).
 
Kuhusu Japan, japo wananchi wao wanaishi miaka mingi sana, vijana wao sasa wanaanza kuwa vibonge na kupatwa na magonjwa kama ya kisukari na ugonjwa wa moyo kwa kula vyakula vibaya kama vya McDonald's na pizza (trash food na high calorie) Pia, kila nchi inavyotajirika, hamna muda wa kupika nyumbani. Baba na mama wanafanya kazi na huwezi kuweka mfanyakazi nyumbani. Mwisho, wanakula processed food kwa kuwa ni rahisi kutayarisha.

Kuhusu mambo ya kujisaidia, ni vyoo vya serikali hasa shule za serikali au vijijini ndio wanatumia vyoo vya kuchuchumaa.

Choo chao ni hi-tech. Siku ya baridi kikalio unaweza kukipasha moto, maji ya kujinawisha yanatoka (moto, baridi, chemchem, kwa nguvu unayotaka) ndani katika pipe inayolenga sehemu nyeti na huna haja ya kutumia mkono.

Vyoo vingine vinakuja na radio fm na kibonyezo cha perfume. Hata flush huwa automatic ukisimama.

ImageUploadedByJamiiForums1423459953.495561.jpg

ImageUploadedByJamiiForums1423460885.429907.jpg

ImageUploadedByJamiiForums1423460903.729305.jpg
 
Back
Top Bottom