sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Watoto hufanya kile wanachokipenda ila mtu mzima kabarikiwa uwezo wa kuujua uhalisia, kubuni mipango na kuifata.
Kuna kitu muhimu ambacho hakikwepeki mimi na wewe tunapotumia pesa, si kingine bali ni "HESABU", yawezekana ni wengi tu tunazijua hesabu lakini hapa ni kuhusu kuzitumia.
Tunajiingiza katika matarizo, mawazo, umaskini, mikopo kwa sababu hatuna wito wa kufanya hesabu kabla ya kufanya miamala.
Si ajabu mtu akawa una uwezo wa kumsomesha mwanao shule za milioni 2 lakini misaada kwa ndugu ikaongezeka na hivyo kulazimika kumeta mtoto wako saint kayumba sababu ulipuuza hesabu.
Si ajabu kijana anaepokea laki 9 ya mshahara kwenda kukopa benki milioni 10 anunue gari ila akalipaki kwasababu mshahara umepungua kwajili ya makato mapya sababu alipuuza hesabu, Haiingii akilini utapata pumziko maridhawa la kuendesha gari bila stress kwa hii mbinu.
Mtu masikini wa mawazo yeye anaponunua kitu anachofikiria kinachompa tiketi ya kununua kitu ni "nina uwezo wa kununua hiki kitu (hata kwa mkopo) huku wakisahau kama wataweza kuvitunza bila stress.
Angalia hali yako jabla ya kufanya maamuzi ya fedha na sio baada ya kufanya muamala, hesabu ni hizi za kawaida tu za shule ya msingi, usiwe nyuma bali uwe mbele ya hizi hesabu.
Una miaka 30 lakini hali yako ni mbaya vile vile tangu uajiriwe ukiwa na miaka 25 na pengine ikawa mbaya zaidi, kila unaporejesha deni baada ya miaka mingi ya mateso ya marejesho unarudia tena kukopa ili ununue gari au ufanye anasa, nakwambia ya kwamba hadi uote mvi utamtafuta mchawi kumbe ni wewe.
Unaponunua vitu ambavyo huvihitaji ama havina umuhimu sana katika maisha yako basi jua kuna siku utashindwa kununua vitu muhimu utavyohitaji. hesabu nuepesi hii.
Anza kujengga tabia ya kuchukia kutumia pesa, jifunze kutengeneza pesa hata kama ni kutunza hazina, wewe kunja noti yako mara mbili irudishe mfukoni uone ndani ya mwaka umeweza kutunza ngapi, kwa maana hii achana na matumizi yasiyo na umuhimu/
Usiishi maisha ya mboga saba kwenye kipato cha tembele
Usiishi maisha ya kufurahisha wengine au kufanya ujulikane unazo, wewe una ex wako mshamalizana ya nini kujaza lita za ziada kwenye gari ili tu ujipitishe anaposhindaga akuone?