Siri ya maendeleo ya taifa masikini kuinuka

Maendeleo ya taifa yanategemea maemdeleo ya mtu mmoja mmoja.....na ifike hatua kila mtanzania ajue/apewe elimu ya pesa [uchumi] kulingana na uelewa wake yaani ile foundation...

Kila mwananchi awe na uweza wa kujua pato Lake,matumizi yake na faida yake...Mtu hajui hata kwa siku/wiki au mwezi anaingiza sh ngapi anatumia sh ngapi je, anaendesha maisha kihasara au kifaida...yupo tu kama mbuzi..!!

Embu fikira watu nane kati ya watu kumi...wanatumia zaid ya wanachotafuta[wanaishi kihasara],na watu wawili wana wanatafuta kingi zaidi ya wanachotumia[wanaishi kifaida]...afu wote wapo kwwnye nyumba moja,nini kitatokea apo..??
 
Mkuu vitu gani tumeweza fanikiwa vya kujivunia kama taifa toka uhuru ?

Mtu asiye na utashi ni ishara ya kukosa akili ndio maana hana huo utashi kama sipo Sawa katika hili naomba usahihi wake maana nipo kujifunza pia

Siku zote wenye akili huwa hawana muda na mambo ya kijinga ili nao wasionekane ni wajinga na madhara yake ndo haya "wajinga kuwa viongozi na kosa kubwa la mjinga ni kujiona mwenye akili kumbe ni mjinga tu"

Ndio maana Mwanafalsafa Plato alipendekeza nadharia ya "mfalme Mwanafalsafa (philosopher king)"; kwa maana kwamba Kiongozi lazima awe mtu mwenye akili nyingi sana.
 
Ni sahihi kuwa, siri ya mafanikio kwa nchi, taasisi, kampuni, familia na hata mtu binafsi mmoja moja, kiukweli ni moja tu; yaani kufanya kazi kwa bidii tu..

Hii kanuni iliwekwa na Mungu muumba mwenyewe alipomwambia Adam Babu yetu wote mara baada ya anguko la dhambi pale bustanini Edeni, kuwa KWA JACHO LAKO UTAKULA (tafsiri yake ni utafanikiwa, utaendelea kiuchumi, utajenga nyumba nzuri, utanunua gari au magari, utamiliki mali, nk nk)...

Na Kwa kutuhakikishia kuwa kanuni yake hii (Mungu) aliyoiweka si ya adhabu wala ya kuwafanya watu wake wajute, aliongeza kusema, "..nitabariki kazi yoyote (halali) ambayo kila mtu ataamua kuifanya kwa mikono yake..."


Kama huo ndio ukweli, ni kitu gani kinatukwamisha sisi Tanganyika kama taifa tusipige hatua za haraka za maendeleo ya kiuchumi na kijamii? Je, hatufanyi kazi kwa bidii? Mifumo ya nchi yetu kutengeneza mazingira ya watu kufanya kazi zao ni mibovu? Mfano Kuna maeneo Kwa siku mbili sasa hayana umeme!!

Shida iko wapi??
 
Mambo kama haya yanakatisha tamaa sana.

Nchi ambayo inaamua kuendelea ni ile ambayo viongozi na wananchi wanakuwa na mtazamo mmoja kwamba tunafanya kazi kwa bidii na tunanufaika wote.

Juzi kati katika mkutano wa raisi na bodi za mashirikka, akasema kuna wakurugenzi wa bodi wamepanda ndege kutoka Dar kwenda Arusha na wakati huo huo V8 VX yamewafuata Arusha kupitia barabara.

Hii nchi na zingine za Kiafrika ni ngumu kuendelea kwa sababu viongozi hawataki kuwa role models.

Viongozi wa umma hawawezi kueleweka kwa wananchi wenye akili timamu wanapowasisitiza wafanye kazi kwa bidii wakati wao wanaiba mali za wananchi.

Ninaamini asilimia 99% ya viongozi wa Tanzania wanawaza kujitajirisha wao na familia zao na kujenga mizizi ambapo familia na koo zao zitakuwa na uchumo imara miaka na miaka.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Nilipata kutoka kwenye media kwamba, enzi za ukoloni, jiji la Harare lilikuwa limepangika mpaka kuzidi baadhi ya majiji huko Ulaya, lakini leo hii Harare baada ya uhuru imechafuka kwa ujenzi holela na mabanda.

Vivyo hivyo angalia kotazi za railway zilizojengwa na mwingereza, mitaa inaeleweka, huduma za soko, shule, viwanja vya michezo nk. Leo hii kuna makazi holela nyumba nzuri lakini hakuna huduma za msingi bali zipo mbali sana.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Muhimu ni matumizi ya sayansi na teknolojia. Uwe na wazalishaji wengi kuliko walaji.
Nchi masikini hutumia watu wao waliosoma kudhibiti/kuzuia uzalishaji mali badala ya kuzalisha directly.
Punguza kazi za walaji, ongeza kazi za uzalishaji mali, hakuna zaidi ya hapo.
 
Ni kweli kabisa kwamba viongozi hutokana na jamii.
Wajinga hutoa viongozi wajinga.
Hivyo kimsingi tunahitaji watu au wananchi wenye akili nzuri ambao watasabisha viongozi wawe wenye akili nzuri kwa kutokubaliana na wajinga au wapuuzi.
 
Hatuna viongozi tuna majangili tupu
 
Ni kweli kabisa kwamba viongozi hutokana na jamii.
Wajinga hutoa viongozi wajinga.
Hivyo kimsingi tunahitaji watu au wananchi wenye akili nzuri ambao watasabisha viongozi wawe wenye akili nzuri kwa kutokubaliana na wajinga au wapuuzi.
Aibu kubwa sn
 
Tanzania hata tuchukuliwe tupelekwe huko Japan tutakula vya huko vitaisha tutabaki makapuku tena,tumezoea anasa na starehe za kuzidi uwezo kutoboa ni ngumu
Sure hata tupelekwe Marekani, kwa aina ya viongozi hawa wa hovyo tutavimaliza mapema sn hata mwaka 1 hautaisha
 
Umemaliza, tujikite katika matumizi sahihi ya fedha na rasilimali tulizonazo
 
Tanzania hata tuchukuliwe tupelekwe huko Japan tutakula vya huko vitaisha tutabaki makapuku tena,tumezoea anasa na starehe za kuzidi uwezo kutoboa ni ngumu
Tunapenda starehe kuliko kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…