Yericko,
Huijui historia ya TANU.
TAA haikuasisiwa 1927 bali 1929 na wakati ule nafasi za uongozi
hazigombewi.
Msome
Iliffe "Modern Tanzanians"
Kleist Sykes the Townsman
(
Daisy Sykes) (1973) historia nzima ya AA imeandikwa mle.
Nimekuwekea "note" ya
JV kwa
Edmund akieleza mkakati wa
Nansio kati ya
Hamza Mwapachu na
Abdul Sykes vipi wabadili
uongozi 1953.
Kuhusu uchaguzi wa 1950 uliowatia madarakani
Abdul na
Kyaruzi
msome
Listowel (1965) "The Making of Tanganyika," utajifunza
mengi na utajua kuwa juhudi kubwa ya kuwaingiza vijana hawa
madarakani ilitoka kwa
Schneider Abdillah Plantan na huyu
alikuwa mmoja wa baba zake
Abdul na aliyekuwa ametolewa
madarakani alikuwa
Mwl. Thomas Plantan kaka yake
Schneider
kwa hiyo ni baba yake mkubwa
Abdul.
Hebu soma hiki kipande na mtafute
Dr. Kyaruzi katika uongozi wa
TAA mwaka 1953 kabla TANU haijaasisiwa:
Hayo hapo chini ni kutoka kitabu changu: "The Life and Times of
Abdulwahid Sykes..." (1998):
In June, TAA headquarters announced its executive committee with
J.K. Nyerere, President;
Abdulwahid Sykes, Vice-President;
J.P.
Kasella Bantu, General Secretary;
Alexander M. Tobias and
Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary;
John Rupia, Treasurer
and
Ally K. Sykes as Assistant Treasurer.
Committee members were
Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani,
Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo
and
Patrick Aoko.[1]
Yuko
Kyaruzi hapo?
Sasa ikiwa viongozi ndiyo hao 1953 mwaka mmoja kabla ya TANU
kuasisiwa
Kyaruzi katoa mchango kutoka chama kipi na katika
mwakaupi?
Mwisho tunarudi palepale tulipoanzia na mimi kupata sababu ya
kuandika kitabu ambacho kwa miaka sasa kila uchao tunakizungumza
hapa jamvini.
Ikiwa historia ya uhuru wa Tanganyika ndiyo hii na historia ya TANU
chama cha uhuru ndiyo hii...
Imekuwaje historia ya TANU ikaja kuandikwa na ikawaacha nje wengi
wa wazalendo hawa?
Inawezekana
Yericko Nyerere akaja na jibu.
Ningependa kumweleza Yericko kuwa
Abdul alikuwa Kaimu
Rais TAA baada ya
Dr. Kyaruzi kupewa uhamisho kwenda Kingolwira
(ingawa
Yericko anasema uhamisho ulikuwa Sengerema) na alikaimu
nafasi hiyo toka 1951 - 1953.
Baada ya uchaguzi wa 1953 uliomuingiza
Nyerere madarakani kama
rais wa TAA
Abdul akawa makamu wa rais.
Unapoandika historia ya TANU na ukaanza na
Nyerere na kumtoa nje
Abdul Sykes hapo mtafiti anakuwa kajipalia makaa.
Historia hiyo haiwezi kusimama kwani mtafiti anakuwa si kama kajipunja
yeye mwenyewe bali pia kaipunja historia ya uhuru wa Tanganyika.
Jambo la kushangaza ni kuwa
Dr. Kyaruzi alipatapo kueleza kuhusu
historia yake ya siasa na akasema kuwa ilikuwa yeye ndiye aliyemwachia
Nyerere chama.
Katika makala nzima hakupata kumtaja
Abdul Sykes wala uchaguzi wa
1950 wala hakumtaja
Schneider Plantan.
Ilikuwa yeye
Kyaruzi na
Nyerere peke yao katika historia ya TANU.
Hizi ndizo historia zetu.
Wanamajlis,
Anaetaka kumjua vizuri
Dr. Kyaruzi aingie hapa:
Mohamed Said: DK. VEDASTO KYARUZI DAKTARI MWANAHARAKATI WA TAA
[1]
Tanganyika Standard, 19 th June 1953.