Aliyeamua kufanya siri mshahara huo ni Mkapa baada ya kuuongeza mshahara huo na marupurupu mara tu alipoingia madarakani hakutaka Watanzania tuujue.
Macinkus,
Kama ungeweza ku-scan na kuipost angalau some few pages ingesaidia sana kama kaushahidi wa uliyosema ili mjadala upanuke zaidi.
Macinkus,
Kama ungeweza ku-scan na kuipost angalau some few pages ingesaidia sana kama kaushahidi wa uliyosema ili mjadala upanuke zaidi.
Nakubaliana na hoja hizi.
Mishahara ya viongozi ni Kodi ya Wananchi wa aina zote. Haipaswi kuwa siri. Mishahara ni malipo kwa shughuli zilizofanyika. Kazi inaweza kupimika kwa vipimo na vigezo vinavyoweza kuwekwa na kukubalika. Iwapo na mshahara utajulikana kuna uwezekano wa kupima kama Mshahara huo unastahili kwa uwajibikiji unaohusika.
Nakumbuka nilipoingia Bungeni Mshahara wa Rais bado haukuwa siri, sielewi ni kitu gani kimetokea. Mabadiliko hayo yalitokea pamoja na kubadili pia mfumo wa uandikaji wa Vitabu vyetu vya Bajet yaani Volumes 11 hadi lV. Kwa mfumo wa sasa ambao kimsingi umefumba sana, si rahisi hata kwa Wabunge kuisimamia Serikali kama inavyotakiwa na Katiba Ibara ya 63(3).
Majadiliano haya yanatupanua wote wenye nia njema na nchi hii na ninahakika pressure itajijenga kutumia mfumo wa Bajet ulio wazi zaidi. Tukaze mwendo kudai mabadiliko mengi kuelekea Transparency katika nchi yetu. Nina hakika wote wanaofuatilia masuala ya Bunge wakati Bunge likikaa kama Kamati ya Matumizi wanaona kinachofanyika hakina tofauti na mchezo wa kuigiza.
Watanzania ni haki yenu kupata hizi Taarifa, ni wajibu wenu kuzidai. Waliobahatika kufika Zambia, Mauritius, India wanafahamu mfumo wa Bajet ulivyo 'simple' lakini very Transparent wenye kuruhusu Bunge kwa niaba ya Wananchi kusimamia.
Mathalan, Safari za Rais zinajulikana ni ngapi za mwaka, zikitokea za ziada, zinaelezwa ni zipi na kwanini ili kupata idhini ya Bunge kwa fedha zilizotumika ambazo hazikuidhinishwa na Bunge. Kwetu ukiomba hiyo ni sawa na uhaini. Ukiuliza safari za Mawaziri au kiongozi yeyote wa Serikali na hasa ukitaka ku 'tie up' safari hizo na tija inayoambatana nayo unatazamwa kama mhaini. Kuna mafungu tunayaidhinisha kwa Mabilioni bila maelezo lakini mafungu mengine hata ya Shs 2,000,000 yameonyeshwa.
Kuna swala linafungwa fungwa hasa kuhusu masuala yanayohusu majeshi yetu. Ni dhahiri kabisa hakuna mzalendo yeyote anayetaka masuala ya mikakati ya ulinzi wa nchi au ya usalama wa nchi kujadiliwa hadharani. Lakini masuala ya matumizi ya kawaida ya fedha hata kama ni jeshi au chombo chochote cha usalama hata siku moja hayatakiwi kuwa siri, kwa sababu uwizi/ubadhirifu,ufisadi yanaweza kutokea kwa kisingizio cha Ulinzi na Usalama wa nchi kumbe hoja hapa ni uhalalishaji tu wa Ufisadi mkubwa. Watanzania tunahitaji kuwa macho katika kulinda rasilimali zetu.
Fedha zinazoidhinishwa na hivyo kukusanywa kutoka kodi zetu ni nyingi sana. Ni lazima tuwe wakali katika kuzilinda ipasavyo, alimradi tunafuata taratibu za kawaida za Transparency. Tuko mbali sana na lengo hili. Kwamba hatukufuka leo haina maana kuwa hatutafika na au tusipige hatua ya kwanza kuelekea huko. Inahitaji moyo.
Ya nini tuandikie wino wakati mate yapo.......I mean mate wakati wino upo...
Pale utumishi yuko mama mmoja anaitwa mama"....". Anaweza kwenda kuchungulia na kutuambia Specific figure, sio tunagesigesi tu hapa. Maana ni lazima utakuwa umeandikwa mahali. I'll get back to you......
Wakoloni walipo ondoka Tanganyika, walituachia kitabu kilichoitwa Staff List. Kilikuwa kinachapishwa mara mbili kwa mwaka na wizara ya Utumishi. Nilicho nacho cha mwish kuchapishwa ni cha 1972. Maafisa wote wa serkiali walikuwa wanaandikwa kwenye kitabu hiki. Taarifa zifuatazo zilikuwamo: mshahara, tarehe ya kuzaliwa, ya kuajiriwa, elimu, mahali alipo, jinsia, hali ya ndoa nk. Sijui kulitokea nini baada ya hapo, kwani sijakiona tena kitabu hicho tangu kufariki kwa ofisa aliyekuwa anashughulikia uchapishaji wake (marehemu Hussein Haji). Ukurasa wa Ikulu wa mwaka 1972 kwa mfano, unasomeka ifuatavyo:
Basic Salary Appointment Name BirthDate Station Date of Appointment Remarks
Per annum marital status
48,000 President m Mwl J.K.Nyerere Dsalaam 9.12.62
M.A. LLD (Edin.) 1922
56,000 1st VP mSheikh A.A.Kaarume Zanzibar 27.4.64
48,000 Minister m A.Jumbe Zanzibar 27.4.64
of State
48,000 Minister of m Sheikh A.M.Mwinyi Dsalaam 6.11.70
State
50,000 Princ Sec m D.A Nkembo B.A. Dsalaam 13.3.56
(Lond) 28.6.30
Orodha hii ilikuwa nik kwa wizara zote.Wakati huo kulikuwa hakuna watumish hewa.
Macinkus
Nyinyi, Bunge la Tanzania, mmempa Raisi nguvu ambazo hata Mola hana.
Mmeandika sheria inayosema "Rais asilipe kodi."
Mmeandika sheria inayosema mtu hashitaki, hashitakiwi kama Raisi hapendi, kwa kupitia nguvu alizonazo juu ya DPP. Yani Raisi anaweza kuruhusu uvunjaji sheria.
Hata Mungu hajajiruhusu kuruhusu dhambi.
Raisi wa Tanzania ana nguvu wanasheria wanaziita "plenary powers." Anaweza kufanya lolote lile na huwezi kumuuliza, hata mshahara wake ni nini.
Tushukuru Mungu hajaja Dikteta muua watu hapa, kwa sababu sheria za Tanzania zingemrahisishia. Yani tuko primed, tumewiva kwa mazingira hayo ya Kidikteta japo hayajaja. Tushukuru Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete wamekuwa binadamu katika hilo. Kuna siku litakuja jitu hapa lita abuse hizi sheria.
Sio lita abuse, litatumia, hizi sheria, litaanzisha unduli hapa.
Bunge lenu lina hatia kuandika hizi sheria.
Ni wapi duniani Raisi halipi kodi?
Mkapa also received a winding-up allowance of a sum equal to the amount that would be received as salary in 24 months by incumbent President Kikwete.
The current Political Service Retirement Benefits Act, passed by the National Assembly in 2000, spells out a generous package of retirement perks for the former president, including an annual pension granted monthly of a sum equal to 80 per cent of the salary of incumbent President Jakaya Kikwete.
Furthermore, after leaving public office, he was entitled to receive a gratuity of a sum equal to 50 per cent of the total sum received by himself as salaries during his entire ten-year tenure as head of state from 1995.
Wakoloni walipo ondoka Tanganyika, walituachia kitabu kilichoitwa Staff List. Kilikuwa kinachapishwa mara mbili kwa mwaka na wizara ya Utumishi. Nilicho nacho cha mwish kuchapishwa ni cha 1972. Maafisa wote wa serkiali walikuwa wanaandikwa kwenye kitabu hiki. Taarifa zifuatazo zilikuwamo: mshahara, tarehe ya kuzaliwa, ya kuajiriwa, elimu, mahali alipo, jinsia, hali ya ndoa nk. Sijui kulitokea nini baada ya hapo, kwani sijakiona tena kitabu hicho tangu kufariki kwa ofisa aliyekuwa anashughulikia uchapishaji wake (marehemu Hussein Haji). Ukurasa wa Ikulu wa mwaka 1972 kwa mfano, unasomeka ifuatavyo:
Basic Salary Appointment Name BirthDate Station Date of Appointment Remarks
Per annum marital status
48,000 President m Mwl J.K.Nyerere Dsalaam 9.12.62
M.A. LLD (Edin.) 1922
56,000 1st VP mSheikh A.A.Kaarume Zanzibar 27.4.64
48,000 Minister m A.Jumbe Zanzibar 27.4.64
of State
48,000 Minister of m Sheikh A.M.Mwinyi Dsalaam 6.11.70
State
50,000 Princ Sec m D.A Nkembo B.A. Dsalaam 13.3.56
(Lond) 28.6.30
Orodha hii ilikuwa nik kwa wizara zote.Wakati huo kulikuwa hakuna watumish hewa.
Macinkus
Imepinda, Nyerere hakusoma M.A LLD (Edin) alisoma Economics and History.
Halafu Makerere alisomea stashahada au shahada?
The wikipedia page needs some editing, wanasema Nyerere alikuwa Mtanzania wa kwanza kusoma katika a British University, kwanza Tanzania haikuwapo, halafu hata kama unaongelea Tanzania ya leo kuna mzee wao kina Mwapachu alisoma Uingereza miaka ya 1920's.
http://en.wikipedia.org/wiki/Julius_Nyerere
Haya mafao mbona ya kawaida tu kama mtu angekuwa mwadilifu? Tatizo la huyo mzee ni kukosa uadilifu. Nyie mnataka Rais mstaafu akauze karanga ili aishi au aingie jikoni kujipikia? Give me a break! No country in the world will fail to give these to its ex-President.