Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
MIMBA
- Mimba ilitungwa baada ya baba kutoa hongo kwa kimada
- Ili kuthibitisha kama ni mimba kweli kimada akatoa rushwa kwa daktari ili apimwe harakaharaka kwa kuwa kulikuwa na msongamano wa wagonjwa
- Kila alipoenda kliniki wakati wote wa Ujauzito alitoa 'chai' ili ahudumiwe vizuri na wauguzi na madaktari
- Hata wakati wa kujifungua akatoa 'chai' kwa manesi apate huduma safi
- Baada ya kujifungua aliendelea kutoa hongo awe wa kwanza kuhudumiwa, mwanae awe wa kwanza kuchomwa sindano za Chanjo n.k.
- Mwanae akaitwa 'Precious'
- Kuandikishwa chekechekea akatoa hongo ili Precious apate nafasi katika shule nzuri kwa kuwa nafasi zilikuwa chache, Precious anaangalia
- Kuandikishwa shule ya msingi mchezo uleule, Precious anaangalia
- Tena sekondari akatoa 'Chai' kwa mwalimu wa Hisabati ili Precious apate alama nzuri
- Chuo kikuu Precious hali ikawa ngumu, akagawa uroda kwa mkufunzi ili apate alama nzuri
- Precious akagawa uroda ili apate kazi, akapata
- Precious akatishiwa mara kwa mara kufukuzwa kazi kutokana na utendaji mbovu kinga ikawa ni kugawa uroda
- Akatumia nafasi yake kwa manufaa yake binafsi
- Kwa tamaa ya vitu vya thamani kuliko mshahara wake akaendelea kupokea rushwa
- Kwa kuwa wazazi wake (baba yake) hakuwa mwaminifu katika ndoa yake (Precious ni mtoto wa kimada), naye Precious hakuona sababu ya kuwa mwaminifu ktk ndoa
- Watoto wake wote walifuata mlolongo kama wa kuzaliwa kwake
- Hata alipougua ghafla , hongo ikatumika apate huduma bora lakini Mungu alimpenda zaidi
- Walipoenda kuchonga jeneza, wakakuta kuna order nyingi ikabidi watoe 'Cha Juu' ili kuchukua jeneza lilokuwepo tayari
- Wakati wa mazishi Kwaya iliyotakiwa kuimba wakati wa Maombolezo ilikuwa na safari , ikapewa 'cha juu' ili kuahirisha safari
Kwaya ikaimba na Kumsifia Precious alivyokuwa 'mtumishi mwema wa Mungu', tena wakamwomba Mungu ampokee kwa mikono miwili , amuepushe na Moto wa milele.
Risala ikasomwa, na kusifia utumishi wake uliotukuka, tena kaacha pengo lisilozibika.
CHUKUWA UJUMBE WA NYUMBANI
- Wazazi 'huwapakaza' watoto wao matope ya dhambi toka pale mimba inapotungwa hata baada ya kuzaliwa
- Watoto wote huakisi tabia walizojifunza toka kwetu, kama wazazi (Observational Learning)
- Kama hatuwezi kuwa wawazi hasa pale kaburini hata kwa mtu aliyekufa na sifa mbaya akasifiwa basi tunahalalisha matendo mabaya aliyoyafanya marehemu.
- Ili Kupambana na Rushwa twahitaji kuanzia wakati wa Ujauzito, mtoto azaliwe bila rushwa, akue bila rushwa n.k