Siri ya thamani ya mimba

Siri ya thamani ya mimba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363



MIMBA
  • Mimba ilitungwa baada ya baba kutoa hongo kwa kimada
  • Ili kuthibitisha kama ni mimba kweli kimada akatoa rushwa kwa daktari ili apimwe harakaharaka kwa kuwa kulikuwa na msongamano wa wagonjwa
  • Kila alipoenda kliniki wakati wote wa Ujauzito alitoa 'chai' ili ahudumiwe vizuri na wauguzi na madaktari
  • Hata wakati wa kujifungua akatoa 'chai' kwa manesi apate huduma safi
Baada ya Kujifungua
  • Baada ya kujifungua aliendelea kutoa hongo awe wa kwanza kuhudumiwa, mwanae awe wa kwanza kuchomwa sindano za Chanjo n.k.
  • Mwanae akaitwa 'Precious'
Elimu kwa Precious
  • Kuandikishwa chekechekea akatoa hongo ili Precious apate nafasi katika shule nzuri kwa kuwa nafasi zilikuwa chache, Precious anaangalia
  • Kuandikishwa shule ya msingi mchezo uleule, Precious anaangalia
  • Tena sekondari akatoa 'Chai' kwa mwalimu wa Hisabati ili Precious apate alama nzuri
  • Chuo kikuu Precious hali ikawa ngumu, akagawa uroda kwa mkufunzi ili apate alama nzuri
Kazi
  • Precious akagawa uroda ili apate kazi, akapata
  • Precious akatishiwa mara kwa mara kufukuzwa kazi kutokana na utendaji mbovu kinga ikawa ni kugawa uroda
  • Akatumia nafasi yake kwa manufaa yake binafsi
  • Kwa tamaa ya vitu vya thamani kuliko mshahara wake akaendelea kupokea rushwa
Ndoa
  • Kwa kuwa wazazi wake (baba yake) hakuwa mwaminifu katika ndoa yake (Precious ni mtoto wa kimada), naye Precious hakuona sababu ya kuwa mwaminifu ktk ndoa
  • Watoto wake wote walifuata mlolongo kama wa kuzaliwa kwake
KIFO
  • Hata alipougua ghafla , hongo ikatumika apate huduma bora lakini Mungu alimpenda zaidi
  • Walipoenda kuchonga jeneza, wakakuta kuna order nyingi ikabidi watoe 'Cha Juu' ili kuchukua jeneza lilokuwepo tayari
  • Wakati wa mazishi Kwaya iliyotakiwa kuimba wakati wa Maombolezo ilikuwa na safari , ikapewa 'cha juu' ili kuahirisha safari
MWISHO
Kwaya ikaimba na Kumsifia Precious alivyokuwa 'mtumishi mwema wa Mungu', tena wakamwomba Mungu ampokee kwa mikono miwili , amuepushe na Moto wa milele.
Risala ikasomwa, na kusifia utumishi wake uliotukuka, tena kaacha pengo lisilozibika.

CHUKUWA UJUMBE WA NYUMBANI
  • Wazazi 'huwapakaza' watoto wao matope ya dhambi toka pale mimba inapotungwa hata baada ya kuzaliwa
  • Watoto wote huakisi tabia walizojifunza toka kwetu, kama wazazi (Observational Learning)
  • Kama hatuwezi kuwa wawazi hasa pale kaburini hata kwa mtu aliyekufa na sifa mbaya akasifiwa basi tunahalalisha matendo mabaya aliyoyafanya marehemu.
  • Ili Kupambana na Rushwa twahitaji kuanzia wakati wa Ujauzito, mtoto azaliwe bila rushwa, akue bila rushwa n.k
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Nimekubali mkuu! Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa ukiwa unapenda kusema maneno machafu wakati wa tendo la ndoa basi kuna uwezekano mkubwa kuzaa toto tukutu na jeuri linalopenda kutukana hovyo!
 
MziziMkavu, Bible inasema 'Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao'
Lakini Mungu alivyo mwema, hakosi kuwa na suluhisho, anaendelea 'Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu', hii inavunja ile laana ya mwanzo. Ni kweli malezi na njia anazokuzwa mtoto zinamfanya awe atakavyokuwa. Lakini kama akipata mwanga kutoka kwa jamii inayomzunguka, huenda ikamsaidia kurekebisha walipokosea wazazi na kuanza mwanzo mpya kwa ajili ya wanae!
 
Nimekubali mkuu! Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa ukiwa unapenda kusema maneno machafu wakati wa tendo la ndoa basi kuna uwezekano mkubwa kuzaa toto tukutu na jeuri linalopenda kutukana hovyo!
mhhh kama yapi hebu fafanua ni maneno gani hayo wakati wa starehe
 
Back
Top Bottom