Siri ya utajiri wa Majizzo

Hii thread imenikumbusha story mbili tofauti lakini zinazofanana,

1) Ya kwanza ni ya Diamond Platnmuz vs Bob Junior.
Hapo mwanzo Bob Junior alikua juu kiumaarufu, kimuziki na kifedha kuzidi Diamond. Hii ni kwa sababu Bob Junior alikua Producer mkali that time pia muimbaji. So kote kote anaingiza mkwanja ukichukulia pia kimuziki alikua Juu. Diamond that timealikua muimbaji underground tu but chini ya lebo ya Bob Junior, Sharobaro.

Sasa basi Bob Junior akawa anajiita Rais wa Masharobaro, na Diamond kwa kutaka kukuza jina akawa anajiita Makamu Rais wa Sharobaro na akaitangaza sana although hakumshirikisha Bob Junior. Baadae Bob Junior akaja akamaind akamtimua Diamond kwenye lebo yake na kujitangaza yeye Bob Junior ndio mmiliki pekee wa Sharobaro na hana makamu wake. Ikabidi kinyonge Diamond aunde lebo ingine ya Wasafi

Leo hii Diamond ni mkubwa kimuziki, kiumaarufu na kifedha kuliko Bob Junior ambae sina uhakika kama Sharobaro Records bado iko hai.

2) Ya pili inahusu Abubakar Sadik (a.k.a Kwa Fujo) v/s Dj Majay/Majizo
Clouds FM ilikua na Ma-DJ wenye majina wa kutosha tu. Alikuwepo Muli B, Steve B, Dj Venture, Ndugu yake Dj Bonny Luv hapo Kitambo, Dj Too Short, Dj Nelly etc. Hawa walikua wakijiita Nyuki DJs. Sasa basi kundi hili la Ma Djs wa Clouds lilitisha sana na hata kwenye makumbi ya starehe mengi makubwa ni hawa waliotikisa. Kwa kua hawa wote walikua Clouds basi Ma-Dj wa stations zingine walikua kama wakibaniwa hivi na hawasikiki zaidi ya vituo vyao.

Ndipo ikabidi waungane na wao na wakaanzisha Kwa Fujo Djs. Hili kundi lilishirikisha Abubakar Sadiki wa Radio One, Francis Ciza (Dj Majay/Majizo) aliekua Magic FM, kuna alietoka EA Radio nafikiri na wengineo. Sasa basi Majizo akiwa Magic FM miaka hiyo ya 2005 alitumia muda mwingi sana kuibeba Kwa Fujo Djs na hata kwenye kipindi chake kile cha Jioni alikua aki-scratch sana jingo ya Kwa Fujo Deeeeejjjjjaaays. Ilionekana kana kwamba Yeye sasa ndio anakua maarufu kuliko mwenye jina mwenye Abubakar Sadik ndani ya Kwa Fujo Djs mpaka ikafikia wakati ikabidi Abubakar Sadiki avunje kundi achukue jina lake. Hapo kinyonge ikabidi Majizo akubali matokeo.

Leo hii Majizo ni MMiliki wa Radio na yuko juu ki umaarufu, kifedha na pengine hata ki U-Dj wakati Abubakar Sadiki bado ni DJ anaesubiri mshahara tarehe 30
 
Mdau shark umeleta story zinazofurahisha na kufundisha kutangulia sio kufika. Enzi hizo lakini so kweli madj Wa mawingu na Wa EA radios walikuwa na bifu kweli lakini la kikazi sio kiuhalisia mtaani na maisha ya kawaida.
Kuna shindano la madj everlasting dj jd alishinda lakini mawingu walileta figisu akashinda steve mdoe alias dj skillz.

Japo dj JD akiwa the cruise alikuwa ana wa shout kina stve bizzo na wengineo wa mawingu kama " The cruise inasikilizwa na ma DJ wakali kabisa DJ skills toka pale rose garden" .
 
Umeongea point ni wivu tu unasumbua hapa majizo ameleta ushindani kwenye radio cloufs wenyw wanamuogopa na nimependa jinc anavyojiyangaza na imvestment aliofnya hasa katika mapresnter na matangazo big up bro[emoji16][emoji16][emoji16][emoji23]
 
huwezi kujua kajipangaje kila mmoja ana siri yake ya maisha hadi kufanikiwa na huwez kujua waliofanikisha mpango wake ni watu gani
 
Mkuu sijasema walikua wana bifu, wala hawajawahi kugombana hata siku moja. Nazungumzia kufunikana
 

Steve B(Dj Skills) hakushiriki kabisa hayo mashindano. Kutoka Clouds aliwakilisha Muli B pekee, na ndio alishinda akim'bwaga JD kwenye final.
 
Steve B(Dj Skills) hakushiriki kabisa hayo mashindano. Kutoka Clouds aliwakilisha Muli B pekee, na ndio alishinda akim'bwaga JD kwenye final.

This thing was rigged!
JD was n still the illest DJ kwenye taifa hili la Baba Jesca
 
Hahahaaa...... Umenikumbusha sana Nyuki dj's hasa Dj Venture na Nelly.

Though mwenda pole hajikwai.
 
SHILAWADU?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…