Unajua wao haikuwa kampuni ya uzalishaji bali ni umoja wa watanzania walioamua kukusanya mtaji na kununua hisa katika mashirika ya serikali yaliyokuwa yakiuzwa. Baada ya kupata mtaji walinunua hisa NMB, na mashirika mengine sina uhakika TBL na CRDB au TOL maana haya yaliuza hisa kabla ya NICOL kuanza. Hivyo basi kila hisa za NMB zikipanda nao zao zinapanda kwa uwiano halkadharika kama waliwekeza kwingine. Mbali ya kupanda kwa thamani ya hisa,hupata gawio la faida kwa hisa.
Ukiwa na hela ni kununua na kuitunza huko. Mfano mwaka ule hisa za TBL zilikuwa 550 kwa hisa moja. sasa hivi hisa moja ni 12,500/=. Kama unazo hisa 100 utakuwa ulitoa 55,000/= sasa ni 1,250,000/=. Hapo achilia mbali gawio la faida.