Siri ya vipaji vya kuimba ‘bafuni’ wakati wa kuoga, hasa kwa watoto na watu wazima kama wapo

Siri ya vipaji vya kuimba ‘bafuni’ wakati wa kuoga, hasa kwa watoto na watu wazima kama wapo

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Salamu kwenu Wanyabe!

Leo nimekuja na hili suala, nimekuwa nikiliona na kusikia siku nyingi japo sikuwahi kulipa umuhimu.

Basi kijana wangu mwenye kawaida ya kuimba kiustadi kila aingiapo maliwato ‘kuoga’ sio ile shughuli nyingine, leo ametia vokali kali sana kiasi cha kumkera mgeni wangu na akashindwa kujivunga.

Sijui yeye amepokeaje, kaonesha kutofurahishwa na ‘tabia’ hiyo... na kunishauri nimkanye mtoto asiimbe eti ‘chooni sio studio’.

Ndipo nikapata wasaa kulitafakari kwa upana wake, nikakumbuka kuwa sio watoto tu wanaopenda kuimba wakiwa kuoga, wapo baadhi ya watu wazima.

Hii ina maana gani.? Ni dalili ya nini, na haya ‘makatazo’ ya wazazi huenda vipaji vingi vimezimika kwa njia hiyo.?

Hebu tushirikishane tunaoshudia hii, na pia wale ambao ni mahodari wa kuimba, au wale ambao ‘walikoma’ watatupa sababu zao.

Karibuni.
 
Mwambie huyo mgeni wako ajikite kufanya yake, ya ngoswe amwachie ngoswe.

Hakika, yeye kamaliza na hana cha kufanya zaidi kaniachia mimi... ila tu kanipa tafakuri ndo hii hapa nimekushirikisheni.

Hii ina maana gani.?
 
[emoji23][emoji23][emoji23]hako kamchezo nilikuwa nakafanya sana the reason behind ilikuwaga ni sauti.

My voice is horrible sema nilikuwa nikiimba bafuni it sounds angelic.

Mama alikuwa anapiga vita sana anasema sio vizuri kuongea tukiwa huko.

Mama alikupa sababu ya zuio.?

Je, despite voice factors.... nje ya bafuni ulikuwa unaimba pia.?
 
alikuwa anaimba nyimbo za namna gani au mahadhi gani?? Kama ni mapenzi elewa kuwa alikuwa kwenye mambo yaleee lakini kama ni za dini basi jua alishakutana na malaika huko
 
Siku kama sina haraka basi ntaenda bafuni na simu kabisa kwa ajili ya kuskiliza music af nikiimba huko hua nakua na sauti flani amaizing balaa.
Tatzo nikitoka huko inakua kama sio mie dk chache zilizopita
 
alikuwa anaimba nyimbo za namna gani au mahadhi gani?? Kama ni mapenzi elewa kuwa alikuwa kwenye mambo yaleee lakini kama ni za dini basi jua alishakutana na malaika huko

Huwa anaimba nyimbo tofauti tofauti, mixer kila unaomjia kichwani... sana sana nyimbo za vijana hizi ila kuhusu mambo yetu yale huyu bado sana.
 
Siku kama sina haraka basi ntaenda bafuni na simu kabisa kwa ajili ya kuskiliza music af nikiimba huko hua nakua na sauti flani amaizing balaa.
Tatzo nikitoka huko inakua kama sio mie dk chache zilizopita

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom