Siri ya vipaji vya kuimba ‘bafuni’ wakati wa kuoga, hasa kwa watoto na watu wazima kama wapo

Siri ya vipaji vya kuimba ‘bafuni’ wakati wa kuoga, hasa kwa watoto na watu wazima kama wapo

Huwa anaimba nyimbo tofauti tofauti, mixer kila unaomjia kichwani... sana sana nyimbo za vijana hizi ila kuhusu mambo yetu yale huyu bado sana.
Yaani hayajui au? Cause aweza kuwa mtoto kwako ila kwa wengine kesha kua
 
Yaani hayajui au? Cause aweza kuwa mtoto kwako ila kwa wengine kesha kua

Hayajui, kuna umri wa kuhisia hizo mambo ila sio miaka saba... we ulianza kujichukulia ‘sheria mkononi’ ukiwa umri gani.?
 
Kuimba bafuni ni kukosa majukumu
Huna unachokiwaza kichwani huna stress zozote za maisha
Kinyume na hapo ni sehemu ya kuwaza na kuwazua
Hiyo nguvu ya kuimba itatoka wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayajui, kuna umri wa kuhisia hizo mambo ila sio miaka saba... we ulianza kujichukulia ‘sheria mkononi’ ukiwa umri gani.?
Dah! Saba mbona mzee huyo? Nakumbuka nlikuwa std 1 nikaandika barua ya kwanza ya kumtaka mapenzi
 
Salamu kwenu Wanyabe!

Leo nimekuja na hili suala, nimekuwa nikiliona na kusikia siku nyingi japo sikuwahi kulipa umuhimu.

Basi kijana wangu mwenye kawaida ya kuimba kiustadi kila aingiapo maliwato ‘kuoga’ sio ile shughuli nyingine, leo ametia vokali kali sana kiasi cha kumkera mgeni wangu na akashindwa kujivunga.

Sijui yeye amepokeaje, kaonesha kutofurahishwa na ‘tabia’ hiyo... na kunishauri nimkanye mtoto asiimbe eti ‘chooni sio studio’.

Ndipo nikapata wasaa kulitafakari kwa upana wake, nikakumbuka kuwa sio watoto tu wanaopenda kuimba wakiwa kuoga, wapo baadhi ya watu wazima.

Hii ina maana gani.? Ni dalili ya nini, na haya ‘makatazo’ ya wazazi huenda vipaji vingi vimezimika kwa njia hiyo.?

Hebu tushirikishane tunaoshudia hii, na pia wale ambao ni mahodari wa kuimba, au wale ambao ‘walikoma’ watatupa sababu zao.

Karibuni.
mzee watoto wanaendeleaje
 
Back
Top Bottom